Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Oktoba 2012
Kuheshimu Maagano Yetu
Soma kifaa hiki kwa maombi na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.
Ualimu Tembelezi ni ishara ya uanafuzi wetu na njia ya kuheshimu maagano yetu tunapohudumiana na kuimarishana mmoja na mwingine. Agano ni ahadi takatifu na ya kudumu kati ya Mungu na watoto Wake. “Tunapotambua kwamba sisi ni watoto wa agano, tunafahamu sisi ni kina nani na kile Mungu anachotarajia kutoka kwetu,” alisema Mzee Russell M. Nelson wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili. “Sheria Yake imeandikwa katika mioyo yetu. Yeye ni Mungu wetu na sisi ni watu Wake.”1
Kama waalimu watembelezi tunafaa kuwaimarisha wale tunaowatembelea katika juhudi zao za kuweka maagano yao matakatifu. Kwa kufanya hivyo, tunawasaidia wao kujitayarisha kwa baraka za uzima wa milele. “Kila dada katika Kanisa hili ambao wamefanya maagano na Bwana wana jukumu takatifu la kusaidia kuokoa nafsi, kuongoza wanawake wa ulimwengu, kuimarisha nyumba za Sayuni, kujenga ufalme wa Mungu,”2 alisema Mzee M. Russell Ballard wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili.
Tunapofanya na kuweka maagano matakatifu, tunakuwa vyombo katika mikono ya Mungu. Tutakuwa tunaweza kueleza kwa ufasaha imani yetu na kuimarisha imani ya kila mmoja katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Kutoka kwa Maandiko
1 Nefi 14:14; Mosia 5:5–7; 18:8–13; Mafundisho na Maagano 42:78; 84:106
Kutoka kwa Historia Yetu
Hekalu ni “mahali pa shukrani kwa watakatifu wote,” Bwana alifunua kwa Nabii Joseph Smith katika mwaka wa 1833. Ni “mahali pa mafunzo kwa wale wote walioitwa kufanya kazi ya huduma katika miito na ofisi zao zote mbalimbali; Ili waweze kukamilishwa katika ufahamu wa huduma zao, katika nadharia, katika kanuni, na katika mafundisho, katika mambo yote yahusuyo ufalme wa Mungu juu ya dunia, ufalme ambao funguo zake zimewekwa juu yenu” (M&M 97:13–14).
Kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama katika Nauvoo, Illinois, katika miaka ya mapema ya 1840 walisaidiana kutayarisha maagizo ya hekalu. Katika maagizo ya ukuhani mkuu ambao Watakatifu wa Siku za Mwisho walipokea katika Hekalu la Nauvoo, “nguvu za uchamungu [zili] dhihirisha” (M&M 84:20). Jinsi vile Watakatifu waliweka maagano yao, hizi nguvu ziliwaimarisha na kuwahimili wao katika majaribu yao katika siku na miaka iliyokuwa mbele zao.”3
Katika Kanisa siku hizi, wanawake na wamaume watakatifu kote ulimwenguni wanahudumu katika mahekalu na wanaendelea kupata nguvu katika hizi baraka ambazo zinaweza kupokelewa tu katika maagano ya hekalu.
© 2012 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/11. Tafsiri iliidhinishwa: 6/11. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, October 2012. Swahili. 10370 743