2012
Daima kuwa Katikati
Julai 2012


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Julai 2012

Daima kuwa Katikati

Na Rais Dieter F. Uchtdorf

Kwa kalenda nyingi za ulimwengu, Julai uashiria katikati mwa mwaka. Hali mwanzo na mwisho wa mambo usherekewa na kukumbukwa, katikati ya mambo hupitaw bila kutambulika.

Mwanzo ni nyakati za kufanya azimio, kuanzisha mipango, mpasuko wa nishati. Mwisho ni nyakati za kumaliza na unaweza kujumuisha hisia za ukamilishaji au kupoteza. Lakini kwa mtazamo mwema, kujichukulia sisi kama kuwa katikati ya mambo kunaweza kutusaidia sio tu kuelewa maisha vyema zaidi bali pia tutayaishi vyema zaidi.

Katikati ya Kazi ya Umisionari

Ninapoongea na wamisionari wetu vijana, kila mara huwambia wao wako katikati ya misheni zao. Hata kama wamewasili siku iliyopita au wanaondoka kwenda nyumbani siku ifuatayo, huwauliza wajifikirie daima kama kuwa katikati.

Wamisionari wapya wanaweza kuhisi kuwa hawana uzoefu kabisa, na wanachelewa kuongea au kutenda kwa imani na ujasiri. Wamisionari mahiri ambao wako karibu kumaliza misheni zao wanaweza kuhisi huzuni misheni zao zinafikia mwisho, au wanaweza kulegea wanapofikiria kile watafanya baada ya misheni zao.

Hata hali ikiwa vipi na popote wanapohudumu, ukweli ni kwamba wamisionari wa Bwana kila siku wanapanda mbegu zisizohesabika za habari njema. Wakijifikiria daima kuwa katikati ya misheni zao kutawatia hamasa na kuwapataia nguvu hawa wawakilishi waaminifu wa Bwana. Kama ilivyo kwa wamisionari, ndivyo ilivyo kwetu sote.

Tuko Daima Katikati

Mabadiliko haya katika mtazamo ni zaidi ya kitimbi rahisi cha akili. Kuna ukweli mtukufu ndani ya wazo kwamba tupo daima katikati. Kama tukitazama eneo letu katika ramani, tunaweza kujaribu kusema kuwa tuko mwanzoni. Lakini kama tukitazama kwa makini, popote tulipo ni kihalisi katikati ya sehemu kubwa.

Kama vile ilivyo na uwanda, ndivyo ilivyo na wakati. Tunaweza kuhisi tuko mwanzoni au mwisho wa maisha yetu, lakini tunapotazama pale tulipo dhidi ya madhari ya umilele—ndio tunagundua kwamba roho zetu zilikuwepo kwa wakati ulio zaidi ya uwezo wa kupima na, kwa sababu dhabihu kamili na Upatanisho wa Yesu Kristo, ndiyo nafsi zetu zitakuwepo kwa milele ijayo—tunatambua kwamba kwa kweli tuko katikati.

Majuzi nilihisi msukumo wa kutengeneza upya mawe ya makaburi ya wazazi wangu. Muda umedororesha sehemu ya makaburi, na nilihisi kwamba jiwe jipya lingefaa kwa mfano wao mwema wa maisha. Nilipotazama tarehe za kuzaliwa na tarehe za kufariki katika jiwe zikiunganishwa na dashi ndogo, hii alama ndogo ya maisha yote ghafula ilijaza akili yangu na moyo wangu na utele wa kumbukumbu nzuri. Kila moja wa hizi kumbukumbu za thamani zinamlika chembe katika maisha ya wazazi wangu na katikati ya maisha yangu.

Hata uwe umri gani, hata maeneo yetu yaweje, mambo yanapotokeza katika maisha yetu, tuko daima katikati. Zaidi ya hayo, tutakuwa katikati milele.

Tumaini la Kuwa Katikati

Naam, kutakuwa na nyakati za kuanza na nyakati za kumaliza maishani mwetu mwote, lakini hizi ni marka tu katika njia ya katikati kuu ya maisha yetu ya milele. Kama tuko mwanzo au mwisho, kama tu vijana au wazee, Bwana anaweza kututumia kwa madhumuni Yake kama kiurahisi tutaweka kando mawazo yoyote yanayozuia uwezo wetu wa kuhudumu na kukubali mapenzi Yake kutengeneza maisha yetu.

Mtunga zaburi alisema, Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, Tutashangilia na kuifurahia. (Zaburi 118:24). Amuleki anatukumbusha kwamba “maisha haya ndiyo wakati wa watu kujitayarisha kukutana na Mungu; ndio, tazama, wakati wa maisha haya ndiyo siku ya watu kufanya kazi yao wanayohitaji. Alma 34:32 mkazo umeongezewa). Naye mshairi anawaza, “Milele—vijenzi vyake ni Sasa.”1

Kuwa daima katikati inamaanisha kwamba mchezo haujaisha kamwe, tumaini halijapotea kamwe, kushindwa sio mwisho. Kwani bila kujali pale tulipo au hali zetu ni zipi, umilele wa mwanzo na umilele wa mwisho umetandikwa mbele zetu.

Daima Tuko Katikati.

Muhtasari

  1. Emily Dickinson, “Forever—is composed of Nows,” in The Complete Poems of Emily Dickinson, ed. Thomas H. Johnson (1960), 624.

Kufundisha Ujumbe Huu

Fikiria kuzungumza na familia jinsi wao wako “daima katikati,” hata kama wanaanza au kumaliza kitu. Watie moyo kufanya vyema wawezavyo katika shughuli zao za sasa, wasishindie yaliyopita au wasingojee shughuli zifuatazo au mradi. Unaweza kuwashauri wachague kitu kimoja wanachoweza kufanya kama familia kutekeleza ushauri huu na kuweka tarehe ambayo kwayo wanatumainia kukamilisha hiyo shabaha.