Ujumbe Wa Urais wa Kwanza, Aprili 2010
Kazi Kuu ya Mungu
Apili 6, 1830
Miaka mia na themanini iliyopita, Joseph Smith, Oliver Cowdery, na wengine wachache walikusanyika pamoja ili kupanga Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kwa maelezo yote ilikuwa ni mkutano wa kawaida lakini wa kiroho. Joseph anaandika kwamba baada ya sakramenti, “Roho Mtakatifu alimwagwa juu yetu kiasi kwamba—wengine walitoa unabii, wakati sisi sote tulipomsifu Bwana, na kusherekea sana.”1
Matukio ya siku hii yalipita bila kujulikana na ulimwengu; hayakuambatana na vichwa vya habari au mbiu. Hata hivyo, jinsi gani mbingu lazima zilifurahia na kutukuza Mungu—kwamba siku hiyo, Kanisa la Yesu Kristo lilirudi duniani!
Solomon Chamberlain
Tangu siku hiyo hadi leo, mamillioni ya wana na mabinti wa Baba wa Mbinguni waliojawa na imani wamefuata ushawishi wa Roho Mtakatifu na kuingia katika maji matakatifu ya ubatizo. Mtu mmojapo alikuwa Solomon Chamberlain.
Solomon alikuwa mtu wa kiroho na alitumia masaa mengi katika maombi, akitafuta ondoleo la dhambi zake na kumsihi Baba kumwelekeza kwa ukweli. Wakati mwingine karibu 1816, Solomon aliahidiwa katika ono kwamba ataishi ili kuona siku Kanisa la Kristo litakapopangwa baada ya muundo wa kiutume ulipoundwa tena duniani.
Miaka baadaye Solomon alikuwa anasafiri kwa mashua kuelekea Canada wakati chombo chake kiliposimama katika mji mdogo wa Palmyra, New York. Hapo alihisi nguvu za ushawishi zikimhimiza kushuka. Bila kujua kwa nini alikuwa pale, alianza kuongea na watu wa mji. Haipita muda mferu kabla asikie maongezi ya “biblia ya dhahabu.” Alisema maneno hayo mawili yalituma “nguvu kama umeme[ambayo] ilienda kutoka juu ya kichwa changu hadi mwisho wa vidole vya miguu yangu.”
Maulizo yake yalimwelekeza kwa nyumba ya Smith, ambako aliongea na waliokuwemo kuhusu habari ya ajabu ya injili ya urejesho. Baada ya kukaa pale siku mbili na kupokea ushuhuda wa ukweli, Solomon aliendelea na safari yake kuelekea Canada, akienda na kurasa 64 mpya zilizochapishwa,za Kitabu cha Mormoni zilizokuwa hazikufunganishwa. Kila mahali alikoenda, alifundisha watu, “wote mashuhuri na duni, tajiri na masikini, … ili kujitayarisha kwa kazi kuu ya Mungu ambayo ilikuwa sasa inakaribia kutokezea.”2
Kazi Kuu ya Mungu
Tangu siku hiyo wa Aprili 1830, mamillioni wamegundua ukweli wa injili ya urejesho na wameingia katika maji ya ubatizo. Nashuhudia kwamba hii “kazi kuu ya Mungu” imo duniani leo. Nashuhudia kwamba Bwana anatazama Kanisa Lake na kuliongoza kupitia kwa Nabii Wake, Rais Thomas S. Monson. Sio baraka ya kawaida kuishi katika siku hizi za mwisho. Hizi ni nyakati tukufu, zilizotabiriwa na manabii wa zamani na kutunzwa ni jeshi la malaika angalifu. Bwana anajali Kanisa Lake. Yeye pia anajali wale ambao, kama Solomon Chamberlain,hufuata ushawishi wa Roho Mtakatifu na kuungana na ndugu na dada zao ulimwenguni kwote katika kusaidia ili kuwezesha kazi hii kuu ya Mungu.
© 2009 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/09. Tafsiri iliidhinishwa: 6/09. Tafsiri ya First Presidency Message, April 2010. Swahili. 09364 743