Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Novemba 2010
Karama ya Kiungu ya Shukrani
Moyo wa shukrani … huja kwa kuwasilisha shukrani kwa Baba wetu wa Mbinguni kwa ajili ya baraka zake na kwa ajili ya wale walio karibu nasi kwa yale yote wanayoleta maishani mwetu.
Hiki kimekuwa kikao cha ajabu. Nilipoteuliwa kuwa Rais wa Kanisa, nilisema, “nitajichukulia jukumu moja’. Nitakuwa mshauri wa Kwaya ya Hema.” Najuvunia kwaya yangu!
Mama yangu alisema wakati mmoja kunihusu, “Tommy, najivunia sana yale yote ambayo umefanya’ Lakini nina la kusema kwako. Ungebaki tu kwenye kinanda.”
Kwa hivyo nikaenda kwenye kinanda na kumchezea wimbo moja: “Here we go, [here we go] to a birthday party.”1 Kisha nikampa busu, naye akanikumbatia.
Ninamuwaza Ninawaza kuhusu Baba yangu. Ninawaza kuhusu viongozi wote wenye mamlaka walioniathiri na wengine, pamoja na wajane niliowatembelea, wote 85, na kuku wa tanuru, wakati mwingine na pesa kidogo kwa matumizi yao.
Nilimtembelea mmoja usiku mmoja Ilikuwa usiku wa manane, nilienda kwenye kao la uuguzi, na mpokezi akaniambia, “nina hakika bado amelala, lakini aliniambia nihakikishe nimemwamsha, kwani alisema, ‘Ninajua atakuja.’”
Nikashika mkono wake, naye akaniita Alikwa macho. Akashikilia mkono wangu kwenye midomo yake na kusema, “Nilijua ungekuja.” Ningewezaje kukosa kuja?
Muziki mtamu hunigusa hivyo.
Kina ndugu na dada wapendwa, tumesikia ujumbe wenye ari ya kweli, tumaini na upendo. Mawazo yetu yamegeuzwa kwake Yeye aliyepatanisha kwa ajili ya dhambi zetu, aliyetuonyesha jinsi ya kuishi na kuomba, na ambaye alidhihirisha kwa matendo yake baraka za huduma.
Katika kitabu cha Luka Sura ya 17, tunasoma kumhusu:
“Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipitia katikati ya Samaria na Galilaya.
“Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali.
“Wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu.
“Alipowaona aliwaambia Enendeni, makajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
“Na moja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;
“Akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
“Yesu akajibu akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?
“Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?
“Akamwambia, Inuka enenda zako, imani yako imekuokoa.”2
Kupitia kwa upatanishi mtakatifu, wale waliokuwa wenye ukoma waliepushwa kutokana na kifo cha ukatili cha mateso na kupatiwa maisha mapya. Maonyesho ya shukrani ya mmoja aliyefaa baraka za Bwana, kutokuwa na shukrani kulikoonyesha na wale tisa hakukumfurahisha Yeye.
Ndugu na dada zangu, Je! Tunakumbuka kutoa shukrani kwa baraka tunazopokea? Kutoa shukrani kwa kweli hakutusaidii tu kugundua baraka zetu, bali pia kunafungua milango ya mbinguni na kutusaidia kuhisi upendo wa Mungu.
Rafiki yangu mpendwa Rais Gordon B. Hinckley alisema, “Unapotembea kwa shukrani, hautembei kwa ujeuri na kujiona na majisifu; unatembea kwa roho wa shukrani ambavyo ni vyema kwako na vya kubariki maisha yenu.”3
Katika kitabu cha Mathayo katika Biblia tunapata taarifa nyingine ya shukrani, wakati huu ni maonyesho kutoka kwa Mwokozi. Alipokuwa akitembea nyikani kwa siku tatu, zaidi ya watu 4,000 walimfuata na kusafiri pamoja Naye. Alionyesha huruma kwao, kwani walikuwa hawajala kwa siku tatu. Wafuasi Wake, hata hivyo, waliuliza, “Tupate wapi mikate mingi nyikani hata kusibisha mkutano mkuu namna hii?” Kama vile wengi wetu, wafuasi waliona tu kulichokosekana.
“Yesu akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema [wanafunzi], Saba na visamaki vichache.
“[Yesu] Akawaagiza mkutano kuketi chini;
“Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, na akashukuru, na akavimega na akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.”
