“Kusaidia Waumini Wapya Kubakia kwenye Njia ya Agano,” Kusaidia Waumini Wapya Kubakia kwenye Njia ya Agano (2020)
“Kusaidia Waumini Wapya Kubakia kwenye Njia ya Agano,” Kusaidia Waumini Wapya Kubakia kwenye Njia ya Agano
Kusaidia Waumini Wapya Kubakia kwenye Njia ya Agano
Kabla ya Ubatizo
-
Je, wameanzisha urafiki na waumini?
-
Je, wanashiriki mahitaji yao na waumini? Je, wamejiunga na darasa la kujitegemea kama inahitajika?
-
Je, wanajifunza na kusali kuhusu injili ya Yesu Kristo?
-
Je, wamejifunza kuhusu mahekalu na familia za milele na kuanza kazi ya historia ya familia?
-
Je, wamepanga tarehe ya kufanya ubatizo kwa ajili ya mababu zao wafu?
-
Je, wanakidhi viwango vya ubatizo?
-
Je, wanahudhuria mikutano ya sakramenti kwa uthabiti?
Punde baada ya Ubatizo
-
Je, wanahisi kukubalika na kata?
-
Je, akina kaka au kina dada wahudumiaji wameanza kuwatunza?
-
Je, wanahudhuria mkutano wa sakramenti kila mara?
-
Je, waumini wanaume wamepokea Ukuhani wa Haruni?
-
Je, wamepokea kibali cha hekalu kwa ajili ya ubatizo na uthibitisho kwa ajili ya wafu na kushiriki katika ubatizo kwa ajili ya babu zao waliofariki?
-
Je, wanaendelea kusali na kujfunza injili ya Yesu Kristo kwa kuungwa mkono na waumini na wamisionari?
-
Je, wamepokea wito Kanisani au kazi za uhudumiaji?
-
Je, wameshiriki katika darasa la kujitegemea kama inahitajika?
Katika Mwaka wa Kwanza
-
Je, wamekuza urafiki wa kudumu na washiriki wa kata?
-
Je, wameimarisha imani yao katika Yesu Kristo kupitia sala na kujifunza injili kwa uthabiti?
-
Je, waumini wanaume wamepokea Ukuhani wa Melkidezeki?
-
Je, wanatoa huduma kwa wale walio na mahitaji? Je, wana wito wa Kanisa?
-
Je, wamepanga tarehe ya ibada zao wenywe za hekaluni? Je, wanaendelea kufanya kazi ya hekalu na kazi ya historia ya familia?