Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Februari 2011
Itakuwa Shangwe Kubwa Namna Gani
Shangwe chache maishani ni tamu na ndefu kuliko kujua kwamba umewasaidia wengine kwa kupeleka injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo katika mioyo yao. Kuwa na shangwe hiyo ni fursa ya kila mshiriki wa Kanisa. Tulipobatizwa, tulifanya ahadi ya kuwa “[tu]ngesimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote, na katika vitu vyote na katika mahali popote [tu]lipo, hata hadi kifo ili [tu]weze kukombolewa na Mungu, na kuhesabiwa pamoja na wale wa ufufuko wa kwanza, ili [tu]pokee uzima wa milele” (Mosia 18:9).
Washiriki wote wanakubali sehemu ya jukumu lililopewa Kanisa la kupeleka injili ya Yesu Kristo kwa ulimwengu, popote pale na ilimradi wanaishi. Bwana amesema bayana: “Tazama nimewatuma ninyi kwenda kushuhudia na kuwaonya watu, na ni wajibu wa kila mtu ambaye ameonywa amwonye jirani yake” (M&M 88:81). Wamisionari watakuwa na uwezo wa kuwafundisha wale ambao bado si washiriki wa kanisa. Washiriki wa Kanisa wana uwezo wa kuwatafuta wale ambao Bwana amewatayarisha ili wamisionari wawafundishe.
Tunafaa kutumia imani kwamba Bwana amewatayarisha watu walio karibu nasi ili kufundishwa. Anafahamu wao ni akina nani, na anaweza kutuongoza kwao kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kutupa maneno ya kuwaalika ili wafundishwe. Ahadi ambayo Bwana alimpa mmisionari mmoja katika 1832 pia ni ahadi anayotupa katika jukumu letu la kutafuta watu walio tayari kufundushwa na wamisionari. “Nami nitamleta Mfariji, atakaye mfundisha ukweli na kumwonyesha njia ya kwenda, na kadiri atakavyokuwa mwaminifu, nitamtuza tena miganda” (M&M 79:2–3).
Na ahadi ya shangwe kuu kwa mmisionari mwaminifu ni yetu pia kama washiriki waaminifu ambao hutoa mioyo yao kwa kazi ya umisionari:
“Na sasa, ikiwa shangwe yako itakuwa kubwa kwa nafsi moja ambayo umeileta Kwangu katika ufalme wa Baba Yangu, itakuwa shangwe kubwa namna gani kwako kama utazileta nafsi nyingi kwangu!
“Tazama, unayo injili yangu mbele yako, na mwamba wangu, na wakovu wangu.
“Mwombe Baba katika jina langu, katika imani, ukiamini kwamba utapokea na utapata Roho Mtakatifu, ambaye hudhihirisha mambo yote yaliyo muhimu kwa wanadamu” (M&M 18:16–18).
Zaidi ya Roho Mtakatifu kutusaidia kufahamu na kuwaalika walio tayari kufundishwa, Bwana amewaita na kuwafundisha viongozi ili watuongoze. Katika barua iliyoandikwa mnamo 28, 2002, Urais wa Kwanza umeweka wajibu zaidi wa kazi ya umisionari kwa maaskofu na kata.1 Kwa usaidizi wa baraza la tawi au kata, kamati kuu ya ukuhani hutayarisha mpango wa kazi ya umisionari kwa kitengo. Katika mpango huo, kuna maoni ya jinsi washiriki wanaweza kuwapata wale waliotayari kufundishwa na wamisionari Kuna mtu aliyeitwa kama kiongozi wa misheni katika kata au tawi. Kiongozi huyo wa misheni anawasiliana kwa karibu na wamisionari na wachunguzi wao.
Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutimiza wajibu wako wa kibinafsi wa kutafuta watu kwa wamisionari kuwafundisha. Njia rahisi zaidi ndiyo bora zaidi
Omba ili Kuongozwa na Roho Mtakatifu Zungumza na viongozi wa mahali pako na wamisionari ukiwauliza maoni yao na kuwaahidi usaidizi wako. Watie moyo wale ambao wanahusika nawe katika kazi hii. Na kuwa shahidi wakati wote katika yale unayosema na kutenda kwamba Yesu ndiye Kristo na kwamba Mungu hujibu maombi
Nashuhudia kuwa Roho Mtakatifu atakuongoza kwa wale wanaotafuta ukweli unapoomba na kufanya bidii kwa ajili ya uongozi huo. Na ninajua kutoka kwa uzoefu kwamba shangwe yako itadumu pamoja na wale wanaochagua kupeleka injili katika mioyo yao na kisha kuvumilia kwa imani.