Tazama kwamba Mwokozi alishukuru kwa kile walichokuwa nacho na muujiza ukafuata. “Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.”4
Sote tumepata uzoefu wakati kuangazia kwetu ni juu ya kile ambacho hatuna, badala ya baraka zetu. Mwanafalsafa Mgiriki Epictetus alisema, “Alikuwa mtu mwenye hekima ambaye hahuzunishwi na vitu ambavyo hana, bali husherekea vile alivyonavyo.”5
Shukrani ni kanuni takatifu. Bwana ametamka, kupitia ufunuo uliotolewa kwa Nabii Joseph Smith:
“Nawe utamshukuru Bwana Mungu wako katika mambo yote. …
“Na katika lolote mwanadamu hamkosei Mungu, au ghadhabu ya Mungu haiwaki kwa yeyote, isipokuwa wale tu wasiokiri mkono Wake katika mambo yote.”6
Katika Kitabu cha Mormoni tunaambiwa “muishi katika kushukuru kila siku, kwa rehema nyingi na baraka ambazo anaweka kwenu.”7
Licha ya hali zetu, kila mmoja wetu ana mengi ya kuwa na shukrani kama tu tutatua na kutafakari kuhusu baraka zetu.
Huu ni wakati maridhawa kuwa ulimwenguni. Ingawa kuna mengi yaliyo na makosa katika ulimwengu siku hizi, kuna mambo mengi ambayo ni sahihi na mema. Kuna ndoa ambazo zinafanikwa, wazazi ambao wanawapenda watoto wao na wanajitolea kwa sababu yao, marafiki ambao wanajali masilahi yetu na wanatusaidia, waalimu ambao wanafunza. Maisha yetu yamebarikiwa katika njia zisizohesabika.
Tunaweza kujiinua wenyewe, na wale wengine pia, tunapokataa kukaa chini ya utawala wa mawazo duni na kupalilia ndani ya moyo wetu mtazamo wa shukrani. Kama kukosa shukrani kunaweza kuorodheshwa katika dhambi kuu, basi kuwa na shukrani kunachukua nafasi yake katika maadili mema zaidi. Mtu mmoja alisema kwamba shukrani sio tu maadili makuu bali mzazi wa yale mengine.8
Je! Tunawezaje kukuza ndani ya moyo wetu mtazamo wa shukrani? Rais Joseph F. Smith, Rais wa sita wa Kanisa, alitoa jibu. Alisema: “Mtu wenye shukrani huona mengi sana katika dunia ya kushukuru, na kwake mema yanashinda uovu. Upendo unashinda wivu, na nuru huiondosha giza kutoka kwenye maisha yake.” Aliendelea, “Kiburi huangamiza shukrani zetu na kuweka ubinafsi badala yake. Tunakuwa na fuhara jinsi gani kuwa katika mbele za nafsi yenye shukrani na upendo, na tunatakiwa kuwa makini kupalilia kupitia kwa tabia ya maisha ya maombi, mtazamo wa shukrani kwa Mungu na binadamu!”9
Rais Smith anatuambia kwamba maisha ya maombi ni funguo za kupata shukrani.
Je! Kupata vitu kunatufanya kuwa na furaha na shukrani? Labda kwa muda mchache. Hata hivyo, vitu vile vinavyoleta furaha ya kina na ya kudumu na shukrani ni vitu ambavyo fedha haziwezi kununua: familia zetu, injili, marafiki wema, afya yetu, uwezo wetu, upendo tunaopokea kutoka kwa wale walio karibu nasi. Ya kusikitisha, hivi ndivyo kati ya vitu ambavyo tunakubali kutovitilia maanani.
Mtunzi Mwingereza Aldous Huxley aliandika, “Binadamu wengi wana karibu uwezo mwingi wa kutotilia vitu maanani.”10
Mara nyingi hatuwatilii maanani wale watu ambao wanafaa shukrani zetu. Tusingojee mpaka tuchelewe kuonyesha hizo shukrani. Akiongea kuhusu wapendwa wake aliokuwa amewapoteza, mwanamke mmoja alisema majuto yake kwa njia hii: “Nakumbuka siku hizo za furaha na kila mara natamani kuongea katika masikio ya wafu hao shukrani ambazo ningewapatia walipokuwa hai na hawakuzipata.”11
Kupoteza wapendwa wetu bila shaka huleta majuto fulani katika mioyo yetu. Acha tupunguze hisia kama hizo jinsi tunavyoweza kibinadamu kwa kuonyesha upendo wetu kila mara na shukrani zetu kwao. Hatujui ni lini itakuwa imechelewa.
