“Somo la 23: Afya,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 23,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 23
Health
Shabaha: Nitajifunza kutaja sehemu za mwili na kusema kwa nini zinauma.
Personal Study
Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ
Tumia imani katika Yesu Kristo.
Jesus Christ can help me do all things as I exercise faith in Him.
Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya mambo yote ninapoonyesha imani Kwake.
Katika Biblia, tunajifunza kuhusu mwanamke aliyeugua kwa miaka mingi. Alitumia fedha zake zote akijaribu kupata tiba. Alikuwa ameenda kwa madaktari wengi, lakini maradhi yake yalimzidi sana. Kisha yule mwanamke alisikia kuhusu Yesu. Alimwona katikati ya umati wa watu. Aliamini Yesu alikuwa na uwezo wa kumponya. Aliamini kama yeye angegusa tu mavazi Yake, angeweza kuponywa. Alikuja nyuma ya Yesu na aligusa vazi Lake. Alihisi mwili wake ukipona. Yesu alijihisi nguvu zikimtoka mwilini Mwake. Wakati alipouliza ni nani aliyegusa mavazi Yake, mwanamke yule alikuwa na uoga kukubali kwamba ilikuwa ni yeye hapo mwanzoni, lakini kisha alikiri kwamba ilikuwa ni yeye.
Yesu alisema, “Jipe moyo mkuu, imani yako imekuponya; enenda zako na amani” (Luka 8:48).
Mwanamke huyu aliamini, na alitenda kwa Imani. Kumfikia Yesu kilikuwa ni kitendo kidogo, lakini kilileta nguvu Zake katika maisha yake. Hauhitaji kuwa na aibu au kuogopa kumwomba Mungu msaada. Yeye anataka kukusaidia. Unapoweka imani, hata katika njia ndogo, italeta nguvu ya Yesu Kristo katika maisha yako.
Ponder
-
Ni kwa jinsi gani umehisi kuimarishwa unapojifunza Kiingereza?
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia imani katika maeneo mengine ya maisha yako?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Fikiria hali ambapo ungeweza kutumia neno hili katika mazoezi yako ya kila siku.
What happened to … ? |
Ni nini kilichomtokea … |
What is wrong?/What’s wrong? |
Kuna shida gani?/Kuna shida gani? |
Nouns
arm/arms |
mkono/mikono |
back |
mgongo |
ear/ears |
sikio/masikio |
eye/eyes |
jicho/macho |
finger/fingers |
kidole/vidole |
foot/feet |
mguu/miguu |
hand/hands |
mkono/mikono |
head |
kichwa |
knee/knees |
goti/magoti |
leg/legs |
mguu/miguu |
mouth |
mdomo |
neck |
shingo |
stomach |
tumbo |
tooth/teeth |
jino/meno |
Verbs Present /Verbs Past
break/broke |
vunja/iliyovunjika |
burn/burned |
choma/aliyochomwa |
cut/cut |
kata/kata |
hurt/hurt |
umia/umia |
hit/hit |
piga/piga |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: What is wrong?A: My (noun) hurts.
Examples
Q: What’s wrong?A: His knees hurt.
Q: What’s wrong?A: My stomach hurts.
Q: What’s wrong?A: Her head hurts.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kujifunza zaidi kuhusu mipangilio katika somo hili. Fikiria kutumia vitabu vya sarufi au tovuti.
Q: What happened to your (noun)?A: I (verb past) my (noun).
Examples
Q: What happened to your finger?A: I cut my finger.
Q: What happened to his leg?A: He broke his leg.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu mtu aliye katika kila picha Chukueni zamu.
Example
-
A: What’s wrong?
-
B: Her head hurts.
-
A: What happened to her head?
-
B: She hit her head.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Fanya igizo. Mwenza A ni mtu aliye katika picha. Mwenza B ni rafiki. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila picha. Kuwa mbunifu! Badilishaneni nafasi. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
New Vocabulary
fall/fell |
anguka/alianguka |
Example
-
A: What’s wrong?
-
B: My knee hurts.
-
A: What happened to your knee?
-
B: I fell and I hit my knee.