Vijana
Kuongozwa na Nabii Aishie
Nilipokuwa wa umri wa miaka 16, nilipata fursa ya kuhudhuria mkutano mkuu kwa mara ya kwanza. Familia yangu ilikuwa inaishi magharibi mwa Oregon, Marekani, na tulisafiri kwa gari hadi Utah ili kuhudhuria mkutano mkuu na kumpeleka kaka mkubwa kwenye kituo cha mafunzo cha mamisionari.
Mimi nilienda kwenye mkutano mkuu nikiwa na hamu ya kufunzwa na Roho Mtakatifu. Matokeo yake, nilipokea maonyesho kutoka kwa Roho ambayo labda singepokea kama sikuwa nimejitayarisha mwenyewe.
Katika majowapo wa vikao hivi, kila mtu alisimama na kuimba wimbo wa kusanyiko, “Tuongoze, Ewe Yehova Mkuu.” Tupokuwa tukiimba, nilipata onyesho wazi kwamba nitazame kote katika Kituo cha Mkutano Mkuu. Nilifanya hivyo na nikavutiwa na nguvu za umoja wa maelfu ya watu hapo jinsi sote tulivyopaza sauti zetu katika sifa kwa Mungu.
Kisha nikapata uzoefu ambapo nilihisi kama Nefi wakati alipoona ono la mti wa uzima, kwani Roho aliniambia, “Tazama” (ona 1 Nefi 11–14). Nilimtazama Rais Thomas S. Monson na nikahisi kwamba umoja wa Kanisa ulikuwepo kwa sababu tunaongozwa na nabii aishie. Kupitia ushuhuda wa Roho Mtakatifu, mimi najua Rais Monson ni nabii wa kweli wa siku zetu, na najua kwamba Yesu Kristo anaongoza Kanisa hili kupitia kwake.