Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Juni 2011
Kundi la Wanawake Watakatifu
Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.
Eliza R. Snow, rais mkuu wa pili wa Muungano wa Usaidizi wa Kina mama: “Paulo Mtume wa kale aliongea kuhusu wanawake wa kale. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuwa wanamke mtakatifu. Tutakuwa na mrengo wa juu, kama tu wanawake watakatifu. Tutahisi kwamba tumeitwa kutenda majukumu muhimu. Hakuna aliye samehewa kutoka kwayo. Hakuna dada aliyetengwa, na nafasi yake duni sana bali kile anachoweza kufanya ni kikuu katika kuendeleza Ufalme wa Mungu juu ya dunia.”1
Kina dada, hatujatengwa wala nafasi yetu si duni. Kwa kukubali kipawa cha shughuli katika Muungano wa Usaidizi wa kina dada, tunakuwa sehemu ya kile Nabii Joseph alichoeleza kama kikundi “kilichotengwa kutokana kwa uovu wa ulimwengu—bora, wema, na utakatifu.”2
Hili kundi linatusaidia kuimarisha imani yetu na kukua kiroho kwa kutupatia uongozi, huduma, na nafasi za kufunza. Katika huduma yetu kadiri mpya imeongezewa katika maisha yetu. Tunaendelea kiroho, na hisia ya kustahili, utambulisho, na heshima huongezeka. Tunafahamu kwamba lengo kamili la mpango wa injili ni kutoa nafasi kwetu ya kufikia uwezo wetu wote.
Muungano wa Usaidizi wa kina mama hutusaidia kupokea baraka za hekalu, kuheshimu maagano tunayofanya, na kujishughulisha na kazi ya Sayuni. Muungano wa Usaidizi wa kina mama huongeza imani yetu na wema wa kibinafsi, kuimarisha familia, na kutafuta na kuwasaidia wale walio na mahitaji.
Kazi ya Muungano wa Usaidizi wa kina mama ni takatifu, na kufanya kazi takatifu hufanyiza utakatifu ndani yetu.
Silvia H. Allred, mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama.
Kutoka kwa Maandiko
Kutoka 19:5; Zaburi 24:3–4; 1 Wathesalonike 4:7; Tito 2:3–4; M&M 38:24; 46:33; 82:14; 87:8; Musa 7:18
Kutoka kwa Historia Yetu
Akiongea kwa Muungano wa Usaidizi wa kina mama wa Nauvoo, Nabii Joseph alisisitiza utakatifu, akieleza kwamba jinsi kina dada wanavyo kuwa halisi na watakatifu, watakuwa na ushawishi mkuu juu ya ulimwengu. Alieleza: “Unyenyekevu, upendo, uasili—haya ndiyo mambo ambayo yanaweza kukupanua. … Kikundi hiki … kitakuwa na nguvu za kuwaamuru malkia miongoni mwao. … Wafalme na malkia wa dunia hii watakuja Sayuni, na kutoa heshima zao.” Kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa kina mama wanaoishi maagano yao wanapewa heshima sio tu na watu wangwana, lakini “kama mtaishi kulingana na haki zenu,” Joseph aliahidi kina dada, “malaika hawawezi kuzuiwa kuwa wenzi wao.”3
Jinsi kina dada wanavyoshiriki katika kazi ya kuhudumu na kuwaokoa wengine, wanatakaswa kibinafsi. Lucy Mack Smith, mamake Nabii, alishirikisha kile ambacho Muungano mzuri wa Usaidizi wa kina mama unaweza kutimiza: “Ni lazima tutunzane mmoja kwa mwengine, tuchungane, tufarijiane na kupokea maelekezo, kwa tuweze kukaa chini sote mbinguni pamoja.”4
© 2011 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/10. Tafsiri iliidhinishwa: 6/10. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, June 2011. Swahili. 09766 743