“Chagua,” Kwa Ajili ya Nguvu ya Vijana, Juni 2022
Ujumbe wa kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Juni 2022
Chagua
Yoshua aliwahimiza watu wake wafanye uamuzi sahihi—wa kumfuata Bwana.
chagua
Uwezo wetu wa kuchagua na kujitendea unaitwa uhuru wa kuchagua. Ni sehemu muhimu ya mpango wa Baba wa Mbinguni. Kusudi moja la maisha haya ni kuonyesha kwamba tutachagua kutii amri za Mungu ili tuwe zaidi kama Yeye. Tutahukumiwa kulingana na chaguzi zetu. (Ona 2 Nefi 2:27; Mafundisho na Maagano 101:78; Abrahamu 3:25.)
leo hii
Yoshua aliwahimiza watu wake wachague “leo hii,” au sasa hivi. Tunaweza kufanya maamuzi muhimu mara moja na kisha kujaribu kuyatimiza. (Ona Zaburi 37:5.)
hudumu
Katika mstari huu, kutumikia kunamaanisha kuabudu, kusaidia, kutii na kujitoa kwa ajili ya mtu fulani. Tunapaswa kumtumikia Bwana (ona Musa 1:15).
miungu
Israeli ilikuwa imeamriwa kumtumikia Mungu wa kweli na aliye hai, Yesu Kristo (ona Kutoka 20:2–5). Yoshua alitoa mifano ya miungu mingine ambayo watu wake hawapaswi kuabudu. Miungu mingine katika maisha yetu inaweza kuwa ni pamoja na mali, maoni ya wengine, vivutio vingine—chochote kinachotutoa kwa Bwana.
mimi na nyumba yangu
Yoshua aliongea kujihusu mwenyewe na nyumba yake. Alisema watamtumikia Bwana. Alitaka kuongoza familia yake kwa uadilifu na kuwafunza kumfuata Bwana (ona Mafundisho na Maagano 93:40).
© 2022 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly For the Strength of Youth Message, June 2022. Swahili. 18315 743