Maelekezo kwa ajili ya Mtaala
Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2021


“Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2021,” Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2021 (2020)

“Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2021,” Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2021

Picha
familia ikisoma maandiko

Maelekezo kwa ajili ya Mtaala wa Mwaka 2021

Hati hii inaorodhesha nyenzo za mtaala wa Kanisa zitakazotumika katika mwaka 2021. Kwa lugha nyingi, nyenzo hizi zinapatikana kidijitali katika app ya Gospel Library na kwenye ComeFollowMe.ChurchofJesusChrist.org. Vitu vipya kwa ajili ya mwaka 2021 vimezingatiwa.

Watu Binafsi na Familia

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 MPYA (16587)

Kama waumini katika kata au tawi lako wanaongea Kihiligainoni, Kisinhala, Kituruki, Kihindi, Kitamili, Kitelugu, au Kiurdu, tumia Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2021 (16899).

Msingi

Darasa la Chekechea (Umri wa Miezi 18–Miaka 2)

Tazama Watoto Wenu: Kitabu cha Kiada cha Chekechea (37108)

Wakati wa Kuimba na Madarasa Yote ya Msingi (Miaka 3–11)

Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 MPYA (16588)

Kama waumini wa kata au tawi lako wanaongea Kiamhariki, Kihilgainoni, Kihindi, kihimong, Kiaisilandi, Kilao, Kilingala, Kiserbia, Kishona, Kisinhala, Kislovaki, Kislovenia, Kitamili, Kitelugu, Kituruki, Kiurdu, Kixhosa, au Kizulu, tohoa mawazo kutoka Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa ajili ya matumizi katika Msingi, au tumia vitabu vingine vya kiada vya Kanisa kwa ajili ya watoto.

Shule ya Jumapili

Shule ya Jumapili kwa Watu Wazima na Vijana

Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 MPYA (16589)

Kama waumini katika kata au tawi lako wanaongea Kiamhariki, Kihiligainoni, Kihindi, Kihimong, Kiaiselandi, Kilao, Kilingala, Kiserbia, Kishona, Kisinhala, Kislovaki, Kislovenia, Kitamili, Kitelugu, Kituruki, Kiurdu, Kixhosa, au Kizulu, tohoa mawazo kutoka Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa matumizi katika Shule ya Jumapili, au tumia vitabu vya kiada vingine vya Kanisa.

Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama

Kujifunza kutoka katika Ujumbe wa Mkutano Mkuu” (toleo lililochapishwa linalopatikana katika chapisho la Ensign au Liahona)

Kama waumini wa kata au tawi lako wanaongea Kiamhariki, Kihiligainoni, Kihindi, Kihimong, Kiaiselandi, Kilao, Kilingala, Kiserbia, Kishona, Kisinhala, Kislovaki, Kislovenia, Kitamili, Kitelugu, Kituruki, Kiurdu, Kixhosa, au Kizulu, fundisha kutoka kwenye ujumbe wa mkutano mkuu wa hivi karibuni ambao unakidhi mahitaji ya akidi yako ya wazee au Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, au tumia vitabu vingine vya kiada vya Kanisa.

Ukuhani wa Haruni na Wasichana

Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 MPYA (16639)

Kama waumini wa kata au tawi lako wanaongea Kiamhariki, Kihiligainoni, Kihindi, Kihimong, Kiaiselandi, Kilao, Kilingala, Kiserbia, Kishona, Kisinhala, Kislovaki, Kislovenia, Kitamili, Kitelugu, Kituruki, Kixhosa, Kizulu, au Kiurdu, tumia masomo katika mlango wa 3 wa Preach My Gospel (16229). Pia ungeweza kufundisha kutoka katika ujumbe wa mkutano mkuu wa hivi karibuni ambao unakidhi mahitaji ya vijana wako.

Makundi Yote

Mkutano wa Baraza la Walimu

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kozi zingine (ikiwa vitabu vya kiada vinapatikana)

Kozi kwa ajili ya kuimarisha ndoa na familia, matayarisho ya kwenda hekaluni, na matayarisho ya umisionari hayatafanyika wakati wa saa ya pili ya Kanisa. Hata hivyo, kwa ridhaa ya askofu au rais wa tawi na kulingana na mahitaji ya eneo husika, kozi hizi zinaweza kufundishwa wakati mwingine kwa ajili ya watu binafsi, familia, au makundi.

Ndoa na Uhusiano katika Familia

Kitabu cha Kiada cha Mwalimu cha Ndoa na Uhusiano katika Familia (35865) na Mwongozo wa Mafunzo ya Ndoa na Uhusiano katika Familia kwa Mshiriki (36357)

Maandalizi ya kwenda Hekaluni

Endowed from on High: Temple Preparation Seminar Teacher’s Manual (36854) na Preparing to Enter the Holy Temple (36793)

Maelekezo kwa ajili ya Uagizaji wa Mtaala wa Mwaka kwa ajili ya Kata au Tawi

Kwa mwaka 2021, maaskofu na marais wa matawi watapokea nakala zilizochapishwa za Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa ajili ya kugawa kwa waumini katika kata au matawi yao. Watapokea nakala moja kwa ajili ya kila kaya inayohudhuria kikamilifu katika kata au tawi. Kata au matawi husika hayatahitajika kugharamia nakala hizi. Hata hivyo, kata au matawi yatahitajika kuagiza na kulipia nakala zilizochapishwa za vitabu vya kiada kwa ajili ya kutumia katika Msingi, Shule ya Jumapili, na Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana.

Unaweza kuagiza nyenzo kwa ajili ya tawi au kata kuanzia Juni 30, 2020. Tafadhali weka oda yako kabla ya Agosti 31, 2020. Nyenzo zitakazoagizwa baada ya tarehe hii zinaweza zisifike ifikapo Januari 1, 2021. Kuagiza nyenzo zilizochapishwa, tembelea store.ChurchofJesusChrist.org, chagua Units and Callings, na kisha chagua Annual Curriculum.

Zingatia maswali yafuatayo ili kukusaidia kuepuka kuagiza nakala zilizochapishwa zaidi ya zinazohitajika:

  • Ni nakala ngapi za kila nyenzo zilizochapishwa tayari ziko kwenye tawi au kata yako?

  • Ni walimu wangapi wanatumia nyenzo katika mfumo wa kidijitali badala ya nakala zilizochapishwa?

Nyenzo kwa ajili ya Wale Walio na Ulemavu

Nyenzo katika mfumo wa sauti, katika mfumo wa maandishi kwa ajili ya wenye ulemavu wa uoni, na katika maandishi makubwa pia zinapatikana katika store.ChurchofJesusChrist.org.

Chapisha