2012
Kasi ya Maisha
Mei 2012


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Mei 2012

Mbio za Maisha

Picha
Rais Thomas S. Monson

Sisi tulitoka wapi? Kwa nini tuko hapa? Tutaenda wapi baada ya maisha haya? Haya maswali ya kawaida hayafai kubaki bila kujibiwa.

Ndugu na dada zangu wapendwa, asubuhi hii ningependa kuwambia ninyi kweli za milele—hizo kweli ambazo zinaimarisha maisha yetu na kutupeleka nyumbani salama.

Kila mahali, watu wako mbioni. Ndege za jeti zinaharikisha mizigo yake ya binadamu ya thamani kuvuka bara pana na bahari kuu ili kwamba mikutano ya biashara iweze kufanyika, majukumu yatendeke, likizo zifanyike, na familia kutembelewa. Barabara kila mahali—ikijumuisha baraste, baraste kuu—hupitia mamilioni ya magari, yanayobeba mamilioni zaidi ya watu, katika mfulululizo unaonekana kutokwisha na kwa sababu nyingi sana tunapuruka katika shughuli kila siku.

Katika mwendo huu wa harakaharaka wa maisha je! Tunatua na kwa muda kutaamali—hata mawazo ya kweli za milele?

Tunapolinganisha kweli za milele, maswali mengi ya maisha na mambo ya kila siku kwa kweli ni ya maana kidogo sana. “Ni nini tutakula njioni? Ni rangi gani tutapaka sebuleni? Je! Tumsajili Johnny kwa kandanda?” Maswali haya na mengine mengi kama haya hufifia katika umuhimu wake wakati matatizo yanapoibuka, wakati wapendwa wetu wanapoumia au kujeruhiwa, wakati ugonjwa unapoingia katika nyumba yenye afya, wakati mshumaa wa maisha unapofifia na giza linapotishia. Mawazo yetu yanachongwa, na kwa urahisi tunaweza kutambua kile kilicho cha muhimu hasa na kilicho duni tu.

Majuzi nilimtembelea mwanamke ambaye alikuwa anapigana na ugonjwa unaotishia uzima kwa miaka miwili. Alisema kwamba kabla ya ugonjwa wake, siku zake zilijawa na shughuli kama vile kusafisha nyumba mpaka ikwatuke na kuijaza na fanicha na vyombo vya urembo. Alikwenda kwa mtengeneza nywele wake mara mbili kila wiki na kutumia fedha na muda kila wiki kuongeza mavazi yake. Wajukuu walikuwa wanaalikwa kwa uadimifu sana, kwani alikuwa na hofu kwamba kile alichofikiria kuwa mali yake ya thamani ingeweza kuvunjwa au kuharibiwa na mikono midogo isiyo na uangalifu.

Na halafu akapokea habari za kustusha kwamba maisha yake yakuwa hatarini na kwamba angekuwa na maisha mafupi sana yaliyobakia. Yeye alisema kwamba wakati aliposikia utambuzi wa daktari, na alijua mara moja kwamba atatumia muda wowote uliobakia na familia yake na marafiki zake na akiwa na injili kama kitovu cha maisha yake, kwani haya yaliwakilisha kile kilichokuwa cha thamani kwake.

Nyakati kama hizi banaya zinakuja kwetu sote katika wakati mmoja au mwingine, ingawa labda sio kila mara kupitia hali za kusisimua. Tunaona wazi kile ambacho kina maana katika maisha yetu na jinsi tunafaa kuishi.

Mwokozi alisema:“

Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;

“Bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

“Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”1

Katika nyakati zetu za tafakari ya kina au mahitaji makuu, nafsi ya mtu uelekea mbinguni,kutafuta majibu matakatifu kwa maswali yao makuu: Je! Tulitoka wapi? Kwa nini tuko hapa? Tutaenda wapi baada ya kuacha maisha haya?

Majibu ya maswali haya hayawezi kupatikana ndani ya vitabu vya usomi, kwa kutafuta katika Intaneti. Haya maswali yanashinda maisha ya muda. Yanakumbatia umilele.

