“Neno la Hekima,” Rafiki, Agosti. 2021.
Ujumbe wa Kila Mwezi wa Gazeti la Rafiki Agosti 2021
Neno la Hekima
Joseph Smith alifanya mikutano ili kuwafundisha watu kuhusu injili. Wakati mwingine wanaume walivuta na kutafuna tumbaku.
Hili lilimtia wasiwasi Emma Smith. Moshi na tumbaku vilisababisha tatizo kubwa, na haikuonekana sawa. Emma na Joseph walijiuliza jinsi Mungu alivyohisi kuhusu hili.
Joseph alisali na Bwana akajibu. Bwana aliwaonya waumini wa Kanisa kuhusu kuvuta sigara na tumbaku. Alisema kuwa si nzuri kwa miili yetu. Pia aliwaonya kuhusu kunywa chai, kahawa na pombe.
Mungu alisema tule matunda, mboga za majani na vyakula vingine vyenye afya. Tunayaita mafundisho haya Neno la Hekima.
Ninaweza kuishi Neno la Hekima. Baba wa Mbinguni atanibariki ninapoutunza mwili wangu.
© 2021 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Kila Mwezi ya Ujumbe wa Rafiki, Agosti 2021. Swahili. 17471 743