Historia ya Kanisa
“Sisi Ni Sehemu Yao”


“Sisi Ni Sehemu Yao”

Mnamo 2015, Brian Kigundu alikuwa kiongozi wa genge lenye silaha la vijana wa mtaani huko Kibera, eneo la mjini karibu na Nairobi lenye idadi kubwa ya watu kwa mamia na maelfu—eneo kubwa la kipekee Afrika. Wengi wa wakazi wa Kibera walipata chini ya dola 2 kwa siku. Kulikuwa na shule chache kwa sababu wengi wa watu hawakuweza kumudu elimu kwa ajili ya watoto wao. Huduma za msingi kama vile umeme, maji yatiririkayo, vyoo na huduma za afya mara nyingi hazikupatikana Kibera.

Karibu na eneo jirani lenye nyumba nyingi ndogo ndogo na chakavu, mitaa na reli, misuguano ilikuwa ikiibuka kutokana na migongano ya kisiasa na mirindimo ya risasi. Usiku, Brian na rafiki zake walitoka kwenda kuanzisha uchokozi na police mara kwa mara waliwafyatulia risasi.

Kisha Brian alikutana na Samsom, Mtakatifu wa Siku za Mwisho, ambaye alimshawishi Brian kuachana na bunduki yake na kubadili maisha yake kabla hajachelewa. Samson alimtambulisha Brian kwa wamisionari, na baada ya miaka miwili ya kukutana nao, Brian aliamua kubatizwa.

Samson baadae alikuwa mzee na msemaji kwa ajili ya Kibera Vision Youth Group, taasisi ambayo ilijitolea kwenye kuwasaidia vijana kupata ujuzi na uzoefu waliohitaji ili kufanikiwa kupitia biashara ndogondogo za ujasiriamali. Brian alikuwa mtunza hazina wa Kibera Vision Youth Group.

Kwa pamoja, Brian na Samson wamefanya kazi kuwasaidia wasichana na wavulana. Kwa kuanza na kazi ya uoshaji magari mnamo 2007 shughuli za kikundi hiki cha vijana za ujasiriamali zilitanuka mpaka kwenye utengenezaji kandambili kutokana na matairi ya magari, uchomeleaji, utengenezaji pikipiki, uchakataji wa plastiki na chuma, uendeshaji wa bodaboda (pikipiki), na ukondakta kwenye matatu (mabasi madogo). Hata walianzisha timu ya mpira wa miguu ya vijana.

Samson na Brian walifundisha Neno la Hekima kwa wasichana na wavulana wa Kibera Vision Youth Group. Baadhi yao walikuwa hapo awali wamedhurika kutokana na vitu viletavyo uraibu, kama wakazi wa eneo, mama wa watoto watano, ambaye alipoteza uoni kutokana na unusaji wa gundi akiwa kijana.

Kwa kufanya kazi na vijana na kuwasaidia kuanzisha bishara za pamoja ili kupata fedha, Samson na Brian waliwasaidia kujifunza kusaidiana.

Picha
Brian Kigundu akiwa na vijana

Washiriki wa Kibera Vision Youth Group, 2021 (picha kwa ruhusa ya Brian Kigundu).

Kazi ya Samson na Brian huko Kibera ilitambuliwa na kiongozi wa eneo na msaidizi wa kamishna wa jimbo. Kwa sababu ya mfano mzuri wa wawili hawa, wamisionari wa Watakatifu wa Siku za Mwisho walikaribishwa na wawakilishi wa serikali ya eneo. Samson alitumikia kwenye kata ya Riruta kama kiongozi wa wamisionari wa kata, na Brian alitumikia kama rais wa Shule ya Jumapili.

“Lengo letu ni kuwabadilisha vijana hawa, na wanafuata hilo vizuri kwa sababu sisi tu sehemu yao, na wanaona badiliko kwenye maisha yetu ,” alisema Samson

Chapisha