Kujifunza Kiingereza
Somo la 24: Afya


“Somo la 24: Afya,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 24,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi

marafiki wakitabasamu nje

Lesson 24

Health

Shabaha: Nitajfunza kuelezea jinsi gani mtu anahisi wakati anapougua.

Personal Study

Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Press Forward

Songa Mbele

With God’s help, I can press forward even when I face obstacles.

Kwa msaada wa Mungu, ninaweza kusonga mbele hata wakati ninapokabiliana na vikwazo.

Nabii Lehi katika Kitabu cha Mormoni aliota ndoto ambayo inatufundisha jinsi ya kusonga mbele. Aliona watu wengi wakitembea katika njia kwenda kwenye mti mzuri ulio na tunda tamu. Tunda hili lilikuwa ni upendo wa Mungu. Safari yao katika njia hii ilikuwa ngumu kwa sababu “ukungu wa giza” ulificha njia hii (1 Nefi 8:23). Kwa bahati nzuri, kulikuwa na “fimbo ya chuma” wangeweza kushikilia ili kubaki katika njia ile (1 Nefi 8:24). Fimbo ya chuma ni neno la Mungu, ikijumuisha maandiko. Hapa kuna kile Lehi alichosema kuhusu safari yao.

“Wakasonga mbele, daima wameshikilia ile fimbo ya chuma, hadi wakafika … na kula matunda ya ule mti” (1 Nefi 8:30).

Watu walifika kwenye ule mti kwa sababu waliendelea kushikilia fimbo ya chuma na kuendelea kutembea kwenda mbele, wakimtumainia Mungu. Hawakuvutwa mawazo au kukata tamaa wakati giza lilipokuja. Wewe unafanya bidii ya kujifunza Kiingereza. Wakati mwingine unachoka na hauhisi kujifunza. Wakati mwingine kuna mambo mengine yanahitaji usikivu wako na muda wako. Umepata njia za kujifunza hata hivyo. Usiache sasa. Unaweza kuendelea kupata elimu unaposonga mbele ukiwa na tumaini katika Mungu.

watu wameshikilia fimbo ya chuma

Ponder

  • Ni nini kilicho “ukungu wa giza” kwako katika kujifunza Kiingereza?

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kusonga mbele hata wakati ambapo kujifunza ni vigumu?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutengeneza kadi za kunyanyua ili kukusaidia kukariri maneno mapya. Unaweza kutumia karatasi au app.

How do you feel?

Je, unahisije?

Nouns

backache

maumivu ya mgongo

cold

mafua

diarrhea

kuhara

earache

maumivu ya sikio

headache

maumivu ya kichwa

sore throat

maumivu ya koo

stomachache

maumivu ya tumbo

toothache

maumivu ya jino

Adjectives

congested

songamana

dizzy

kizunguzungu

nauseated

kichefuchefu

sick

mgonjwa

tired

choka

weak

dhaifu

Verbs

breathe

pumua

eat nuts

kula njugu

run

kimbia

stand up

simama

work

kazi

Ona somo la 10 kwa ajili ya verbszaidi.

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: How do you feel?A: I have a (noun).

Questions

swali la mpangilio wa 1 unahisi vipi

Answers

jibu la mpangilio wa 1 nina nomino

Examples

mwanaume mwenye vidonda vya koo

Q: How do you feel?A: I have a sore throat.

Q: How does he feel?A: He has diarrhea.

mwanaume ameshika tumbo linalouma

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kutambua mipangilio hii wakati wa mazoezi yako ya kila siku.

Q: Do you feel (adjective)?A: I feel (adjective) when I (verb).

Questions

swali la mpangilio wa 2 unahisi kivumishi

Answers

jibu la mpangilio wa 2 ninahisi kivumishi wakati nina kitenzi

Examples

msichana ameshika tumbo linalouma

Q: Do you feel dizzy?A: I feel dizzy when I stand up.

Q: Does she feel nauseated?A: She feels nauseated when she eats nuts.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources na katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 1.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi” chako. Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Press Forward

(20–30 minutes)

watu wakishikilia fimbo ya chuma

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Chagua mpango. Usimwambie mwenzako ni mtu gani umemchagua. Uliza na ujibu maswali ili kukisia mtu huyu. Chukueni zamu.

