Kujifunza Kiingereza
Somo la 20: Nyumbani


“Somo la 20: Nyumbani,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 20,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi

wasichana wakiwa hekaluni

Lesson 20

Home

Shabaha: Nitajifunza kuuliza na kujibu maswali kuhusu mahali ambapo mtu fulani anaishi.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Love and Teach One Another

Pendaneni na Fundishaneni

I can learn by the Spirit as I love, teach, and learn with others.

Ninaweza kujifunza kutoka kwa Roho ninapowapenda, kuwafundisha, na kujifunza pamoja na wengine.

Wewe ni Mtoto wa Mungu. Yeye anataka kukusaidia ukue na uendelee. Yeye anataka kukusaidia ukuze uwezo mpya na ujifunze mambo mengi mazuri. Njia mojawapo muhimu ya kujifunza ni kumfundisha mtu mwingine. Wakati unapomfundisha mtu mwingine, uelewa wako mwenyewe unaweza kukua. Mungu alikupa ahadi ya ajabu.

“Na ninatoa kwenu amri ya kuwa mfundishane mafundisho ya ufalme.

“Fundishaneni kwa bidii na neema yangu itakuwa pamoja nanyi, ili mpate kuelekezwa kiukamilifu zaidi, …

“Ili mpate kuandaliwa katika mambo yote” (Mafundisho na Maagano 88:77–78, 80).

Wakati tunapofundishana na kutumikiana, tunamwalika Roho kuwa pamoja nasi. Roho anaweza kutusaidia tuelewe vyema na kujifunza haraka. Kuwafundisha wengine ni njia mojawapo ambayo Mungu huongeza uwezo wetu wa kujifunza. Wakati mwingine tunaogopa kuwafundisha wengine. Wakati mwingine hatufikirii kuwa tuna chochote cha kutoa. Lakini Mungu anajua kwamba wewe una mengi sana mazuri ya kushiriki na wengine. Wakati tunashiriki kitu tunachojifunza, ni kwamba sisi tunafundishana. Unapowafundisha wengine na kushiriki uzoefu wako, Roho atakusaidia wewe kujifunza hata zaidi.

watu watatu katika darasa la Kiingereza wakitabasamu

Ponder

  • Je, ni kwa jinsi gani kumfundisha mtu mwingine kunakusaidia wewe kuongeza kujifunza kwako?

  • Ni baadhi ya njia gani ambazo unaweza kusaidia kuwafundisha na kuwainua wale walio katika kikundi chako za EnglishConnect?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kuwekalebo kwenye vitu katika nyumba yako ili ikukusaidia wewe kukumbuka maneno ya Kiingereza.

Where do you live?

Unaishi wapi?

I live in …

Ninaishi …

Nouns 1

apartment

fleti

house

nyumba

Nouns 2

bathroom/bathrooms

bafu/bafu

bedroom/bedrooms

chumba cha kulala/vyumba vya kulala

closet/closets

kabati la nguo/makabati ya nguo

dining room

chumba cha maakuli

family room

chumba cha familia

kitchen

jikoni

living room

sebuleni

room/rooms

chumba/vyumba

stairs

ngazi

Prepositions

above

juu

across from

kuvuka kutoka

below

chini

next to

karibu na

left of/to the left of

kushoto kwa/upande kwa kushoto kwa

right of/to the right of

kulia kwa/upande wa kulia kwa

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: Where do you live?A: I live in an (noun 1).

Questions

swali la mpangilio wa 1 unaishi wapi

Answers

jibu la mpangilio wa 1 ninaishi katika nomino ya 1

Examples

jumba la gorofa nyingi la fleti

Q: Where do you live?A: I live in an apartment.

Q: Where does she live?A: She lives in a house.

nyumba iliyo na mnazi

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kusema mipangilio kwa sauti. Fikiria kujirekodi mwenyewe. Zingatia matamshi yako na ufasaha wako.

Q: Where is the (noun 2)?A: It’s (preposition) the (noun 2).

Questions

swali la mpangilio wa 2 iko wapi nomino ya 2

Answers

jibu la mpangilio wa 2 iko kihusishi nomino ya 2

Examples

ramani ya chumba cha kulala na ramani ya sakafu ya kabati

Q: Where is the closet?A: It’s next to the bedroom.

ramani ya jikoni na sakau ya chumba cha chakula

Q: Where is the dining room?A: It’s to the right of the kitchen.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 1.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi”. Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Love and Teach One Another

(20–30 minutes)

watu watatu katika darasa la Kiingereza wakitabasamu

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 pamoja na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Uliza na ujibu maswali kuhusu mahali wewe na familia yako inaishi. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.

mwanamke akimimina chai
  • A: Where do you live?

  • B: I live in an apartment.

  • A: Where is the kitchen in your apartment?

  • B: In my apartment, the kitchen is next to the living room.

ikoni ya 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Part 1

Tazama ramani ya sakafu. Uliza na ujibu maswali kuhusu mahali ambapo vyumba viko. Chukueni zamu.

ramani ya sakafu ya fleti
Example
  • A: Where is the dining room?

  • B: The dining room is to the right of the kitchen.

Part 2

Haraka chora ramani ya sakafu. weka vibandiko kwenye vyumba. Uliza na ujibu maswali kuhusu ramani ya sakafu ya nyumba Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu.

New Vocabulary

How many bedrooms are there?

Kuna vyumba vya kulala vingapi?

Is there a living room?

Je, kuna sebule?

Example
  • A: How many rooms are there?

  • B: There are two rooms.

  • A: Is there a kitchen?

  • B: Yes, there is.

  • A: Where is the living room?

  • B: The living room is next to the kitchen.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya nia na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Talk about where I live.

    Zungumza kuhusu mahali ninapoishi.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Ask and talk about where others live.

    Uliza na uzungumze kuhusu mahali wengine waponaishi.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Say where rooms are in a house or an apartment.

    Sema mahali ambapo vyumba viko katika nyumba au fleti.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mipangilio.

  4. Kufanya mazoezi kila siku.

Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Kama tunafundisha na kujifunza kwa njia ya Bwana aliyoelekeza, yeye atamtuma Roho Wake kutujenga na kutuelimisha tunapofanya hivyo” (Dallin H. Oaks, “Teaching and Learning by the Spirit,” Ensign, March 1997, 6).