“Kiambatisho: Michezo ya Kikundi cha Mazungumzo,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Michezo ya Kikundi cha Mazungumzo,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Appendix
Conversation Group Games
Michezo ya Kikundi cha Mazungumzo
Kilichojumuishwa katika kitabu cha kiada hiki ni michezo ya burudani ili kufanyia mazoezi Kiingereza. Unaweza kucheza michezo hii wakati wa mkutano wowote wa kikundi. Tumia mpangilio na msamiati kutoka katika somo ambalo upo au somo la awali. Mingi ya michezo hii inakuhitaji wewe kufanya kazi na mwenza au kikundi kidogo.
Questions (10–15 minutes)
Maswali (dakika 10–15)
Steps
Hatua
-
Chagua swali kutoka kwenye orodha. Kumbuka unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno mengine na virai.
-
Shiriki jibu lako na kikundi.
-
Chukueni zamu. kuchagua maswali na kushiriki majibu. Unaweza kuzungumza kuhusu maswali mengi kama upendavyo.
Questions to Review Patterns:
Maswali ya Kurejelea Mipangilio:
-
What do you like to do?
-
Why do you like to study English?
-
Can you tell me about your family?
-
What are you wearing?
-
What do you do before you come to the conversation group?
-
What do you do in the morning?
-
When do you work?
-
What’s the weather in New York?
-
Where do you work?
-
What do you do for work?
-
Do you like to teach people?
-
What do you eat for dinner?
-
What foods do you like?
-
What do you want for lunch?
-
What is your favorite food? How do you make it?
-
How much do groceries cost?
-
Where do you live?
-
Tell me about your house.
-
Where is your favorite place to eat?
More Questions:
Maswali Zaidi:
-
Tell me about your friends.
-
Tell me about your job.
-
Tell me about your city.
-
Tell me about your favorite place.
-
Tell me about your daily routine. What do you do every day?
-
What do you like to wear?
-
What do you do when you are sick?
-
What do you do when you are hurt?
-
What is expensive in your city?
-
What is cheap in your city?
Notes
Mihutasari
-
Unaweza kucheza mchezo huu pamoja na kikundi chote au vikundi vidogo vya watu watatu hadi watano.
-
Hakuna ukomo wa maswali kwenye orodha hii. Unaweza kubuni maswali mapya. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mistari ili kubuni maswali zaidi.
-
Kama unataka kufanya mchezo huu kuwa wenye changamoto zaidi, chukueni zamu kushiriki majibu unayokumbuka kutoka kwa kila mshiriki wa kikundi.
-
Unaweza kutumia maswali haya pamoja na michezo mingine kama vile “mnyororo ya Baiskeli” au “Kutupiana Mpira.”
Hot Seat (10–20 minutes)
Kiti cha Moto (dakika 10–20)
Steps
Hatua
-
Gawanyika katika timu mbili.
-
Chagua wanafunzi wawili (mwanafunzi mmoja kutoka kwenye kila timu). Wanafunzi hawa waketi kwa kukitazama kikundi (katika “kiti cha moto”) migongo yao ikitazama ubaoni.
-
Mwalimu wenu anaandika neno la msamiati au kirai ubaoni. Wanafunzi walio katika “kiti cha moto” hawawezi kuona lile neno.
-
Timu zinachukua dakika mbili kuwasaidia wenzao wa timu moja walio katika “kiti cha moto” kubahatisha lile neno lililo ubaoni bila kulisema lile neno.
-
Mtu aliye katika “kiti cha moto” ambaye anasema lile neno kwanza anapata alama moja kwa ajili ya timu yake. Kama timu inasema lile neno lililo ubaoni huku wakijaribu kumsaidia mwanatimu wao kubahatisha, hawapati alama.
-
Rudia na maneno mapya.
Notes
Mihutasari
-
Unda timu moja hadi tatu kutegemeana na ukubwa wa kikundi.
-
Kama mnafanya mkutano mtandaoni, chezeni mchezo wa kikundi chote badala ya timu. Mtu mmoja anakuwa katika “kiti cha moto.” Mtu huyu hajui lile neno. Mtu mmoja anakuwa “mtoa kidokezo.” Yule “mtoa kidokezo” anachagua neno na kutoa vidokezo ili yule katika “kiti cha moto” aweze kubahatisha lile neno.
Ball Toss (10–15 minutes)
Kutupiana Mpira (dakika 10–15)
Steps
Hatua
-
Tafuta mpira, kitu laini, au kipande cha karatasi kilichoviringishwa.
-
Chagua swali. (Tumia swali mojawapo kutoka katika somo au ona “Maswali” katika kiambatisho hiki.)
-
Uliza swali na umtupie mwanafunzi mpira.
-
Mwanafunzi anadaka mpira na anajibu lile swali.
