Kujifunza Kiingereza
Somo la 18: Chakula


“Somo la 18: Chakula,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 18,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi

wanawake wakitabasamu

Lesson 18

Food

Shabaha: Nitajfunza kuelezea jinsi ya kutengeneza chakula.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: You Are a Child of God

Wewe ni mtoto wa Mungu

I am a child of God with eternal potential and purpose.

Mimi ni mtoto wa Mungu aliye na uwezekano wa kuwa na kusudi la milele.

Wewe ni mtoto mpendwa wa Mungu. Unayo thamani na uwezekano wa milele. Tunajifunza zaidi kuhusu hili kutoka katika Kitabu cha Mormoni. Tunasoma kuhusu wakati ambapo Yesu Kristo alikuwa anawafundisha na kuwabariki watu. Yeye alitumia muda kumbariki kila mtu, mmoja mmoja. Yeye alitumia muda kuwabariki na kuwafundisha watoto wao.

Yeye alipowabariki watoto wadogo, kitu fulani cha kushangaza kilitokea: [Yesu Kristo] aliwapatia uwezo wa kuongea, na waliwazungumzia baba zao vitu vikubwa na vya ajabu, … na alifungua ndimi zao kwamba wangezungumza” (3 Nefi 26:14).

Watoto wadogo walifundisha watu mambo makubwa na ya ajabu. Hawa watoto wadogo walikuwa na uwezekano mkubwa sana, na Yesu Kristo aliwasaidia kuona uwezekano wao. Mungu anaweza kukusaidia uone uwezekano wako wa kuwa. Unayo mengi sana ya kutoa. Unalo dhumuni, na Mungu anaweza kukuonyesha kile kinachowezekana wakati unapotafuta msaada Wake. Kama vile Yesu Kristo alivyowapa watoto uwezo wa kuongea, Mungu anaweza kufungua ulimi wako pia. Yeye anaweza kukusaidia kuongea. Yeye anaweza kukusaidia wewe uamini katika uwezekano wako wa milele.

Kristo pamoja na watoto

Ponder

  • Ni nini kinaweza kukusaidia wewe kuamini katika uwezekano wako wa milele?

  • Ni hofu gani inakuzuia katika kuamini kwamba wewe unaweza kuongea Kiingereza.

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kutafuta msaada wa Mungu kwa ajili ya ujasiri wa kushinda hofu yako na kuongea mara nyingi zaidi?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo.

first

kwanza

next

inayofuata

then

kisha

last

mwisho

ingredients

viambato

How do you make … ?

Je, ni kwa jinsi gani unatengeneza … ?

You need …

Wewe unahitaji …

Nouns

bread

mkate

butter

siagi

cheese sandwich

sandwichi ya jibini

egg/eggs

yai/mayai

flour

unga

oil

mafuta

oven

jiko la kuoka

pan

kikaango

stove

jiko

water

maji

Ona kiambatisho kwa ajili ya food nounszaidi.

Verbs

add

ongeza

bake

oka

boil

chemsha

cook

pika

heat

moto

mix

changanya

put

weka

Prepositions

in

ndani

on

kwenye

to

hadi

with

pamoja

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: What are the ingredients for (noun)?A: You need (noun), (noun), and (noun).

Questions

swali la mpangilio wa 1 ni nini viambato vya nomino

Answers

jibu la mpangilio wa 1 unahitaji nomino, nomino na nomino

Examples

kuchanganya siagi

Q: What are the ingredients for bread?A: You need flour, eggs, and water.

Q: What are the ingredients for a cheese sandwich?A: You need bread, butter, and cheese.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kutumia mipangilio katika mazungumzo na rafiki. Ungeweza kuzungumza au kutuma jumbe

Q: How do you make (noun)?A: First, (verb) the (noun) (preposition) the (noun).Then, (verb) the (noun) (preposition) the (noun).Last, (verb) the (noun) (preposition) the (noun).

Questions

swali la mpangilio wa 2 unatengenezaje nomino

Answers

jibu la mpangilio wa 2 kwanza, fanya kitenzi kwa nomino husisha nomino

Examples

sandwishi ya jibini ya kuchomwa

Q: How do you make bread?A: First, put the oil in the flour.Then, mix the water with the flour.Last, bake the bread in the oven.

Q: How do you make a cheese sandwich?A: First, put the cheese on the bread.Then, add the oil to the pan.Then, heat the pan on the stove.Last, cook the sandwich.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources na katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 1.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi”. Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: You Are a Child of God

(20–30 minutes)

Kristo na watoto

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu viambato vya kila chakula. Kisha, uliza na ujibu maswali kuhusu jinsi ya kutengeneza kila chakula. Chukueni zamu.

New Vocabulary

cut

kata

stir

koroga

banana/bananas

ndizi/ndizi

milk

maziwa

pot

chungu

salt

chumvi

sugar

sukari

Example

rundo la chapati za maji zilizopikwa
  • A: What are the ingredients for banana pancakes?

  • B: You need eggs, milk, bananas, and flour.

  • A: How do you make them?

  • B: First, mix the bananas with the eggs.

  • Next, add the milk.

  • Then, add the flour and stir.

  • Last, cook the pancakes in a pan on the stove.

Image 1

chungu kinachochemka juu ya jiko

Image 2

mikate miwili

ikoni 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Uliza na ujibu maswali kuhusu jinsi ya kutengeneza chakula unachopenda. Chukueni zamu.

New Vocabulary

grill

jiko la kuchomea

tortillas

totila

Example

nyama ya nguruwe na totila za unga wa ngano
  • A: What food do you like?

  • B: I like tortillas.

  • A: What are the ingredients?

  • B: You need flour, salt, water, and oil.

  • A: How do you make them?

  • B: First, mix the flour and salt.

  • Next, stir the oil and water with the flour.

  • Last, cook on the grill then, eat it.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya shabaha na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Say what ingredients are in foods.

    Sema viambato gani vilivyo ndani ya chakula.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Describe how to make foods I like.

    Elezea jinsi ya kutengeneza vyakula ninavyopenda.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Ask others how to make foods they like.

    Waulize wengine jinsi ya kutengeneza chakula wanachopenda.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mpangilio.

  4. Kufanya mazoezi kila siku.

Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Kwa sababu sisi ni watoto wa kiroho wa Mungu, kila mmoja ana chimbuko la kiungu, asili na uwezekano wa kuwa. Kila mmoja wetu ‘ni mwana au binti mpendwa wa kiroho wa wazazi wa mbinguni’ [“Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org]. Huu ndio utambulisho wetu! Hii ndivyo kweli tulivyo! (M. Russell Ballard, “Tumaini katika Kristo,” Liahona, Mei 2021, 54).