Je! Tulitoka wapi? Hii swali haliepukiki kufikiriwa, kama alisemwi, na kila mwanadamu.

Mtume Paulo aliwaambia Wathene katika Kilima Mars kwamba “sisi tu wazao wa Mungu.”2 Kwa vile tunajua kwamba miili yetu ni uzao wa wazazi wetu wa kimwili, lazima tuchuguze maana ya maneno ya Paulo. Bwana alitangaza kwamba “Na roho na mwili ndiyo nafsi ya mwanadamu.”3 Na hivyo ndivyo ilivyo roho uzao wa Mungu. Mwandishi wa Waebrania umuita Yeye “Baba wa roho.”4 Roho za wanadamu wote kihalisi “wana na mabinti” Wake.5

Tunatambua kwamba watunzi wa mashahiri wameandika, kujifunza juu ya hili jambo, wakiandika jumbe za kuvutia na kuandika mawazo ya ajabu. William Wordsworth aliandika kweli hii:

Kuzaliwa kwetu ni kama kulala na kusahau;

Nafsi huamuka nasi, Nyota ya maisha yetu,

Ilikuwa sehemu ingine pa kuhisi

Na inatoka mbali,

Sio katika usahaulivu,

Na sio kwa uchi kabisa,

Bali twaja tufuatia mawingu ya utukufu

Kutoka kwa Mungu, ambaye ndiye nyumba yetu

Mbinguni ipo karibu nasi uchangani!6

Wazazi utafakari majukumu yao ya kufunza, kuwavutia, na kuwapatia mwongozo, maelekezo na mfano. Na wazazi wakitafakari, watoto—na hasa vijana—wanauliza ili swali la muhimu. kwa nini tuko hapa? Kwa kawaida, linasemwa kimya nafsini na kwa njia ingine, kwa nini mimi niko hapa?

Tunafaa kuwa na shukrani jinsi gani kwamba Muumba mwenye hekima aliumba ulimwengu na kutuweka hapa tukiwa na pazia ya kusahau kuwepo kwetu kwa mapema ili tuweza kupata uzoefu wa wakati wa kujaribiwa, nafasi ya kujithibitisha wenyewe, kwamba ili tuhitimu kwa yote ambayo Mungu ametutayarishia sisi kupokea.

Ni wazi, madhumuni muhimu ya kuwepo kwetu juu ya ulimwengu ni kupokea mwili wa nyama na mifupa. Sisi pia tumepatiwa kipawa cha wakala. Kwa njia elfu, tuna nafasi za kuchagua wenyewe. Hapa tunajifunza kutoka kwa mchapakazi hodari wa uzoefu. Tunatambua kati ya wema na uovu. Tunatofutisha chungu na tamu. Tunagundua kuna matunda yanayoambatana na matendo yetu.

Kwa kutii amri za Mungu, tunaweza kuhitimu kwa ile “nyumba” iliyosemwa na Yesu wakati Yeye alitamka: “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; … maana naenda kuwaandalia mahali … ili nilipo mimi, nanyi mwepo.”7

Ingawa tunakuja katika maisha ya muda katika maisha ya duniani “mawimbi yafuatayo ya utukufu,” maisha yanasonga mbele bila kusita. Ujana ufuata utoto, na ukomavu huja bila kutambulika. Kutokana na uzoefu tunaojifunza haja ya kufikia mbinguni kwa usaidizi tunapotafuta njia katika mapito ya maisha.

