Kuwaimarisha Waumini Wapya
Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi


“Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi,” Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi (2020)

“Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi,” Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi

Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi

Waumini na wamisionari wana jukumu muhimu katika kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi kuendelea kwenye njia ya agano. Urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanawajibika kwa juhudi za kila siku za umisionari katika kata, ikiwa ni pamoja na kuwatunza waumini wapya na wanaorudi. Chini ya maelekezo ya rais wa kigingi na askofu, marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanawajibika kuhakikisha kwamba viongozi wa kata na akina kaka na dada wahudumiaji wanapokea na kutendea kazi maelekezo yanayofuata.

Kwa waumini wapya na wanaorudi ili kuweza kubakia kwenye njia ya agano, ni muhimu kwao (1) kuhisi kuwa wao wanastahili kupitia mahusiano yaliyoimarishwa kwa Mungu na waumini wengine, (2) kuamini katika Yesu Kristo na kuimarisha imani yao Kwake, na ( 3) kuwa wanafunzi wa Kristo kupitia uzoefu muhimu.

Shughuli zifuatazo zitakusaidia kujifunza jinsi ya kutumia rasilimali mpya ili kusaidia katika juhudi hii. Shughuli hizi zinaweza kufanywa katika mazingira ya baraza la kigingi au kata wakiwepo wamisionari wa muda wote. Sehemu mbili za kwanza zinapaswa pia kutolewa kwa wenzi wa kuhudumia waliopangwa kwa waumini wapya.

Chati: Kuwasaidia Waumini Wapya Kubaki kwenye Njia ya Agano

  1. Fungua Maktaba ya Injili (programu au ukurasa wa wavuti) na nenda kwenye Vitabu vya Maelekezo na Miito, kisha Wito wa Kata au Tawi, na kisha Kuwaimarisha Waumini Wapya. (Nyenzo utakazohitaji kwa ajili ya mafunzo haya zinapatikana katika sehemu hii.) Fungua na upitie “Kuwasaidia Waumini Wapya Kubaki kwenye Njia ya Agano.” Kama ushirika au kikundi, jadilini:

    • Kwa nini uzoefu huu ni muhimu kwa ajili ya kuwasaidia watu kuingia na kubaki kwenye njia ya agano?

  2. Tazama sehemu ya video “Hadithi ya Familia ya Bush” (katika sehemu ya Video ya Kuwaimarisha Waumini Wapya).

    Unapotazama video hiyo, tafuta jinsi vipengele vilivyo kwenye chati chini ya “Kabla ya Ubatizo,” “Punde Baada ya Ubatizo,” na “Ndani ya Mwaka Mmoja” vinavyotekelezwa. Jadilini:

    • Nini tunafanya vizuri kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi ili wasonge mbele?

    • Je! Ni sehemu gani moja au mbili tunahisi tunaweza kuboresha?

  3. Tazama kipande cha video “Umuhimu wa Urafiki.” Jadilini:

    • Kwa nini kuwa na urafiki wa kweli na waumini ni moja ya sababu imara katika kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi kuingia na kubaki kwenye njia ya agano?

    • Tunawezaje kusaidia kujenga urafiki wa kweli mapema iwezekanavyo? Je! Tunawezaje kudumisha urafiki huu?

  4. Tazama sehemu ya video “Kufanya kazi Pamoja.” Jadilini:

    • Je! waumini na wamisionari walifanyaje kazi pamoja ili kukidhi mahitaji ya familia ya Bush?

    • Ni nini kingeweza kuboreshwa katika kitengo chetu ili kuwa na waumini na wamisionari wafanye kazi pamoja kwa ufanisi zaidi katika juhudi hizi?

Njia Yangu ya Agano

  1. Katika sehemu hiyo hiyo katika Maktaba ya Injili, fungua Njia Yangu ya Agano na kisha nenda “Njia yangu ya Agano” utangulizi. Someni ukurasa huu pamoja na mjadili jinsi gani Njia yangu ya Agano ingeweza kutumika kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi. Pitieni angalau uzoefu wa aina mbili ndani ya Njia Yangu ya Agano. Jadilini:

    • Akina kaka na akina dada wahudumiaji wanawezaje kufanya kazi pamoja kuwasaidia waumini wapya au wanaorudi?

    • Je! Uzoefu huu unawezaje kutoa nafasi nzuri ya kurudia masomo ya umisionari baada ya kubatizwa? (Ona uzoefu “Jifunze kuhusu Ukuhani wa Haruni” na “Pata Kibali cha Hekaluni kwa ajili ya Ubatizo na Uthibitisho kwa Niaba.”)

  2. Panga jinsi utakavyosaidia waumini wapya na wanaorudi unaowahudumia kupata ufikiaji kwenye Njia Yangu ya Agano. Ikiwa wanatumia kifaa cha Androidi, wanaweza kupakua programu kutoka Google Play store hapa. Ikiwa wanatumia kifaa cha iOS, wanaweza kupakua programu kutoka programu ya Apple Store hapa. Unaweza kutoa nakala iliyochapishwa (Kumbuka: Waumini wapya na wanaorudi wanaweza kupata Njia yangu ya Agano katika Mkusanyiko wa hadhira ya Watu Wazima, Waumini Wapya au Waumini Wanaorudi wa Maktaba ya Injili.)

