“Somo la 17: Chakula,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 17,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 17
Food
Shabaha: Nitajfunza kuagiza chakula na kuchukua oda.
Personal Study
Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Press Forward
Songa Mbele
With God’s help, I can press forward even when I face obstacles.
Kwa msaada wa Mungu, ninaweza kusonga mbele hata wakati ambapo ninakabiliana na vikwazo.
Tunasoma kuhusu mwanamke aliyeitwa Ruthu katika maandiko ambaye alikuwa na changamoto nyingi. Mume wake alifariki, na yeye hakuwa na watoto. Mama mkwe wake, Naomi, alipanga kurudi katika nchi yake na alimwambia Ruthu abakie, lakini Ruthu alijibu,
“Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu, wako, atakuwa Mungu wangu. … [Naomi] aliona kuwa [Ruthu] amekaza nia yake kufuatana naye” (Ruthu 1:16, 18).
Ruthu alikuwa amedhamiria na alikuwa mwaminifu. Ruthu alichagua kukaa na Naomi na kuishi katika mahali pa ugeni, mbali na familia yake na utamaduni wake. Alichagua kuwa mwaminifu kwa dini yake mpya. Mambo yalikuwa magumu sana kwa Ruthu na Naomi. Walikuwa masikini sana na walisumbuka kupata chakula cha kutosha. Ruthu aliendelea kusonga mbele na kumtumainia Mungu, na alimtunza Naomi. Mungu aliona mapambano yake na alibariki juhudi zake. Baada ya muda, Ruthu aliolewa tena, alipata watoto, na alikuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya familia yake. Unaweza kumtumainia Mungu kama Ruthu Unaweza kusonga mbele kwa imani hata wakati mambo ni magumu.
Ponder
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kujihusisha na uzoefu wa Ruthu?
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kusonga mbele kwa tumaini katika Mungu?
-
Ni kwa jinsi gani hii inatumika kwa uzoefu wako wa kujifunza Kiingereza?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno haya katika maisha yako. Fikiria kuhusu lini na wapi ungetumia maneno haya.
Can I take your order? |
Naweza kuchukua agizo lako? |
What would you like to order? |
Ungependa kuagiza nini? |
I’d like … |
Ningependa … |
I’d like to order … |
Ningependa kuagiza … |
in |
katika |
on |
kwenye |
with |
pamoja na |
Nouns
beans |
maharage |
dessert |
kitindamlo |
drink |
kinywaji |
fries |
viazi vya kukaanga |
hamburger (burger) |
Hambaga (baga) |
ice |
barafu |
noodles |
tambi |
onion |
kitunguu |
pizza |
piza |
salad |
saladi |
sandwich |
sandiwichi |
sauce |
mchuzi |
soup |
supu |
spices |
viungo |
tomato/tomatoes |
nyanya/nyanya |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: Can I take your order?A: I’d like to order (noun), please.
Examples
Q: Can I take your order?A: Yes, I’d like to order beans, rice, and a drink, please.
Q: What would you like to order?A: I’d like soup and a salad, please.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kutambua mipangilio hii wakati wa mazoezi yako ya kila siku.
Q: What do you want in your (noun)?A: I want (noun) in my (noun).
Examples
Q: What do you want in your soup?A: I want noodles in my soup.
Q: What do you want with your hamburger?A: I want a drink with my hamburger.
Q: What do you want on your pizza?A: I want tomatoes on my pizza.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Fanya Igizo. Mwenza A hufanya kazi katika mgahawa. Mwenza B ni mteja katika mgahawa. Uliza na ujibu maswali kuhusu vyakula katika kila picha. Sema mengi kadri uwezavyo. Badilishaneni nafasi. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: Can I take your order?
-
B: I’d like pizza, please.
-
A: OK. What do you want on your pizza?
-
B: I want cheese, meat, and olives on my pizza.
-
A: Great. And what do you want with your pizza?
-
B: I want a drink, please.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Tazama menyu. Fanya Igizo. Mwenza A hufanya kazi katika mgahawa. Mwenza B mteja katika mgahawa. Tumia msamiati kutoka kwenye somo hili na somo la 16. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
New Vocabulary
Anything else? |
Nini kingine? |
Example
-
A: What would you like to order?
-
B: I’d like chicken, please.
-
A: What do you want with your chicken?
-
B: I want rice with my chicken.
-
A: OK. Anything else?
-
B: Yes. I’d like cake, please. Thank you!