Mungu, Baba yetu, na Yesu Kristo, wameweka njia alama hadi ukamilisho. Wanatuita sisi tufuatie kweli za milele na kuwa wakamilifu, kama Wao walivyo kamili.8

Mtume Paulo alilinganisha maisha na mbio. Kwa Waebrania aliwasihi, “Tuweke kando …dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.”9

Katika ari, tusikutilia maana ushauri wa busara kutoka kwa Mhubiri: “Si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani.”10

Ninapotazama mbio za maisha, nakumbuka mbio za aina ingine, hata kutoka siku za utotoni. Marafiki zangu nami tulitwaa visu vidogo wa kukunja na, kutoka kwa mbao laini za mti maji, tulijenga mfano wa mashua ndogo. Kwa anga ya umbo la pembetatu mraba ya kitambaa cha pamba, kila mmoja wetu alishua chombo katika mashindano katika maji maasi ya Mto Provo wa Utah. Tungekimbia kwenye ukingo wa mto na kutazama vyombo vidogo wakati mwingine vikiyumbayumba sana katika mkondo wa kasi na wakati mwingine hivi vilisafiri shwari jinsi maji yalipata kina.

Wakati wa mashindano fulani, tuliona kwamba mashua moja iliongoza zile zingine kuelekea mstari wa kumalizia uliyowekwa. Ghafula, mkondo unaichukua karibu sana na kizingia cha maji kikubwa, na hiyo mashua ikipinduka na kuzama. Ilizungushwazungushwa na kubebwa, isiweze kurudi katika mkondoni. Na mwishowe kutua vibaya huko katika takataka iliyoizunguka kuishikilia kwa minyiri yenye kubana ya kuvumwani ya kijani.

Mfano ya mashua ya utotoni haikuwa na mkuku wa uthabiti, haikuwa na usukani wa kupatiana mwekeleo, na haikuwa na mtambo wa nguvu. Bila shaka cha safari yake kilikuwa kufuata mkondo—mapito yaliyo na pingamizi kidogo.

Tofauti na mifano ya mashua, sisi tumepatiwa sifa za kiasili za kutongoza katika safari yetu. Tunaingia katika maisha ya muda sio kuelea katika mikondo ivumayo ya maisha bali kwa uwezo wa kufikiria, akili, na kupata.

Baba yetu wa Mbinguni Hakutushua sisi katika safari yetu ya milele bila kutupatia njia ambazo kwazo tungeweza kupokea kutoka Kwake mwongozo ili kuhakikisha kurudi kwetu salama. Naongea kuhusu maombi. Naongea pia kuhusu ushawishi kutoka kwa ile sauti ndogo, tulivu; Sijasahau maandiko matakatifu, ambayo yana neno la Bwana na maneno ya manabii—yanayotupatia sisi usaidizi wa kufanikiwa kuvuka mstari wa kumaliza.

Wakati fulani katika maisha yetu ya muda, kunatokeza hatua za kisitasita, tabasamu chovu, maumivu ya ugonjwa—hata kuparara kwa ujana, kufikia nyakati za kupukutika, kugandamana, na uzoefu tunaouita kifo.

Kila mtu wenye makini ameshajiuliza swali lililosemwa vyema na Ayubu wa kale: “Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena?”11 Tunaweza kujaribu kuliweka kando hilo swali, daima litarudi. Kifo huja kwa kila mwanadamu. Huja kwa wazee wanapositasita miguu. Mwito wake usikika na wale ambao hawajafika haya katikati ya safari ya maisha. Nyakati zingine hunyamazisha kucheko cha watoto wadogo.

Na je! Kuwepo baada ya kifo? Kifo ni mwisho wa yote? Robert Blatchford katika kitabu chake God and My Neighbor, alishambulia vikali sana imani zinazokubalika za Kikristo kama vile Mungu, Kristo, maombi na hasa maisha ya milele. Alisisitiza kwamba kifo kilikuwa mwisho wa kuishi kwetu na kwamba hakuna yeyote anayeweza kuthibitisha vingine. Kisha kitu cha kushangaza kikafanyika. Ukuta wa shaka ghafula ukabomoka hata mavumbini. Yeye akawachwa wazi na bila kinga. Pole pole akaanza kuhisi njia yake hata kwenye imani ambayo alikuwa anakejeli na kuiacha. Ni nini lichokuwa kimelete haya mabadiliko yake? Mke wake alikuwa amefariki. Kwa moyo uliovunjika alienda hadi kwenye chumba ambako mwili wa mke ulikuwa umelazwa. Akatazama tena uso wa ambao alikuwa anaupenda sana. Akitoka nje, alisema kwa rafikiye: “Ni yeye na hali si yeye. Kila kitu kimebadilika. Kitu kilichokuwepo awali kumetwaliwa. Siye yule yule. Ni kitu gani kilichokwenda kama si nafsi?”