Moyo wenye shukrani, basi, huja kupitia kuonyesha shukrani kwa Baba yetu wa Mbinguni kwa baraka zako na kwa wale walio karibu nawe kwa yale walioleta katika maisha yetu. Hii inahitaji jitihada za makusudi-hata mpaka tumejifunza kikweli na kukuza mtazamo wa shukrani. Mara nyingi tunasikia shukrani na tunataka kuonyesha shukrani zetu lakini tunasahau kufanya hivyo au hatupati nafasi ya kufanya hivyo. Mtu mmoja alisema kwamba kuhisi shukrani na kutoonyesha ni kama kufunga zawadi na hatuipeani.12
Tunapokumbana na changamoto na shida katika maisha yetu, ni vigumu kwetu kuangazia baraka zetu. Hata hivyo, ikiwa tutachunguza sana na kutazama sana zaidi, tutaweza kuhisi na kutambua ni kiasi gani ambacho tumepatiwa.
Nashirikisha taarifa kuhusu familia moja ambayo iliweza kupata baraka katikati ya changamoto kuu. Hii taarifa niliisoma miaka mingi iliyopita na nikaiweka kwa sababu ya ujumbe wake. Imeandikwa na Gordon Green na ilitokea kwenye gazeti la Kiamerika zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Gordon anaelezea jinsi alivyokua katika shamba huko Kanada, ambako yeye na ndugu zake walikuwa wanahitajika kuharikisha kwenda nyumbani kutoka shule hali watoto wengine walikuwa wanabakia wakicheza mpira na kuogelea. Baba, hata hivyo, alikuwa na uwezo wa kuwasaidia wao kufahamu kwamba kazi yao ilikuwa na thamani fulani. Hii ilikuwa ni kweli hasa baada ya mavuno, wakati familia ilikuwa inasherehekea Siku ya Kushukuru, kwani siku hiyo baba yao aliwapa zawadi. Alikadiria kila kitu walichonacho.
Usubuhi ya Siku ya Kushukuru, aliwachukua hadi kwenye ghala la chini likiwa na mapipa ya tufaha, mikebe ya viazisukari, karoti zilizowekwa kwenye changarawe, na milima ya magunia ya viazi, pamoja na njerege, nafaka, maharagwe, jeli, stroberi na vingine vilivyohifadhiwa vilivyojaa kwenye rafu zao. Aliwauliza watoto wahesabu kila kitu kwa makini. Kisha wakatoka nje ya ghala na kupata ni tani ngapi za nyasi walizokuwa nazo na walikuwa na vipimo vingapi vya nafaka katika ghala. Walihesabu ng’ombe, nguruwe, kuku, batamzinga, na bata bukini. Baba yao alisema alikuwa anataka kuona wamekuwa na kiasi gani, lakini walifahamu vyema aliwataka wajue, katika siku hiyo ya karamu, jinsi Mungu alivyowabariki sana na kufurahia masaa yao mengi ya kazi. Mishowe, walipokaa chini kwenye karamu iliyoandaliwa na mama yao, baraka ni kitu ambacho walikuwa wamehisi.
Gordon alisema, hata hivyo, kwamba Siku ya Kushukuru ambayo anakumbuka sana ni ile ya mwaka ambao walionekana hawakuwa na chohote cha kushukuru.
Mwaka huo ulianza vyema: walikuwa masazo ya nyasi, mbegu nyingi, vitoto vinne vya nguruwe; na baba yao alikuwa ametenga fedha kidogo ili kwamba siku moja waweze kununua mashine ya kubeba nyasi—mashine nzuri sana ambayo wakulima wengi walitamani kuwa nayo. Pia ulikuwa mwaka ambao umeme ulikuja kwenye mji wao-ingawaje sio kwao, kwa sababu hawakuweza kuugharamia.
Usiku mmoja mamake Gordon alikuwa anaosha nguo nyingi, baba yake alichukua nafasi na kuchukua zamu yake kwenye bao la kuoshea na kumwambia mkwewe apumzike na kufuma fulana. Alisema, “Unatumia wakati mwingi kuosha nguo kuliko kulala. Je! Unafikiria tunafaa kuachilia na tupate umeme?” Inagawaje alivutiwa na hayo, alimwaga chozi au mawili alipofikiria mashine ya nyasi ambayo haingenunuliwa.
Laini ya umeme ilipita kwenye barabara yao mwaka huo. Inagawaje halikuwa jambo la ajabu, walinunua mashine ya kuosha ambayo ilifanya kazi siku nzima peke yake na mataa ya mg’aro yakining’inia kwenye kila dari. Hapakuwa mataa sasa ya kujaza mafuta, hamna tambi za kukata, hamna chemli cha kusafisha. Mataa yaliendelea polepole darini.
