Vitabu vya Maelekezo na Miito
0. Maelezo ya Jumla ya Utangulizi


“0. Maelezo ya Jumla ya Utangulizi,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho (2020)

“0. Maelezo ya Jumla ya Utangulizi,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

0.

Maelezo ya Jumla ya Utangulizi

0.0

Utangulizi

Bwana alifundisha, “acha kila mtu na ajifunze wajibu wake, na kutenda kazi katika ofisi ambayo ameteuliwa, kwa bidii yote” (Mafundisho na Maagano 107:99). Kama kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, unapaswa kutafuta ufunuo binafsi ili ukusaidie kujifunza na kutimiza majukumu ya wito wako.

Kujifunza maandiko na mafundisho ya manabii wa siku za mwisho kutakusaidia uelewe na utimize majukumu yako. Unapojifunza maneno ya Mungu, utakuwa mpokeaji mzuri zaidi wa ushawishi wa Roho (ona Mafundisho na Maagano 84:85).

Pia unajifunza majukumu yako kwa kusoma maelekezo katika kitabu hiki cha maelezo. Maelekezo haya yanaweza kualika ufunuo kama yatatumika kutoa uelewa wa kanuni, sera, na taratibu za kutumia wakati unapotafuta mwongozo wa Roho.

0.1

Kitabu Hiki cha Maelezo Jumla

Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kinatoa mwongozo kwa ajili ya viongozi wakuu na viongozi wa Kanisa wa maeneo husika. Kimegawanyika katika sehemu nne:

  • Mafundisho ya Msingi: Sura hizi zinatoa mafundisho na kanuni za msingi za kuhudumu katika Kanisa. Zinaelezea:

    • Mpango wa furaha wa Mungu, kazi ya wokovu na kuinuliwa, na lengo la Kanisa.

    • Nafasi ya familia katika Mpango wa Mungu, kazi ya wokovu na kuinuliwa nyumbani, na uhusiano kati ya Kanisa na nyumbani.

    • Kanuni za Ukuhani.

    • Kanuni kwa ajili ya kuongoza katika Kanisa la Mwokozi.

  • Muundo wa Kanisa: Sura hizi zinatoa maelekezo kwa ajili ya urais wa kigingi, na uaskofu, viongozi wa akidi za ukuhani, viongozi wa vikundi katika kigingi na kata, na wengine wanaohudumu katika Kanisa.

  • Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa: Sura hizi zinaelekeza juu ya kazi kuu ya Kanisa:

    • Kuishi Injili ya Yesu Kristo

    • Kuwatunza wale wenye mahitaji

    • Kuwaalika watu wote waipokee injili

    • Kuziunganisha familia milele

  • Utawala wa Kanisa: Sura hizi zinatoa miongozo ya ziada kwa ajili ya kusimamia Kanisa. Mada zinajumuisha mikutano, miito, kumbukumbu, usimamizi wa fedha, na sera.

Vichwa vya habari na vichwa vidogo vya habari katika kitabu hiki cha maelezo vimepewa namba ili kufanya mada ziwe rahisi kupatikana na kurejelea. Kwa mfano, maelekezo kuhusu ndoa ya hekaluni yametolewa katika 27.3.1. Nambari 27 inahusu sura, nambari 3 inahusu sehemu katika sura ile, na nambari 1 inahusu sehemu ndogo.

0.2

Mabadiliko na Nyenzo za Hiari

Si vigingi na kata zote zina mahitaji yaliyo sawa. Kitabu hiki kina miongozo kwa ajili ya mabadiliko pamoja na nyenzo za hiari:

  • Miongozo kwa ajili ya mabadiliko ( ) inatoa maelekezo juu ya jinsi ya kubadili mipangilio ya Kanisa na programu kwa kata au matawi yenye mahitaji na nyenzo zinazotofautiana.

  • Nyenzo za hiari ( ) zina taarifa na maelekezo ya ziada ambayo yanaweza kuwa ya msaada kwa viongozi wa kigingi na kata.

Viongozi wanatafuta mwongozo wa kiungu kuhusu miongozo na nyenzo zipi za hiari zitumike ili kukidhi mahitaji ya waumini.

0.3

Taarifa mpya

Kitabu hiki cha maelezo kitasasishwa kila baada ya kipindi fulani. Orodha ya mabadiliko ya hivi karibuni inapatikana katika “Muhtasari wa Taarifa Mpya.”

0.4

Maswali kuhusu Maelekezo

Wakati maswali yanapotokea ambayo hayana majibu katika maandiko, maneno ya manabii walio hai, au kitabu hiki cha maelezo, waumini wa Kanisa wanapaswa kutegemea katika maagano yao na Mungu, ushauri wa viongozi wa maeneo yao, na mwongozo wa kiungu wa Roho kwa ajili ya kuwaongoza.

Kama viongozi wana maswali kuhusu taarifa katika kitabu hiki cha maelezo au kuhusu maswala ambayo majibu yake hayamo humu, washauriane na mamlaka kiongozi ya eneo lao.

0.5

Istilahi

Isipokuwa pale ilipoelekezwa vinginevyo:

  • Maneno askofu na uaskofu katika kitabu hiki cha maelezo yanahusu pia marais wa matawi na urais wa matawi. Maneno rais wa kigingi na urais wa kigingi yanahusu pia marais wa wilaya na urais wa wilaya. Kwa ajili ya muhtasari wa jinsi mamlaka ya marais wa wilaya yanavyotofautiana na yale ya marais wa vigingi, ona 6.3.

  • Marejeleo ya neno kata na vigingi pia yanatumika kwa matawi, wilaya, na misheni.

  • Marejeleo kuhusu siku ya Jumapili yanatumika kwa siku yoyote ambayo sabato inaadhimishwa katika eneo husika.

  • Neno kitengo linahusu kata na matawi.

  • Marejeleo kuhusu wazazi kwa ujumla pia yanatumika kwa walezi kisheria.

Miito ya askofu na rais wa tawi hailingani katika mamlaka na wajibu, kadhalika miito ya rais wa kigingi na rais wa wilaya. Askofu ni ofisi katika ukuhani, na kutawazwa kwake kunaidhinishwa na Urais wa Kwanza tu. Marais wa vigingi huitwa na Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka na Sabini wa Maeneo.

0.6

Kuwasiliana na Makao Makuu ya Kanisa au Ofisi ya Eneo

Baadhi ya sura katika kitabu hiki cha maelezo zinajumuisha maelekezo ya kuwasiliana na makao makuu ya Kanisa au ofisi ya eneo. Maelekezo ya kuwasiliana na makao makuu ya Kanisa yanahusu wale waliopo Marekani na Kanada. Maelekezo ya kuwasiliana na ofisi za eneo yanahusu wale waliopo nje ya Marekani na Kanada.

Chapisha