Vijana
Katikati ya Matayarisho Yako ya Misheni
Rais Uchtdorf anawaambia wamisionari kujifikiria wenyewe kama kuwa katikati ya misheni zao. Unaweza pia kutumia hili wazo kwa matayarisho yako ya misheni: hata kama una umri wa miaka 12 au 18, unaweza kujitayarisha kuhudumu misheni.
Ni vitu gani unavyoweza kufanya “katikati” ya matayarisho yako ya misheni?
-
Daima kuwa mstahiki kuhudhuria hekalu.
-
Jifunze kutambua mnong’ono kutoka kwa Roho Mtakatifu kwa kuandika chini mnong’ono wako na kutenda juu yake.
-
Ombeeni wamisionari.
-
Waulize wamisionari wa eneo lako kile wanachoweza kukushauri kufanya ili kujitayarisha kuhudumu misheni.
-
Jifunze kusimamia wakati wako vyema, ikijumuisha shughuli muhimu kama vile huduma, masomo ya maandiko, na kuandika shajara.
-
Unapoongea na mwanafamilia, shiriki maandiko yaliyokupatia maongozi majuzi. Elezea kile unachofikiria kuhusu maandiko.
-
Waulize marafiki zako kuhusu dini zao na kile wanachoamini. Kuwa tayari kushiriki imani yako. Waalike kanisani au kwenye shughuli.
Kama unavyotambua kwamba uko katikati ya matayarisho yako ya misheni, unaweza kuishi maisha yako kuwa mstahiki kwa kuaminiwa na Bwana na uenzi wa Roho.