2012
Mkesha wa Krismasi Kamilifu
Desemba 2012


Vijana

Mkesha wa Krsimasi Kamilifu

Nilipokuwa nikikua, mojawapo ya sehemu ya kuvutia ya kila mwaka ilikuwa Mkesha wa Krismasi. Familia yangu nami tulitengeneza piza, tukaenda kuimba nyimbo za Krismasi kisha tukakusanyika kwa ibada ya Krismasi. Tuliimba nyimbo kati sehemu nne patanifu kwa udhaifu na tuliimba kwa sauti kubwa nyimbo za krismasi katika mkusanyiko wa ajabu wa vifaa vyetu vya muziki. Baba yetu kila mara alihitimisha jioni kwa wazo la Krismasi lililotuacha na machozi ya furaha. Maisha hayangeweza kuwa bora kuliko Mkesha wa Krismasi.

Nilipokuwa mkubwa kidogo, mama yangu alianza kumtunza jirani mdogo, Kelly. Kelly alikuja nyumbani kwetu kila siku baada ya shule wakati mama yake Patty, alifanya kazi. Kelly alinifuatafuata kama mwanambwa—mwenye kelele na mhitaji. Ilikuwa nafuu kila mara wakati Patty alipomchukua binti yake na kuondoka nyumbani kwetu na kuacha familia yangu kwa amani.

Disemba moja, nilishtuka wakati mama alimwalika Pati na Kelly kujumuika nasi katika Mkesha wa Krismasi. Mkesha wa Krismasi wangu. Mama alitabasamu na kunihakikishia, “Haitabadili chochote.” Lakini nilijua vyema. Wangekula pizza yetu yote. Kelly angedhihaki kuimba kwetu. Nilijitanibu kuwa na Mkesha wa Krismasi mbaya kabisa.

Jioni ilipoingia, Patty na Kelly walijumuika nasi, na tuliongea na kucheka na kuimba. Mama alikuwa sahihi Ilikuwa kamilifu. Usiku wa manane walitushukuru na shingo upande tukaachana. Nilienda kitandani na moyo uliojaa. Niligundua kuwa zawadi za thamani kweli za Krismasi hazipungui zikigawa. Badala yake zinakuwa tamu na kuongezeka tunapozipeana.