2022
Taa ya Miguu Yetu
Agosti 2022


“Taa ya Miguu Yetu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Agosti 2022.

Ujumbe wa kila Mwezi Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Agosti 2022

Taa ya Miguu Yetu

Chombo cha kawaida kwa Waisraeli wa kale kinaweza kutufundisha jinsi Bwana anavyotuongoza sisi.

taa ya mafuta

Ukweli

Katika nyakati za Agano la Kale, watu walitumia taa za mafuta ili kubeba mwanga gizani. Nyingi za taa hizi zilikuwa na maumbile matatu ya msingi.

  1. Bakuli ya udongo ya kuwekea mafuta ya mzeituni; ndogo kutosha kushikiliwa kwenye kiganja cha mkono wa mtu.

  2. Utambi wa kitani uliwashwa baada kufyonza mafuta.

  3. Mdomo au neli ya kushikilia utambi

Taa za kawaida za mafuta zikiwa na utambi mmoja tu zingetoa nuru futi chache tu kuzunguka walipo wao. Ikiwa zitatumika wakati ukitembea, zingetoa nuru ya kutosha kuona hatua moja mbele yako mwenyewe ili kwamba uweze kutembea kwa makini zaidi gizani.

Kile Tunachoweza Kujifunza

Yesu ameshikilia taa ya mafuta

Imetumika kwa ruhusa. Ongoza, Angaza Pole Pole, na Simon Dewey. Kwa hisani ya altusfineart.com © 2022.

Neno la Bwana linaweza kuangaza njia yetu kutuvusha kwenye giza na mkanganyiko ambao unatuzunguza sisi ulimwenguni.

Bwana ametuomba tusifunike mwanga wetu bali tuibebe nuru ya injili pamoja nasi hili kwamba wengine waweze kuiona (ona Mathayo 5:14–16).

Ni juu yetu kuhakikisha kwamba taa zetu zimejazwa mafuta (ona Mathayo 25: 1–13). Tunafanya hivi kupitia maombi, kujifunza maandiko, huduma, kumfuata nabii, na matendo mengine ya imani na ibada (ona Spencer W. Kimball, Faith Precedes the Miracle [1972], 256).

Kama tutaifanyia kazi imani, Bwana wakati mwingine ataangaza njia vya kutosha kwetu kuchukua hatua moja zaidi (ona Boyd K. Packer, “The Candle of the Lord,” Ensign, Jan. 1983, 54).