“Mwokozi Anayeteseka,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Aprili 2022.
Ujumbe wa kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Aprili 2022
Mwokozi Anayeteseka
Mamia ya miaka kabla ya Yesu Kristo kuja, Isaya alitoa unabii wa kuteseka kwake kwa ajili ya dhambi zetu.
kudharauliwa na kukataliwa
Wakati Yesu Kristo alipokuja duniani, watu wengine walimwamini, lakini wengi hawakumwamini. Hata walimdharau na wengi wakamchukia. Mwishowe, watu waliamua ateswe na kuuawa. (Ona 1 Nefi 19:9.)
amezibeba huzuni zetu
Yesu Kristo alibeba maumivu, ugonjwa na unyonge wetu wote. Alifanya haya ili atuhurumie na kujua jinsi ya kutusaidia. (Ona Alma 7:11–13.)
aliumia kwa ajili ya makosa yetu
Yesu Kristo aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu. Alifanya haya ili tusamehewe tunapotubu. (Ona Mafundisho na Maagano 18:11; 19:15–19.)
na kwa mapigo yake tunaponywa
“Mapigo yake” ni vidonda Vyake. Haya yanasimamia mateso yote aliyovumilia kwa ajili yetu, ikiwemo kumwaga damu na kifo chake. Kwa sababu Yesu Kristo aliteseka kwa ajili yetu, tunaweza kufanywa upya tena. Dhabihu Yake inawezesha dhambi zetu kusamehewa. Tunapotubu na kujaribu kushika maagano yetu, anatuponya na kutubadilisha. (Ona Mosia 3:7–11; Makala ya Imani 1:3.)
© 2022 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly For the Strength of Youth Message, Aprili 2022. Swahili. 18314 743