Kuhusu Magazeti ya Kanisa
Liahona
Jifunze kuhusu Liahona


Liahona,” Jan. 2021.

Liahona

Kutuelekeza Sisi Sote kwa Yesu Kristo

Picha
mwanamume akisoma gazeti

Katika Kitabu cha Mormoni, tunasoma kwamba Bwana alitayarisha Liahona ili kumsaidia Lehi na familia yake kuendelea katika safari yao. Ilikuwa ni “dira, ambayo ingewaonyesha njia iliyonyooka kwenda kwenye nchi ya ahadi” (Alma 37:44). Chini ya maelekezo ya manabii wanaoishi, gazeti la Liahona katika siku zetu ni mwongozo unaokwenda pamoja nasi katika safari yetu na kuelekeza njia ya kumfuata Yesu Kristo, hata katikati ya dhoruba.

Liahona Mpya

Gazeti la Liahona kwa ajili ya watu wazima linaangazia mafundisho na huduma ya viongozi wa Kanisa, linashiriki makala za kutia moyo yanyoonyesha jinsi ya kutumia kanuni za injili, kuunga mkono kujifunza injili nyumbani na kutoa umaizi katika mada za Njoo, Unifuate.

Mwongozo kutoka kwa Manabii Wanaoishi

Kila toleo lina makala mpya, ya kipekee iliyotayarishwa na mshiriki wa Urais wa Kwanza au Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Soma kile manabii na mitume wanafundisha leo.

Hadhira Muhimu

Gazeti la Liahona hutoa nyenzo za injili zenye msukumo kwa waumini wote watu wazima, ikijumuisha maudhui kwa watu wazima waseja, vijana, waumini wapya, waumini waliokomaa na wazazi. Kwa vijana wakubwa, na Liahona pia huchapisha baadhi ya makala zinazopatikana ndani VW Kila Wiki, gazeti la kidijitali kwa vijana.

Kufikia Ulimwenguni

Liahona inajitahidi kuwabariki waumini kote ulimwenguni. Gazeti huchapishwa katika lugha 23 kila mwezi katika miundo ya kidijitali na uchapishaji na katika lugha 25 za ziada kila miezi miwili katika miundo ya kidijitali na ya kuchapisha. Uteuzi wa jumbe muhimu unafanywa upatikane kidijitali ili kusambazwa ndani ya nchi katika lugha 39 za ziada. Hii inafanya maudhui ya Liahona kupatikana kwa waumini katika lugha 87 kila mwezi.

Makala zaidi za Kidijitali

Je, ulijua kwamba Liahona huchapisha maudhui zaidi ya yale utakayoyapata kwenye gazeti lililochapishwa? Nyongeza hizi za kidijitali zinaweza kupatikana katika liahona.ChurchofJesusChrist.org au katika Liahona katika programu ya Maktaba ya Injili.

Makala Maalum ya Eneo

Liahona kamili inatafsiriwa katika lugha 48. Takribani kila toleo likijumuisha maudhui yaliyotolewa na kamati za wafanyakazi wa eneo husika au wafanyakazi wa kujitolea. Maudhui haya ya eneo husika ni pamoja na jumbe kutoka kwa washiriki wa Urais wa Eneo, makala kuhusu matukio ya eneo husika, hadithi na shuhuda kutoka kwa waumini wa eneo hilo, na zaidi. Kwa maeneo mengi, maudhui haya yanapatikana katika Liahona ya mtandaoni kila mwezi katika Maktaba ya Injili.

Tutumie Hadithi Yako

Liahona inataka kusikia kutoka kwako. Unaweza kuwatia moyo waumini ulimwenguni kote unaposhiriki uzoefu wako wa kuishi injili. Wasilisha makala zako, mawazo na maoni kwenye Liahona online.

Jisajili Sasa

Kwa taarifa zaidi za kujisajili kwenye Liahona, tembelea online store na uchague lugha unayotaka. Kurasa za eneo husika zitajumuishwa kiotomatiki kulingana na eneo lako.

Kumbuka: Inaweza kuchukua hadi miezi mitatu kwa usajili wako kukamilika.

Chapisha