Maendeleo kwenye Njia ya Agano

Uaskofu na marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanaweza kupata na kusasisha maendeleo ya muumini mpya kupitia Maendeleo kwenye Njia ya Agano.

  1. Fungua programu ya Zana za Muumini (au Rasilimali za Kiongozi na Karani [LCR] mtandaoni), nenda kwenye Ripoti, na kisha chagua Maendeleo kwenye Njia ya Agano. Mtazamo huu unaonyesha taarifa muhimu juu ya wale ambao wamebatizwa na wanaishi katika kitengo chako ndani ya miaka miwili iliyopita. Pitia orodha ya waumini wapya na jadilini jinsi wanavyoendelea.

  2. Chagua jina la muumini mpya (au chagua Angalia Taarifa katika LCR na IOS). Maelezo ya ziada juu ya maendeleo ya mtu huonyeshwa. Jadilini:

    • Kuna uhusiano gani kati ya taarifa hii na Njia Yangu ya Agano?

    • Ni nini kinahitajika kutokea kusaidia kila mmoja wa waumini wetu wapya kuendelea?

  3. Taarifa inaweza kusasishwa katika programu na uaskofu (ikiwa ni pamoja na makarani na makatibu), marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi, muumini mpya, kiongozi wa misheni wa kata, kiongozi msaidizi wa misheni wa kata na wamisionari wa kata. Wakati wamisionari wanapoongeza taarifa kwenye kitabu cha Mpango wa Eneo, Rekodi ya Maendeleo inasasishwa kiautomatiki. Ili kujipa uzoefu wa hili, chagua jina la muumini mpya (au chagua Angalia Maelezo katika LCR na IOS) na fanya kazi kama zifuatazo:

    • Nakili mahudhurio ya mkutano wa sakramenti. (Kumbuka: Ikiwa muumini mpya hawezi kuhudhuria mkutano wa sakramenti kwa sababu za kiafya, weka alama kwenye mduara ikiwa muumini mpya ameweza kupokea sakramenti nyumbani au kuhudhuria mkutano wa sakramenti akiwa mbali.)

    • Ongeza jina la rafiki kwenye taarifa ya muumini mpya.

    • Sasisha kanuni zilizofundishwa (masomo ya umisionari baada ya kubatizwa).

    • Hakikisha taarifa kuhusu akina kaka na akina dada wahudumiaji ni sahihi.

  4. Viongozi wafuatao wanaweza kuona tu taarifa za Maendeleo kwenye Njia ya Agano:

    • Urais wa kigingi, ikiwa ni pamoja na makarani na makatibu

    • Washauri wakuu

    • Urais wa Muungano wa Usaidizi wa kigingi

    • Urais wa misheni, ikiwa ni pamoja na mwenzi na makarani na makatibu, kupitia Nyenzo za Kiongozi na Karani pekee

    • Washiriki wa urais wa Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi

    • Viongozi wa hekalu na historia ya familia wa kata

    • Washiriki wa urais wa Msingi, Wasichana na Shule ya Jumapili

  5. Arafa za ndani ya programu zitaonekana wakati Maendeleo ya mtu ya Njia ya Agano yanapendekeza ushiriki mdogo katika shughuli za Kanisa.

  6. Waumini wapya wanaweza pia kusasisha maendeleo yao wenyewe. Waruhusu waumini wapya wafuatilie taarifa zao binafsi kutoka kwenye kielekezo katika Nyenzo za Muumini. Kisha, mruhusu muumini mpya abofye kwenye Maendeleo kwenye Njia ya Agano. Fikiria kumwonyesha muumini mpya jinsi ya kufanya hivyo.

  7. Marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanawajibika kuhakikisha taarifa ya muumini mpya imesasishwa kwa wakati sahihi. Wanaweza kunaibisha jukumu hili. Jadilini kuhusu nani atasasisha taarifa ya muumini mpya, mara ngapi (inapendekezwa angalau kila wiki) itasasishwa na ni jinsi gani Maendeleo kwenye Njia ya Agano yatatumika kwenye baraza la kata na mikutano ya uratibu ya kila wiki.

Hitimisho

  1. Onyesha sehemu ya video “Jinsi Mahekalu na Historia ya Familia Vinavyowaimarisha Waumini Wapya.”

    Jadilini jinsi juhudi zenu zinavyoweza kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi kubaki kwenye njia ya agano (ona Yohana 15:16) na mwishowe kupokea ibada zote za wokovu na kuinuliwa. Pangeni kile ambacho kitengo chenu kitafanya ili kuwalea waumini wapya na wanaorudi katika kutaniko lenu.

Chapisha