Kujifunza Kiingereza
Somo la 21: Nyumbani


“Somo la 21: Nyumbani,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 21,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi

familia imekaa kwenye kochi

Lesson 21

Home

Shabaha: Nitajfunza kuelezea bafu na chumba cha kulala.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Counsel with the Lord

Shauriana na Bwana

I improve my learning by counseling with God daily about my efforts.

Ninaweza kuboresha kujifunza kwangu kwa kushauriana na Mungu kila siku kuhusu juhudi zangu.

Yesu Kristo alikuwa anafundisha kundi la watu wakati kijana alipomjia Yeye na kumuuliza alihitaji kufanya nini ili aendelee. Swali hili ambalo kijana yule aliuliza ni swali ambalo kila mmoja wetu anaweza kuuliza tunaposhauriana na Baba wa Mbinguni ili tuweze kuwa bora:

“Nimepungukiwa na nini tena?” (Mathayo 19:20).

Unaweza kuuliza swali hilo hilo katika sala. Tunasali kwa Mungu katika jina la Mwana Wake, Yesu Kristo. Kwa msaada wa Mungu, unaweza kutambua mapengo katika kujifunza kwako na kutatufa kuyaziba. Kwa mfano kama unasumbuka na kuongea kwa ufasaha, unaweza kutenga dakika 10 za kufanya mazoezi ya kuongea bila kujali kuhusu makosa. Au kama unafanya makosa mengi, unaweza kutenga dakika 10 za kufanya mazoezi kuongea pole pole na kwa umakini. Kushauriana na Bwana kunaweza kukusaidia kuelewa ni hatua gani ndogo ndogo unazohitaji kuchukua ili kufikia maelengo yako.

wanandoa wakisali

Ponder

  • Unaposhauriana na Mungu, ni mapengo gani unayaona katika kujifunza kwako?

  • Je, ni malengo gani madogo unayoweza kuweka ili kuziba mapengo haya?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kuweka vibandiko kwenye vitu katika nyumba yako ili kukusaidia kukumbuka maneno ya Kiingereza.

There is …

Kuna …

There are …

Kuna …

Nouns

bathroom/bathrooms

bafu/bafu

bathtub/bathtubs

hodhi/hodhi

bed/beds

kitanda/vitanda

bedroom/bedrooms

chumba cha kulala/vyumba vya kulala

blanket/blankets

blanketi/mablanketi

cupboard/cupboards

kabati la vyombo/makabati ya vyombo

door/doors

mlango/milango

floor

sakafu

lamp/lamps

taa/taa

mirror/mirrors

kioo/vioo

pillow/pillows

mto wa kulalia/mito ya kulalia

shower/showers

bomba la maji ya kuoga/mabomba ya maji ya kuoga

sink/sinks

sinki/sinki

toilet/toilets

choo/vyoo

towel/towels

taulo/mataulo

window/windows

dirisha/madirisha

Ona somo la 20 kwa ajili ya nounszaidi.

Prepositions

above

juu

in

ndani

next to

karibu na

on

kwenye

under

chini ya

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

A: Tell me about your (noun).B: There is (noun) in the (noun).

Request

swali la mpangilio wa 1 niambie kuhusu nomino yako

Answers

jibu la mpangilio wa 1 kuna nomino katika nomino

Examples

chumba cha kulala cheupe

A: Tell me about your bathroom.B: There is a mirror in the bathroom. There are sinks.

A: Tell me about your bedroom.B: There is a window in the bedroom. There are pillows.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kufanya shughuli ya 1 na ya 2 za kikundi cha mazungumzo kabla ya kikundi chako kukutana.

Q: Where is the (noun)?A: The (noun) is above the (noun).

Questions

swali la mpangilio wa 2 iko wapi nomino

Answers

jibu la mpangilio wa 2 nomino iko juu ya nomino

Examples

kitanda cheupe chini ya dirisha

Q: Where are the towels?A: The towels are under the sink.

Q: Where is the window?A: The window is above the bed.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources na katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 1.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi”. Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathimini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Counsel with the Lord

(20–30 minutes)

wanandoa wakisali

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila chumba Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu.

Example

chumba cha kulala kichafu kilicho na mapazia
  • A: Tell me about the bedroom.

  • B: There is a bed in the bedroom. There is a mirror next to the bed. There are clothes on the floor.

  • A: Where is the blanket?

  • B: The blanket is on the bed.

Image 1

chumba cha kulala kichafu kilicho na mapazia

Image 2

chumba cha kuoga

Image 3

chumba cha kulala

Image 4

bafu yenye vigae vya bluu na bomba la kuoga

ikoni 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Part 1

Uliza na ujibu maswali kuhusu chumba cha kulala. Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu.

New Vocabulary

big

kubwa

small

ndogo

messy

chafu

clean

safi

Example
  • A: Tell me about your bedroom.

  • B: There is a pillow on the bed. There is a blanket on the bed. There is a lamp next to the bed.

  • A: Is it messy or clean?

  • B: It is clean.

  • A: Where is the window?

  • B: The window is above the bed.

Part 2

Uliza na ujibu maswali kuhusu bafu. Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu.

Example
  • A: Tell me about your bathroom.

  • B: There is a sink in the bathroom. There is a mirror above the sink. There is a cupboard under the sink. There is a shower next to the toilet.

  • A: Is it big or small?

  • B: It is small.

  • A: Where is the towel?

  • B: The towel is next to the shower.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya shabaha na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Describe a bedroom and a bathroom.

    Elezea chumba cha kulala na bafu.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Describe where things are in a bedroom and a bathroom.

    Elezea mahali ambako vitu viko katika chumba cha kulala na bafu.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mpangilio.

  4. Kufanya mazoezi kila siku.

Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Roho Mtakatifu atatusukuma tuboreshe na atatuongoza kwenda nyumbani, lakini tunahitaji kumuuliza Bwana maelekezo tukiwa njiani” (Larry R. Lawrence, “Nimepungukiwa na Nini Tena?,” Liahona, Nov. 2015, 33).