-
Yule mwanafunzi anauliza swali tena na anamtupia mwanafunzi mwingiine mpira.
-
Rudia mpaka kila mwanafunzi katika kundi lako amejibu swali. Kisha anza tena na swali jipya.
Notes
Muhtasari
-
Ili kufanya mchezo huu kuwa wenye changamoto zaidi, badilisha swali kila mara unapotupa mpira.
-
Kama mnafanya mkutano mtandaoni, ita majina ya wahusika badala ya kutupa mpira.
Dice Game (10–15 minutes)
Mchezo wa Dadu (dakika 10–15)
Steps
Hatua
-
Unahitaji dadu moja (au kadi ya namba iliyo na namba 1 hadi 6).
-
Chagua vitenzi sita na uviandike kwenye ubao namba 1 hadi 6.
-
Fanya kazi na mwenza au kikundi kidogo. Furusha dadu. Buni sentensi ambayo inatumia kitenzi kwa namba iliyotokea. Chukueni zamu.
Example
Mfano
Mwalimu anaandika ubaoni:
-
cook
-
stir
-
bake
-
boil
-
cut
-
add
Mwanafunzi wa 1 anafurusha dadu na anapata namba 6. Anaunda sentesni akitumia add.
-
“I add sugar to my oatmeal.”
Mwanafunzi wa 2 anafurusha dadu na anapata namba 4. Anaunda sentensi akitumia boil
-
“I boil eggs for lunch.”
Mwanafunzi wa 3 anafurusha dadu na anapata namba 3. Anaunda sentesni akitumia bake.
-
“I like to bake cookies.”
Notes
Mihutasari
-
Maneno mengine yanaweza kutumiwa badala ya vitenzi.
-
Kama mnafanya mkutano mtandaoni, chezeni mchezo na kikundi chote. Tumia dadu na mchukue zamu kuunda sentensi.
Give One, Get One (10–20 minutes)
Toa Moja, Pata Moja (dakika 10–20)
Steps
Hatua
-
Chagua mada kwa ajili ya kikundi (kwa mfano: familia, michezo au chakula).
-
Andika chini maneno mengi kadiri unayojua kuhusu mada kwa dakika moja au mbili.
-
Simama na utembee kuzunguka chumba. Tafuta mwenza.
-
Shiriki neno lako kutoka kwenye orodha yako na mwenzako. Mwenza wako anashiriki neno na wewe. Kama ni neno jipya, ongeza neno lile kwenye orodha yako.
-
Tembea kuzunguka chumba tena. Tafuta mwenza mpya. Rudia.
Example
Mfano
Mada: familia
Mwenza A anaandika:
-
mom
-
dad
-
sister
-
brother
Mwenza B anaandika:
-
grandfather
-
grandmother
-
mother
-
father
-
aunt
-
uncle
-
A: What’s one word from your list?
-
B: Grandmother.
-
A: I don’t have that word. I’ll add it to my list.
-
B: What’s a word from your list?
-
A: Mom.
-
B: I have mother. I will write mom next to mother.
Wanafunzi wote wawili wanaongeza maneno mapya kwenye orodha zao.
Orodha ya Mwenza A:
-
mom
-
dad
-
sister
-
brother
-
grandmother
Orodha ya Mwenza B:
-
grandfather
-
grandmother
-
mother, mom
-
father
-
aunt
-
uncle
Notes
Mihutasari
-
Hii ni njia nzuri ya kujifunza au kufanya mazoezi ya msamiati mpya ambao hauko katika somo.
-
Kama mnafanya mkutano mtandaoni, acha kila mtu ashiriki na kikundi chote neno moja kutoka kwenye orodha zao badala ya kucheza katika jozi.
Speculation (15–20 minutes)
Kuotea (dakika 15–20)
Steps
Hatua
-
Fikiria kitenzi.
-
Sema kitenzi kwa sauti.
-
Ukitumia kitenzi hiki, unda sentensi ya kweli kuhusu mwanafunzi mwingine. Sema, “I think that you …” ili kuanza sentensi yako.
-
Mwanafunzi mwingine anasema kama kauli yako ni kweli au la.
-
Kama ni kweli, unapata alama moja. Kama si kweli, haupati alama.
-
Mwanafunzi wa kwanza ambaye anafikisha alama 5 anashinda!
-
Kamilisha raundi 10 hadi 20. Badilisha kitenzi kila mzunguko.
Example
Mfano
Mwanafunzi A (kwa mwanafunzi B): The verb is like. I think that you like chocolate.
Mwanafunzi B: That’s true! (Mwanafunzi A anapata alama.)
Mwanafunzi B (kwa mwanafunzi C): I think that you like to play basketball.
Mwanafunzi C: That’s not true! (Mwanafunzi B hapati alama.)
Notes
Mihutasari
-
Unda vikundi vya watu watatu hadi watano.
