Historia ya Kanisa
Uganda: Muhtasari


ramani ya Uganda

Historia ya Kanisa nchini

Uganda

Muhtasari

Ingawa mikutano ya nyumbani ilikuwa ikifanywa na Watakatifu wa Siku za Mwisho waliokuwa wakiishi Uganda mapema mwaka 1969, hakuna uanzishwaji wa kudumu wa Kanisa uliotokea hadi baadaye sana. Kuanzia miaka ya mwishoni mwa 1980, Waganda waliokuwa wakiishi Ulaya na Marekani walijifunza injili ya urejesho, wakaongolewa, na baadaye wakarudi katika nchi yao ya nyumbani wakiwa na ujumbe. Mnamo Februari 1990, kikundi kidogo cha Watakatifu na majirani zao wakaanza kuwa na mikutano ya mara kwa mara. Tawi likaanzishwa huko Kampala mwaka uliofuata.

Muda mfupi baada ya tawi kuanzishwa huko Kampala, wamisionari na waumini wakaanza kushiriki injili na rafiki zao, familia na majirani kote nchini. Ndani ya miaka miwili wilaya zikawa zimeanzishwa huko Kampala na Jinja, na matawi yakawa yanaanzishwa kote nchini. Mwaka 2010 Kigingi cha Kampala Uganda kilianzishwa.

Watakatifu wa Uganda walitafuta fursa ya kujenga jamii imara kwa kutumia kanuni za injili na wametafuta kusaidiana wao kwa wao kujifunza injili na kwa bidii kutenda kazi katika miito waliyoipokea (ona Mafundisho na Maagano 107:99–100). Wameshiriki katika miradi ya kutoa huduma ya kusafisha na kujenga jumuiya zao. Hii imejumuisha fikra za ubunifu. Mbio za miguu na madereva maalumu vimepangwa ili kuhimiza michango kwa ajili ya wale walio katika shida. Miradi ya kijamii imesafisha na kupaka rangi maeneo ya umma, na madarasa maalumu yaliyolenga mahitaji ya makundi maalumu yamejengwa.