“Muhtasari wa Kufundisha kama Kristo,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi (2022)
Muhtasari wa Kufundisha kama Kristo
Majedwali yafuatayo yanatoa muhtasari wa kanuni zilizofundishwa katika nyenzo hii.
Fokasi kwa Yesu Kristo
Fundisha kuhusu Yesu Kristo Bila KujalI Kile Unachokifundisha
-
Sisitiza Mfano wa Yesu Kristo.
-
Fundisha kuhusu majina, wajibu, na sifa za Yesu Kristo.
-
Tafuta Ishara ambazo hushuhudia juu Yesu Kristo.
Wasaidie Wanafunzi Waje kwa Yesu Kristo
-
Wasaidie wanafunzi watambue upendo, nguvu na rehema za Bwana katika maisha yao.
-
Wasaidie wanafunzi waimarishe uhusiano wao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
-
Wasaidie wanafunzi kwa makusudi kabisa wajitahidi kuwa zaidi kama Yesu Kristo
Kanuni za Kufundisha Kama Kristo
Wapende Wale Unaowaafundisha
-
Waone wanafunzi katika njia ambayo Mungu anawaona.
-
Tafuta kuwajua—kuelewa hali zao, mahitaji yao na nguvu zao.
-
Waombee wao kwa majina.
-
Tengeneza mazingira salama ambapo wote wanaheshimiwa na kujua michango yao inathaminiwa.
-
Tafuta njia sahihi za kuonyesha upendo wako.
Fundisha kupitia Roho
-
Jiandae mwenyewe kiroho.
-
Daima kuwa tayari kuitikia misukumo ya kiroho kuhusu mahitaji ya wanafunzi.
-
Tengeneza mazingira na fursa kwa ajili ya wanafunzi kufundishwa na Roho Mtakatifu.
-
Wasaidie wanafunzi watafute, watambue na watendee kazi ufunuo binafsi.
-
Toa ushuhuda kila mara, na waalike wanafunzi washiriki hisia zao, uzoefu wao na shuhuda zao.
Fundisha Mafundisho
-
Jifunze mafundisho ya Yesu Kristo wewe mwenyewe.
-
Fundisha kutoka katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho.
-
Wasaidie wanafunzi watafute, watambue na waelewe kweli katika maandiko.
-
Fokasi kwenye kweli ambazo zinaongoza kwenye uongofu na kujenga imani katika Yesu Kristo.
-
Wasaidie wanafunzi wapate uhusiano binafsi katika mafundisho ya Yesu Kristo.
Alika Kujifunza kwa Bidii
-
Wasaidie wanafunzi wawajibike kwa kujifunza kwao wenyewe.
-
Wahimize wanafunzi waje kumjua Mwokozi kwa kujifunza injili kila siku.
-
Waalike wanafunzi wajiandae kujifunza.
-
Wahimize wanafunzi kushiriki kweli wanazojifunza.
-
Waalike wanafunzi kuishi kile wanachojifunza.