New Vocabulary

cough

kikohozi

fever

homa

runny nose

mafua

sneeze

chafya

throw up

tapika

Example

Mwenza B anamchagua Virgil.

  • B: Does he or she feel dizzy?

  • A: Yes, he feels dizzy.

  • B: Does he have a cough?

  • A: No, he doesn’t have a cough.

  • B: Is it Virgil?

  • A: Yes.

Sun Wen

  • She feels dizzy.

  • She is tired.

  • She feels nauseated.

  • She has a fever.

  • She throws up a lot.

Virgil

  • He feels weak.

  • He is tired.

  • He feels dizzy.

  • He has a fever.

  • He has diarrhea.

Aamir

  • He feels congested.

  • He has a fever.

  • He sneezes a lot.

  • He has a cough.

  • He has a sore throat.

Frida

  • She feels congested.

  • She has a sore throat.

  • She sneezes a lot.

  • She has a cold.

  • She has a cough.

Franz

  • He feels weak.

  • He is tired.

  • He feels nauseated.

  • He has a fever.

  • He has diarrhea.

Louis

  • He can’t breathe well.

  • He has a fever.

  • He sneezes a lot.

  • He has a cough.

  • He has a runny nose.

Sarai

  • She can’t breathe well.

  • She has a sore throat.

  • She sneezes a lot.

  • She has a cold.

  • She has a runny nose.

Anja

  • She is weak.

  • She is tired.

  • She is nauseated.

  • She has a fever.

  • She throws up a lot.

ikoni ya 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Fanya Igizo la kila hali ya hapo chini. Mwenza A anauliza maswali. Mwenza B anajibu maswali. Tumia mipangilio na msamiati kutoka kwenye somo hili na somo la 23. Sema mengi kadri uwezavyo. Badilisha nafasi.

Example

Mwenza A ni nesi. Mwenza B ni mgonjwa ambaye anaharisha.

msichana akiwa na daktari
  • A: How do you feel?

  • B: My stomach hurts.

  • A: Do you have a fever?

  • B: No, I don’t.

  • A: Do you have diarrhea?

  • B: Yes, I have diarrhea.

  • A: Do you feel nauseated?

  • B: I feel nauseated when I eat.

Situation 1

mwanamke mgonjwa kitandani akizungumza na simu

Mwenza A ni rafiki. Mwenza B anampigia simu rafiki yake kwa sababu rafiki huyu ana mafua.

Situation 2

daktari akiongea na mgonjwa wa kike

Mwenza A ni daktari. Mwenza B anaenda kwa daktari kwa sababu yeye ni mgonjwa na dhaifu.

Situation 3

mwanamke akimtembelea mwanamke mgonjwa aliye kitandani

Mwenza A ni mwanafamilia. Mwenza B ni mgonjwa na anazungumza na mwanafamilia.

Situation 4

mwanawake akifanya kazi katika kituo cha huduma

Mwenza A ni nesi ambaye anajibu simu. Mwenza B anapiga simu kwa sababu yeye ana maumivu ya mgongo na hawezi kupumua vizuri.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya shabaha na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Describe how I feel when sick.

    Elezea jinsi ninavyohisi ninapokuwa mgonjwa.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Describe how others feel when sick.

    Elezea jinsi wengine wanavyohisi wanapokuwa wagonjwa.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Soma kanuni ya kujifunza.

  2. Kariri msamiati.

  3. Fanya mazoezi ya mpangilio.

  4. Fanya mazoezi kila siku.

Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Akina kaka na akina dada, katika Kanisa hili, tunaamini katika uwezekano wa kiungu wa watoto wote wa Mungu na katika uwezo wetu wa kuwa kitu zaidi katika Kristo. Kwa wakati wa Bwana, siyo mahali gani tunapoanzia, bali ni wapi tunaelekea ndiyo muhimu zaidi” (Clark G. Gilbert, “Kuwa Zaidi katika Kristo: Mfano wa Mteremko,” Liahona, Nov. 2021, 19).