“Musa na Mana,” Jumbe za kila Mwezi za Rafiki, Aprili 2022
“Musa na Mana”
Jumbe za kila Mwezi za Rafiki, Aprili 2022
Musa na Mana
Vielelezo na Apryl Stott
Musa alikuwa nabii. Aliwaongoza watu wa Mungu kuelekea nchi ya ahadi. Walitembea kwa siku nyingi.
Watu walikuwa na njaa. Hawakuwa na chakula. Hivyo Mungu aliwatumia chakula kutoka mbinguni. Kiliitwa mana.
Kila asubuhi, watu walikusanya mana ili wale. Lakini mana isingefaa kama ingekaa zaidi ya usiku mmoja. Ilibidi wakusanye zaidi siku iliyofuatia.
Mana hutukumbusha sisi kuhusu Yesu Kristo. Mungu alituma mana ili kuwaokoa watu. Yeye pia alimtuma Yesu duniani ili kutuokoa sisi. Tunamhitaji Yesu kila siku, kama tunavyohitaji chakula kila siku.
Nitamfuata Yesu. Yeye atanipa nguvu na kunisaidia kuhisi upendo Wake kila siku.
Ukurasa wa Kupaka Rangi
Tunamhitaji Yesu Kila Siku
Bonyeza kwenye picha ili kupakua.
Kielelezo na Apryl Stott
Je, Yesu anakusaidia vipi?
© 2022 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, April 2022. Swahili. 18314 743