Hadithi za Maandiko
Yusufu akiwa Misri


“Yusufu akiwa Misri,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Yusufu akiwa Misri,” Hadithi za Agano la Kale

Mwanzo 39–41

Yusufu akiwa Misri

Mtumwa anakuwa kiongozi

Yusufu aliuzwa kwa Potifa

Yusufu aliuzwa kama mtumwa kwa mtu aliyetwa Potifa. Potifa alifanya kazi kwa Farao, mtawala wa Misri. Potifa aliweza kusema kwamba Bwana alimsaidia Yusufu. Alimwamini Yusufu na akamweka kuwa mkuu wa nyumba yake na kila alichokimiliki.

Mwanzo 39:1–6

Yusufu akimwambia mke wa Potifa hapana.

Mke wa Potifa alimpenda Yusufu. Alimtaka Yusufu avunje amri za Bwana pamoja naye. Yusufu alimwambia hapana.

Mwanzo 39:7–10

Yusufu akimkimbia mke wa Potifa.

Mke wa Potifa hakumsikiliza, hivyo Yusufu akamkimbia Alimkasirikia Yusufu.

Mwanzo 39:11–12

Mke wa Potifa akizungumza na Potifa

Alimwonyesha Potifa kipande cha nguo cha Yusufu. Alimdanganya Potifa kuhusu Yusufu. Potifa alimweka Yusufu gerezani.

Mwanzo 39:13–20

Yusufu akiwa gerezani

Yusufu alikuwa ametengwa na familia yake. Alikuwa mtumwa, na sasa amekuwa mfungwa. Lakini Bwana bado alimsaidia Yusufu. Yusufu hakukata tamaa. Bwana alimbariki mlinzi wa gereza ili kuona yaliyo mazuri katika Yusufu. Mlinzi wa gereza walianza kumwamini, hivyo akamweka Yusufu kuwa mkuu wa wafungwa wengine.

Mwanzo 39:21

Yusufu akitafsiri ndoto za wafungwa wengine

Yusufu alikutana na wafungwa wawili, muokaji na mnyweshaji, ambao waliwahi kuwa wafanyakazi wa Farao. Wote wawili waliota ndoto za ajabu. Kwa uweza wa Bwana, Yusufu alielezea ndoto zile zilimaanisha nini. Ndoto ya yule mnyweshaji ilimaanisha kwamba mnyweshaji angeachiliwa huru. Siku tatu baadae, yule mnyweshaji aliachiliwa huru ili afanye kazi kwa Farao tena.

Mwanzo 39:22–23; 40:1–21

Farao anafadhaika

Siku moja Farao alifadhaishwa na ndoto zake. Hakuna mtu aliyeweza kumwambia ndoto zake zina maana gani.

Mwanzo 41:1–8

mnyweshaji akizungumza na Farao

Kisha mnyweshaji akakumbuka kwamba Yusufu angeweza kuelezea maana ya ndoto.

Mwanzo 41:9–13

Yusufu anatafsiri ndoto za Farao

Yusufu alitolewa gerezani ili aelezee maana ya ndoto za Farao. Yusufu alisema ndoto zilimaanisha kwamba Misri ingekuwa na miaka saba yenye chakula kingi ikifuatiwa na miaka saba ya baa la njaa kukiwa na chakula kidogo sana. Yusufu alimwambia Farao kwamba Misri inapaswa kuweka akiba ya chakula hicho cha ziada katika miaka saba ya neema.

Mwanzo 41:14–36

Yusufu akimwonyesha Farao hifadhi ya chakula

Farao alijua kwamba kile ambacho Yusufu alisema kuhusu ndoto zake kilikuwa cha kweli. Akamwachilia huru Yusufu kutoka gerezani na kumfanya Yusufu kuwa kiongozi mkubwa katika Misri. Kwa miaka saba, Yusufu aliisaidia Misri kuhifadhi ghalani chakula cha ziada.

Mwanzo 41:37–53

watu wakisafiri katika Misri

Kisha baa la njaa likaingia. Katika wakati huu, hakukuwa na mtu yeyote aliyeotesha chakula cho chote. Watu walisafiri kwenda Misri kununua chakula ambacho Yusufu alikuwa amekihifadhi. Kwa sababu ya Yusufu, Wamisri walihifadhi chakula cha kutosha ili kuwasaidia wao na watu wengine kuokoka na baa la njaa.

Mwanzo 41:54–57