-
Mchezo huu unajumuisha raundi 10 hadi 20. Utahitajika kuwa na kitenzi kwa kila raundi. Chukueni zamu kusema kitenzi kipya kila wakati raundi inapoanza.
Two Truths and One Lie (10–15 minutes)
Kweli Mbili au Uongo Mmoja (dakika 10–15)
Steps
Hatua
-
Fikiria mambo mawili ambayo ni ya kweli kukuhusu wewe. Buni kimoja ambacho si kweli. Jaribu kutumia msamiati mpya na kirai kutoka kwenye somo.
-
Soma kauli yako kwa sauti kwa kikundi chako.
-
Washiriki wa kikundi chako wanakuuliza maswali ili kubahatisha ni kauli ipi ambayo si kweli. Jibu maswali yao.
Example
Mfano
Mshiriki wa 1 wa Kikundi: “I like pizza. I like French fries. I like chocolate. Which is not true?”
Mshiriki mwingine wa kikundi anauliza maswali:
-
Q: What is your favorite kind of pizza?A: I like cheese pizza.Q: What is your favorite candy bar?A: I like chocolate and caramel.Q: Where do you like to get French fries?A: I don’t have a favorite place.
Mshiriki mwingine wa kikundi anabahatisha: “I think you don’t like French fries.”
Mshiriki wa 1 wa Kikundi: “That’s right! I don’t like French fries.”
Vocabulary Cards (10–15 minutes)
Kadi za Msamiati (dakika 10–15)
Steps
Hatua
-
Andika maneno 5 hadi 10 ya msamiati kwenye vipande vidogo vya karatasi (vipande vyenye gudi ni bora). Weka vipande hivyo vya karatasi katika rundo.
-
Tafuta mwenza.
-
Gueza rundo la maneno juu chini ili wewe usione maneno yale. Badilishana marundo na mwenzako.
-
Chagua karatasi. Usiangalie lile neno. Shikilia karatasi ile kwenye paji lako la uso. Mwenza wako anaelezea neno lile (au anatoa tafsiri), ili kwamba wewe uweze kubahatisha lile neno lililo kwenye karatasi. Kama ukibahatisha vizuri, unapata alama moja.
-
Chukueni zamu. Rudia kwa kila karatasi kwenye rundo lako.
Notes
Muhtasari
-
Kama mnafanya mkutano mtandaoni, chezeni mchezo wa kikundi chote badala ya jozi. Kila mtu anaandika orodha ya maneno. Usionyeshe orodha yako kwa kikundi. Chukueni zamu kuchagua neno moja kutoka kwenye orodha yako. Lielezee kwa kikundi bila kusema neno lile. Washiriki wa kikundi wanabahatisha lile neno.
Bicycle Chain (in person) (10–20 minutes)
Mnyororo ya Baiskeli (ana kwa ana) (dakika 10–20)
Hii shughuli hufanya vyema tu kwa makundi yanayokutana ana kwa ana.
Steps
Hatua
-
Chagua swali. (Tumia mojawapo ya swali kutoka kwenye somo au ona “Maswali” katika kiambatisho hiki.)
-
Jipangeni katika mistari miwili ambayo mtatazamana uso kwa uso.
-
Watu wanaotazamana wao ni wenza.
-
Wenza wanauliza na kujibu swali.
-
Wanatembea katika duara ili kila mtu awe na mwenza mpya.
-
Wenza wanauliza na kujibu swali.
-
Rudia hatua za 5 na 6.
Notes
Mihutasari
-
Kama una watu wa namba witiri, unda kikundi kimoja cha watu watatu.
Mingle and Share (in person) (10–15 minutes)
Changamana na Shiriki (ana kwa ana) (dakika 10–15)
Hii shughuli hufanya vyema tu kwa makundi yanayokutana ana kwa ana.
Steps
Hatua
-
Chagua swali. (Tumia mojawapo kutoka kwenye somo au ona “Maswali” katika kiambatisho hiki.)
-
Simama na utafute mwenza.
-
Muulize mwenza wako swali. Kumbuka jibu la mwenza wako. Jibu swali la mwenza wako.
-
Tembea chumbani na utafute mwenza mpya. Uliza maswali na ujibu maswali. Rudia mara kadhaa na wenza wapya. Kumbuka majibu ya wenza wako wote.
-
Rudi kwenye kiti chako. Shiriki pamoja na kundi lako kile ulichojifunza.
Example
Mfano
Question: How many people are in your family?
Wanafunzi wanatembea wakiuliza na kujibu swali wakiwa na wenza tofauti.
-
Maria: How many people are in your family?
Luna: There are four people in my family. How many people are in your family?
Maria: Three.
Wanafunzi wanashiriki kile walichojifunza.
-
Teacher: How many people are in Maria’s family?
Luna: There are three people in Maria’s family.