Baadaye aliandika: “Kifo sio vile watu fulani wanavyofikiria. Ni kama vile tu kwenda katika chumba kingine. Katika hicho chumba kingine tutapata … wanawake na wanaume wapendwa na watoto wazuri tuliopenda na kupoteza.”12

Ndugu na kina dada, sisi tunajua kwamba kifo siyo kikomo. Ukweli huu umefunzwa na manabii walio hai katika nyakati zote. Pia unapatikana katika maandiko matakatifu yetu. Katika Kitabu cha Mormoni tunasoma maneno mahususi na ya kufariji:

“Sasa, kuhusu hali ya roho kati ya kifo na ufufuo—Tazama, nimejulishwa na malaika, kwamba roho za watu wote, mara zinapotoka kwa mwili huu wa muda, ndio, roho za watu wote, zikiwa njema au ovu, zinachukuliwa nyumbani kwa yule Mungu ambaye alizipatia uhai.

“Na ndipo itakuja kuwa kwamba roho za wale walio haki zinapokelewa kwa hali ambayo ni ya furaha, ambayo inaitwa peponi, hali ya kupumzika, hali ya amani, ambapo zitapumzikia kutoka kwa taabu zao zote na kutoka kwa mashaka yote, na masikitiko.”13

Baada ya Mwokozi kusulubiwa na mwili Wake kulazwa katika kaburi kwa siku tatu, roho iliingia ndani tena. Jiwe lilisukumwa mbali,na Mkombozi mfufuka akaenenda mbele, amevikwa kwa mwili wa nyama na mifupa usiokufa.

Jibu la swali la Ayubu, Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Lilikuja kwa Mariamu na wengine waliokwenda kwenye kaburi na kuwaona watu wawili waliokuwa na mavazi ya kumeremeta ambao wasema na wao: “Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Hayupo hapa, amefufuka.”14

Kama matokeo ya ushindi wa Kristo dhidi ya kaburi, sisi sote tutafufuka. Huu ndio ukombozi wa nafsi. Paulo aliandika: “Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.”15

Ni utukufu wa selestia ambao tunataka. Ni katika uwepo wa Mungu tunatamani kuishi. Ni familia za milele ambazo tunataka ushiriki wake. Baraka kama hizo zinapatikana kupitia kujitahidi maishani, kutafuta, kutubu, na mwishowe kufaulu.

Je! Tulitoka wapi? Je! Kwa nini tuko hapa? Je! Tutaenda wapi baada ya maisha haya? Haifai kamwe kuwa maswali haya muhimu kukosa kujibiwa. Kutoka kwa kina cha nafsi yangu na katika unyenyekevu wote, mimi nashuhudia kwamba hivi vitu vyote ambavyo nimeongea ni vya kweli.

Baba yetu wa Mbinguni hufurahia kwa ajili ya wanaoweka amri Zake. Yeye anajali pia mtoto aliyepotea, kijana ajizi, kijana mpotevu, mzazi mkosaji. Kwa upole Bwana anasema na hawa, na hasa kwa wote: “Njoni tena, Njoni hapa. Njoni ndani. Njoni nyumbani. Njoni kwangu.”

Katika wiki moja sisi tutasherekea Pasaka. Mawazo yetu yatageukia maisha ya Mwokozi, kifo Chake, ufufuko Wake. Kama shahidi maalumu Wake, nashuhudia kwenu kwamba Yeye yu hai na kwamba Yeye anangojea kurudi kwetu kwa ushindi. Kwamba kurudi kama huku kutakuwa kwetu, naomba kwa unyenyekevu—hata Yesu Kristo, Mwokozi wetu na Mkombozi wetu, amina.

Chapisha