Ponografia
Ninazungumzaje na mtoto wangu kuhusu afya ya jinsia?


“Ninazungumzaje na mtoto wangu kuhusu afya ya jinsia?” Msaada kwa ajili ya Wazazi (2021)

“Ninazungumzaje na mtoto wangu kuhusu afya ya jinsia?” Msaada kwa ajili ya Wazazi

Picha
familia ikitembea nje

Ninazungumzaje na mtoto wangu kuhusu afya ya jinsia?

Wazazi wengi wanahisi kusita au kuona aibu kuzungumza na watoto wao kuhusu jinsia, au wanaogopa kwamba kuzungumza na watoto wao kuhusu jinsia kutazua tabia mbaya za kijinsia. Ukweli ni huu, kama hautazungumza na watoto wako kuhusu jinsia, watajifunza kuhusu hilo kutoka chanzo kingine. Kwa kuwa na mazungumzo kila mara na watoto wako kuhusu mada muhimu kama vile afya ya jinsia, utawasaidia wao kuelewa kwamba wewe ni mtu salama wa kumwendea.

Watoto wengi kwa kawaida wana udadisi, na wanataka kuelewa hisia, alizotoa Mungu za kiasili wanazopata. Unaweza kujiandaa mwenyewe kuzungumza na watoto wako kuhusu jinsia kwa kukumbuka vile ulivyokuwa kama wao kipindi cha umri wako. Ni baadhi ya hisia zipi ulizozipata? Ni mawazo gani, maswali, au dukuduku ulikuwa nayo? Ni wapi ulitafuta taarifa? Ni kipi unatamani ungekisikia au kufundishwa?

Ni KAWAIDA kama unahisi kutokuwa na uhakika kuhusu jinsi bora ya kufanya mazungumzo haya. Unaweza kutumia kutokuwa salama kwako kujenga mahusiano yako na watoto wako. Watoto wanaweza kuhisi upendo wako unapokuwa mwaminifu na mnyoofu katika mawasiliano na wao, licha ya kutojisikia sawa ambako ungeweza kukuhisi.

Ili kuendeleza mawasiliano wazi, unaweza:

  • Kuanza wakati watoto wako wangali wadogo kwa kuita sehemu za mwili kwa majina yake sahihi. Hili huwafunza watoto kuhusu miili yao na huwapa wao lugha wanayohitaji ili kuwa na afya na wenye uelewa.

  • Acha watoto wako wajue kuwa wanaweza kukuuliza maswali yoyote, kisha usijaribu kuonyesha kukasirishwa au kuonea aibu maswali yao au kukiri kwao. Furahia kwamba wanazumgumza nawe, waonyeshe upendo na waunge mkono, na fanya vyema uwezavyo kuendelea kuwasiliana.

  • Epukana na kutumia sitiari za kijinsia. Watoto wanahitaji taarifa kuwasilishwa kwa njia wazi na ya uaminifu. Kwa mfano, baadhi ya vijana wanazungumza juu ya masomo ambapo kuvunja sheria ya usafi wa kimwili kunafananishwa na jojo iliyotafunwa au chakula ambacho kinapitishwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwenye chumba na hivyo kuwa kisichotamanika. Japokuwa inasemwa vizuri, aina hii ya sitiari mara nyingi hukuza hofu ya ujinsia au hisia za kutojithamini ambazo ni ngumu kurekebishika.

  • Kuwa na mada zinazohusiana na jinsia na acha watoto wako wafundishe pale wanapokuwa wanahisi wako tayari. Mada zingeweza kujumuisha kubalehe, picha za mwili, na vipengele chanya vya jinsia.

  • Jadili kuhusu kupata hisia za kimapenzi na msisimko kuwa ni jambo la kawaida. Watoto hawahitajiki kutenda juu ya hisia hizo na misisimko lakini wanaweza kujihadhari nazo. Hii inamaanisha kutambua hisia za kimapenzi lakini si kuchukulia katika mtazamo hasi. Utafiti umeonyesha kwamba kujizoeza kuchukua tahadhari kunaweza kuwasaidia watoto kufanya chaguzi bora ambazo zinaendana na viwango vyao na malengo yao.

  • Jaribu kutoudhika au kukasirika pale watoto wanapojihusisha na kujishika shika wenyewe au kijana anapokiri kupiga punyeto. Jinsi wazazi wanavyoitikia juu ya tabia hizi huathiri jinsi watoto na vijana wanahisi kuhusu wao wenyewe na jinsia zao.

  • Wafundishe watoto wako kwa nini za viwango zinazohusiana na mahusiano na jinsia. Unapofundisha viwango hivi na sababu za kwa nini ni vya thamani, kumbuka kwamba ni muhimu kufanya hivyo bila kuwa na aibu au hofu.1

Muhtasari

  1. Nukuu zilizonukuliwa na kutoholewa kutoka kwa Laura M. Padilla-Walker na Meg O. Jankovich, “Jinsi, Lini, na Kwa nini: Kuzungumza na Watoto Wako kuhusu Jinsia,” Liahona, Agosti. 2020.

Chapisha