“Somo la 25: Kupitia Tena,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 25,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 25
Review
Shabaha: Nitapitia tena EnglishConnect 1 na kutafakari juu ya uzoefu wangu.
Personal Study
Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Learn by Study and by Faith
Jifunze Kwa Kusoma na Kwa Imani
I can rely on God to seek learning by study and by faith.
Ninaweza kumtegemea Mungu ili kutafuta kujifunza kwa kusoma na kwa imani.
Bwana ametupatia mpangilio wa kujifunza:
“Tafuteni kwa bidii na kufundishana maneno ya hekima; ndiyo, tafuteni kutoka kwenye vitabu vizuri maneno ya hekima, tafuteni maarifa hata kwa kujifunza na pia kwa imani” (Mafundisho na Maagano 88:118)
Tafakari juu ya uzoefu wako katika EnglishConnect. Je, umetumiaje mpangilio huu? Tafakari juu ya kanuni za kujifunza na kauli tulizojifunza pamoja.
-
“Wewe ni mtoto wa Mungu”—Mimi ni mtoto wa Mungu aliye na uwezekano na kusudi la milele.
-
“Kutumia imani katika Yesu Kristo”—Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya mambo yote ninapoweka imani katika Yeye.
-
“Wajibika”—Nina uwezo wa kuchagua, na ninawajibika kwa ajili ya kujifunza kwangu mwenyewe.
-
“Pendaneni na fundishaneni”—Ninaweza kujifunza kutoka kwa Roho ninapowapenda, kuwafundisha na kujifunza pamoja na wengine.
-
“Songa mbele”—Kwa msaada wa Mungu, ninaweza kusonga mbele hata wakati ninapokabiliana na vikwazo.
-
“Shauriana na Bwana”—Ninaweza kuboresha kujifunza kwangu kwa kushauriana na Mungu kila siku kuhusu juhudi zangu.
Kikundi chako cha EnglishConnect kinaweza kuwa kinaisha, lakini kuna mambo mengi zaidi Mungu anayokutaka ujifunze na uyapitie. Baba yako wa Mbinguni anakupenda na anataka kukubariki ufikie uwezekano wako wa kiungu. Unaweza kumtegemea Mungu na kuendelea “kutafuta kujifunza kwa kusoma na kwa imani.”
Ponder
-
Ni kwa jinsi gani wewe umepata uzoefu wa upendo wa Mungu na msaada katika kujifunza Kiingereza?
-
Ni kwa jinsi gani umetumia kanuni za kujifunza katika EnglishConnect?
-
Ni kwa jinsi gani utatumia kanuni za kujifunza katika maeneo mengine ya maisha yako?
Prepare for Activity 1
Soma maelekezo ya shughuli ya 1. Tazama orodha ya mada. Andika swali moja unaloweza kuuliza kuhusu kila mada. Soma maswali yako kwa sauti.
Mada
Prepare for Activity 2
Soma maelekezo ya shughuli ya 2. Tazama orodha ya mada. Andika maswali manne unayoweza kuuliza kuhusu kila mada. Soma maswali yako kwa sauti.
Mada
Prepare for Activity 3
Soma maelekezo ya shughuli ya 3. Fikiria kuhusu jiji lako. Andika maswali matatu na majibu yake kuhusu jiji hilo. Yasome kwa sauti. Ona somo la 21 na somo la 22 kwa ajili ya msamiati na mipangilio.
Conversation Group
Activity 1: Create Your Own Conversations
(10–15 minutes)
Uliza na ujibu maswali kuhusu jina lako, jinsi unavofanya leo, mahali unakotokea, familia yako na nyumba yako. Chukueni zamu.
Example
-
A: Hi. My name is Ana. What’s your name?
-
B: Hi, Ana. My name is Niko. How are you?
-
A: I am great. Thanks. How about you?
-
B: I am well. Thanks for asking.
-
A: Where are you from?
-
B: I’m from Brazil. And you?
-
A: Nice. I’m from Guatemala. How many people are in your family?
-
B: There are seven people in my family.
-
A: That’s a big family. Do you live in a house or in an apartment?
-
B: I live in an apartment.
Activity 2: Create Your Own Conversations
(10–15 minutes)
Uliza na ujibu maswali kuhusu kile unachopenda kufanya na utaratibu wako wa kila siku, na ni vyakula gani wewe unakula. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
New Vocabulary
banana |
ndizi |
blender |
blenda |
orange |
chungwa |
peach |
pichi |
smoothie |
smuthi |
strawberry |
stroberi |
Example
-
A: What do you like to do?
-
B: I like to read. Do you like to read?
-
A: Yes, I like to read too. Do you read every day?
-
B: Yes, I read every day. Before I go to bed, I read. What food do you like?
-
A: I like fruit because it’s delicious.
-
B: Me too! I eat a smoothie for breakfast every morning.
-
A: Wow! How do you make it?
-
B: First, put an orange, a banana, strawberries, and peaches in a blender. Then, mix all the fruit together.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(10–15 minutes)
Fanya Igizo la kila hali. Mwenza A anauliza maswali. Mwenza B anajibu maswali. Badilisha nafasi.
Partner A
Wewe unatembelea jiji la Mwenza B.
Muulize mwenza wako:
-
Akuelezee kuhusu jiji lao.
-
Maelekezo ya kutoka pale ulipo hadi maeneo mengine katika jiji.
Partner B
Wewe unaishi katika jiji hili.
Mwambie mwenza wako:
-
Kuhusu jiji lako.
-
Jinsi ya kufika sehemu zingine za jiji.
Example
-
A: This is my first time in this city. Tell me about the city.
-
B: It is big and busy.
-
A: Where is the train station?
-
B: It’s on D Street.
-
A: How do I get there from the grocery store?
-
B: Turn right on Main Street. Go straight. Turn left on D Street. The train station is across from the bank.
Hatua Yako Inayofuata
Sasa kwamba umekamilisha EnglishConnect 1, fikiria kuendelea na English Connect 2. Ili kujifunza zaidi, tembelea join.englishconnect.org.
Je, hauko tayari kuanza EnglishConnect 2? Endelea kujifunza Kiingereza katika EnglishConnect 1.
Chochote utakachofanya baada ya hapa, kumbuka kwamba wewe ni mtoto wa Mungu na Yeye anaweza kukusaidia kuendelea.