Hadithi za Maandiko
Ruthu na Naomi


“Ruthu na Naomi,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Ruthu na Naomi,” Hadithi za Agano la Kale

Ruthu 1–4

Ruthu na Naomi

Kuvumilia majaribu kwa upendo na uaminifu

Naomi na familia wakiingia kwenye mji

Naomi na familia yake walihamia Moabu kwa sababu hapakuwa na chakula cha kutosha katika nchi ya Yuda. Kisha mume wa Naomi alifariki. Wana wa Naomi walioa wanawake kutoka Moabu walioitwa Orpa na Ruthu. Walimtunza Naomi kwa miaka 10.

Ruthu 1:1–4

Orpa, Ruthu na Naomi wakikumbatiana

Kisha mume wa Orpa na wa Ruthu walifariki. Sasa wanawake walikuwa peke yao. Naomi hakuweza kuwalisha Ruthu na Orpa.

Ruthu 1:5, 8–10

Ruthu na Naomi wakisafiri kwa ngamia

Orpa alirudi nyumbani. Lakini Ruthu alitaka kubakia na kumtunza Naomi. Ruthu na Naomi walisikia kwamba nchi ya Yuda ilikuwa na mazao tena, hivyo walisafiri kwenda huko.

Ruthu 1:16–19

Ruthu akikusanya nafaka

Ruthu na Naomi walifika Yuda wakati wa mavuno. Walihitaji chakula. Ndugu wa Naomi aliyeitwa Boazi alimiliki mashamba katika Yuda. Alimruhusu Ruthu kuchukua masazo ya nafaka kwenye mashamba yake. Ilikuwa kazi ngumu.

Ruthu 1:22; 2:3

Boazi akizungumza na Ruthu

Boazi alimheshimu Ruthu kwa sababu Ruthu alifanya kazi kwa bidii na kwa sababu alikuwa mwaminifu kwa Naomi na kwa Bwana. Aliwaambia watumishi waache nafaka nyingi kwenye mashamba kwa ajili ya Ruthu.

Ruthu 2:5–17

Ruthu na Naomi

Naomi alitaka Ruthu awe na familia. Alimuhimiza Ruthu aolewe na Boazi. Ruthu alijua kwamba ikiwa yeye na Boazi wangeoana, kwa pamoja wangeweza kumtunza Naomi.

Ruthu 3:1–2; 4:15

Ruthu na Boazi

Ruthu aliamua kumwomba Boazi amwoe. Boazi alifahamu kwamba Ruthu alikuwa mwanamke mwaninifu na mwema. Boazi alikubali.

Ruthu 3:3–18; 4:13

Ruthu, Boazi na mtoto

Ruthu na Boazi walioana. Baada ya muda mfupi Ruthu alipata mtoto wa kiume. Alikuwa babu wa Daudi, mfalme wa siku zijazo. Miaka mingi baadaye, Yesu Kristo alizaliwa kwenye ukoo wa familia hii.

Ruthu 4:13–17