2022
Usisubiri! Kuwa Kama Wachungaji
Disemba 2022


“Usisubiri! Kuwa Kama Wachungaji,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Dis. 2022.

Ujumbe wa kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Disemba 2022

Luka 2:8–20

Usisubiri! Kuwa Kama Wachungaji

Picha
wachungaji

Katika usiku ulio kimya hapo kale, wachungaji walichunga kwa bidii mifugo yao.

Picha
kondoo

Wachungaji walikuwa na kazi muhimu. Kondoo walihitaji chakula, maji na kukingwa dhidi ya hatari.

Picha
malaika

Ghafla, malaika alitokea!

“Msiogope, kwani tazama, naleta kwenu habari njema na ya furaha. … Maana leo … amezaliwa, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.”

Picha
malaika

Malaika aliwaambia wachungaji wangemkuta mtoto amefunikwa kwa nguo, akiwa amelala horini huko Bethlehemu.

Picha
kwaya ya malaika

Kwaya ya malaika ilijaza anga na kuungana katika kumtukuza Mungu.

“Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”

Picha
wachungaji

“Acha twende Bethlehemu na tuone kile Bwana ametujulisha.”

Picha
Wachungaji wakiifuata nyota

Wachungaji hawakusubiri. Hili ilikuwa muhimu sana! “Wakaondoka kwa haraka” kwenda Bethlehemu.

Picha
wachungaji horini

Wachungaji walimkuta Yesu akiwa amefunikwa kwa nguo, amelala horini, kama malaika alivyosema.

Picha
mtoto Yesu

Huyu alikuwa ni Masihi aliyetabiriwa ambaye alikuja ili kuwa Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu na kutuletea furaha ya kweli!

Picha
wachungaji

Wachungaji walifurahi sana! Walishiriki kile walichokisikia na kuona.

“Mwokozi wa ulimwengu amezaliwa!”

“Masihi hatimaye amekuja!”

Picha
mvulana akijifunza maandiko

Wachungaji “walienda kwa haraka” kwa Yesu. Nawe pia unaweza fanya hivyo!

Unaweza kujifunza kuhusu Yeye.

Picha
mvulana akikata nyasi

Unaweza kumtumikia kwa kuwatumikia wengine.

Picha
msichana akishiriki Kitabu cha Mormoni na mvulana

Unaweza kushuhudia kuhusu Yeye.

Chapisha