Kuja kwa umeme kwenye shamba lao kilikuwa kitu cha mwisho kizuri kutokea kwao mwaka huo. Mara, mimea ilipoanza kuchomoza kutoka mchangani, mvua ikaanza. Maji yalipokwisha pungua, hapakuwa na mmea uliobakia popote. Wakapanda tena, lakini mvua zaidi ikaponda mimea katika mchanga. Viazi vikaoza kwenye matope. Wakauza ng’ombe kadha na nguruwe wote, pamoja na wale wanyama wengine ambao walikuwa wanataka kufuga, wakipata bei za chini sana kwa sababu kila mtu alikuwa anafanya vivyo hivyo. Kile walichovuna mwaka huo ilikuwa ni kijisehemu kidogo cha tanipu ambazo zilinusurika hiyo dhoruba.
Kisha ikafika Siku ya Kushukuru tena. Mama yao akasema, “Labda tusahau ya mwaka huu. Hatuna hata bata bukini aliyebakia.”
Asubuhi ya Siku ya Kushukuru, hata hivyo, babake Gordon alitokeza akiwa na sungura na akamwambia mkewe ampike. Akinung’ununika alianza matayarisho, akisema kwamba itachukua muda mrefu kumpika huu manyama mzee. Alipowekwa mezani pamoja tanipu zilizokuwa zimeponea, watoto walikataa kula. Mamake Gordon akalia, na kisha babake akafanya kitu kigeni. Akaenda darini, na kuchukua taa ya mafuta, akaichukua mpaka mezani na kuiwasha. Akawambia watoto wazime taa ya umeme. Wakati walipokuwa na hiyo pekee, hawangeweza kuamini kwamba kulikuwa na giza hapo awali. Walishangaa jinsi walivyokuwa wanaona chochote bila mataa ya mg’ao wa umeme.
Chakula kilibarikiwa, na kila mmoja akala. Chakula kilipokwisha malizika, walikaa kimya. Gordon aliandika,
“Ni kwa mfifio wa mwanga duni wa taa ya zamani tuliweza kuona vyema tena. …
“Ulikuwa mlo mtamu. Sungura alionja kama bata mzinga, na tanipu zilikuwa laini kati ya zile tunazoweza kukumbuka… …
“Nyumba yetu, hata na upungufu wote, ilikuwa na utajiri mkuu kwetu.”13
Ndugu na dada, kuonyesha shukrani ni hisani na heshima; kutenda kwa shukrani ni ukunjufu na uadilifu; lakini kuishi kwa shukrani kila mara mioyoni yetu ni kugusa mbinguni.
Ninapotimitisha asubuhi hii, ni maombi yangu kwamba katika zaida ya kila kitu chote tunachoshukuru juu yake, na tuweze kulenga shukrani zetu kwa Bwana wetu na Mwokozi, Yesu Kristo. Injili yake tukufu anayopeana majibu ya maswali makubwa ya maisha: Je! Tulitoka wapi? Je! Kwa nini tuko hapa? Je! Roho zetu zitaenda wapi tukifariki? Kwamba injili huwaletea wale wanaoishi gizani nuru ya ukweli mtukufu.
Alitufunza jinsi ya kuomba. Alitufunza jinsi ya kuishi. Alitufunza jinsi ya kufa. Maisha yake ni urithi wa upendo. Wagonjwa aliwaponya; waliogandamizwa aliwainua; mwenye dhambi alimwokoa.
Mwishowe, alisimama peke yake. Wengine wa Mitume walimtilia hofu; mmoja akamsaliti. Askari wa Kirumi wakamchoma ubavuni. Umati wenye ghadhabu ukatwaa uhai Wake. Bado kuna mlio kutoka mlima Goligotha maneno Yake ya faraja, “Baba, uwasamehe; kwa kuwa hawajui watendalo.”14
Je! Ni nani huyu Mtu wa simanzi, aliyezoeana na huzuni?15 Je! Ni nani Mfalme wa utukufu, huyu Bwana wa mabwana?16 Yeye ni Bwana wetu. Yeye ni Mwokozi wetu. Yeye ni Mwana wa Mungu. Yeye ni mtunzi wa wokovu wetu. Anatuita, “Njooni Kwangu.”17 Anaagiza, “Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.”18 Anasihi, “Mtazishika amri zangu.”19
Acheni tumfuate Yeye. Acheni tuige mfano Wake. Acheni tutii neno Lake. Kwa kufanya hivyo, tutatoa Kwake kipawa kitakatifu cha shukrani.
Ombi langu la dhati, la moyoni ni kwamba tuweze, katika maisha yetu wenyewe, ya kuonyesha maadili ya ajabu ya shukrani. Na isambae katika nafsi zetu wenyewe, sasa na milele. Katika jina Yesu Kristo, amina.
© 2010 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/09. Tafsiri iliidhinishwa: 6/09. Tafsiri ya First Presidency Message, November 2010. Swahili. 09371 743