“Usisubiri! Kuwa Kama Wachungaji,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Dis. 2022. Ujumbe wa kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Disemba 2022 Luka 2:8–20 Usisubiri! Kuwa Kama Wachungaji Na Eric B. Murdock; Kielelezo na Darren Rawlings Katika usiku ulio kimya hapo kale, wachungaji walichunga kwa bidii mifugo yao. Wachungaji walikuwa na kazi muhimu. Kondoo walihitaji chakula, maji na kukingwa dhidi ya hatari. Ghafla, malaika alitokea! “Msiogope, kwani tazama, naleta kwenu habari njema na ya furaha. … Maana leo … amezaliwa, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.” Malaika aliwaambia wachungaji wangemkuta mtoto amefunikwa kwa nguo, akiwa amelala horini huko Bethlehemu. Kwaya ya malaika ilijaza anga na kuungana katika kumtukuza Mungu. “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.” “Acha twende Bethlehemu na tuone kile Bwana ametujulisha.” Wachungaji hawakusubiri. Hili ilikuwa muhimu sana! “Wakaondoka kwa haraka” kwenda Bethlehemu. Wachungaji walimkuta Yesu akiwa amefunikwa kwa nguo, amelala horini, kama malaika alivyosema. Huyu alikuwa ni Masihi aliyetabiriwa ambaye alikuja ili kuwa Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu na kutuletea furaha ya kweli! Wachungaji walifurahi sana! Walishiriki kile walichokisikia na kuona. “Mwokozi wa ulimwengu amezaliwa!” “Masihi hatimaye amekuja!” Wachungaji “walienda kwa haraka” kwa Yesu. Nawe pia unaweza fanya hivyo! Unaweza kujifunza kuhusu Yeye. Unaweza kumtumikia kwa kuwatumikia wengine. Unaweza kushuhudia kuhusu Yeye. © 2022 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly For the Strength of Youth Message, Decemba 2022. Swahili. 18318 743