“Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2019,” Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2019 (2018)
“Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2019,” Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2019
Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2019
Zilizoorodheshwa hapa chini ni nyenzo za mtaala wa Jumapili za mwaka 2019, si zote kati ya hizo zinapatikana kwenye lugha zote. Vitu vipya kwa mwaka 2019 vimezingatiwa.
Mpangilio
Vitabu vya Kiada na Vifaa vya Nyenzo
Watu Binafsi na Familia
MPYA Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia (14717; Agano Jipya)
Ikiwa hii haipatikani katika lugha yako, tumia Agano Jipya Mwongozo wa Kujifunza kwa Mwanafunzi (35682).
Msingi
Muda wa kuimba (Umri kati ya miaka 3–11)
MPYA Njoo, Unifuate —Kwa Ajili ya Muda wa Kuimba: 2019
Nyenzo hii itapatikana kabla ya mwisho wa 2018 kwenye Njoo Unifuate.lds.org, primary.lds.org, na katika Gospel Library app.
Darasa la Chekechea (Umri wa Miezi 18–Miaka 2)
Tazama Watoto Wako: Kitabu cha Kiada cha Chekechea (37108)
Madarasa Yote ya Msingi (Umri wa miaka 3–11)
MPYA Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi (14718; Agano Jipya)
Ikiwa hii haipatikani katika lugha yako, tumia Msingi 7: Agano Jipya (34604).
Shule ya Jumapili
Shule ya Jumapili kwa Watu Wazima na Vijana
MPYA Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili (14716; Agano Jipya)
Ikiwa hii haipatikani katika lugha yako, tumia Agano Jipya Mafundisho ya Injili Kitabu cha Mwongozo cha Mwalimu (35681).
Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama
Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama
Ikiwa Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama haipatikani katika lugha yako, mada za mkutano huu wa baraza zinaweza kuamuliwa na urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama. Nyenzo zinazoweza kutumika ni maandiko, Kitabu cha Mwongozo 2: Usimamizi wa Kanisa (08702), Majarida ya Kanisa, Mabinti Katika Ufalme Wangu: Historia na Kazi ya Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama (06500), Kitabu cha Mwongozo wa Familia (31180), na nyenzo zingine zilizoidhinishwa na Kanisa.
Jumapili ya Pili na ya Tatu
Washiriki hujifunza, hujadili, na kutumia jumbe za mkutano mkuu kutoka kwa Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, pamoja na viongozi wengine wa Kanisa. Wanatumia mapendekezo kutoka kwenye Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama. Nyenzo hii inapatikana katika toleo la hivi karibuni kabisa la mkutano mkuu la Ensign au Liahona, kwenye ComeFollowMe.lds.org, au katika nyenzo zilizotolewa na ofisi yako ya eneo.
Ikiwa Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama haipatikani katika lugha yako, tumia Wajibu na Baraka za Ukuhani, Sehemu A (31111) au Mwanamke Mtakatifu wa Siku za Mwisho, Sehemu A (31113).
Jumapili ya Nne
Waumini hujifunza mada ya mafundisho inayohusu kazi ya akidi ya wazee au Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama. Wanatumia mapendekezo kutoka kwenye Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama. Nyenzo hii inapatikana katika toleo la hivi karibuni kabisa la mkutano mkuu la Ensign au Liahona, kwenye ComeFollowMe.lds.org, au katika nyenzo zilizotolewa na ofisi yako ya eneo.
Ikiwa Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama haipatikani katika lugha yako, tumia makala ya “Kanuni za Kuhudumu” yaliyoko katika Ensign na Liahona.
Jumapili ya Tano
Uaskofu au urais wa matawi hupanga mkutano.
Ukuhani wa Haruni na Wasichana
Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Wasichana
Kama hizi hazipatikani katika lugha yako, Tumia Kitabu cha Kiada cha Ukuhani wa Haruni 1 (34820) na Kitabu cha Kiada cha Wasichana 1 (34823). Ikiwa hivi havipatikani katika lugha yako, tumia Wajibu na Baraka za Ukuhani, Sehemu A (31111) au Kazi na Baraka za Ukuhani, Sehemu B (31112) na Mwanamke Mtakatifu wa Siku za Mwisho, Sehemu A (31113) au Mwanamke Mtakatifu wa Siku za Mwisho, Sehemu B (31114).
Jumuiya Zote
Mkutano wa Baraza la Walimu
Kufundisha katika Njia ya Mwokozi
Kozi zingine (kama vitabu vya kiada vinapatikana)
Kozi kwa ajili ya kuimarisha ndoa na familia, matayarisho ya kwenda hekaluni, matayarisho ya umisionari, na historia ya familia hayatafanyika wakati wa saa ya pili ya Kanisa. Hata hivyo, kwa busara ya askofu na kutegemea mahitaji ya pale, kozi hizi zinaweza kufundishwa wakati mwingine kwa ajili ya watu binafsi, familia, au makundi.
Maandalizi ya kwenda Hekaluni
Kujaliwa Kutoka Juu: Matayarisho ya kwenda Hekaluni Kitabu cha Kiada cha Semina cha Mwalimu (36854) na Kujitayarisha Kuingia Katika Hekalu Takatifu (36793)
Mahusiano ya Ndoa na Familia
Mahusiano ya Ndoa na Familia Kitabu cha Kiada cha Mwalimu (35865) na Mahusiano ya Ndoa na Familia Mwongozo wa Mshiriki (36357)
Nyenzo kwa Wale Walio na Ulemavu
Kuagiza nyenzo katika mfumo wa sauti, breli, maandishi makubwa, au maelezo mafupi, bonyeza store.lds.org.
© 2018 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Idhini ya Kiingereza: 4/18. Tafsiri ya Instructions for Curriculum 20192019. Swahili. Idhini ya kutafsiri: 4/18. PD60006387 743. Imepigwa chapa Marekani.