2012
Kugundua upya Roho ya Krismasi
Desemba 2012


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Disemba 2012

Kugundua upya Roho ya Krismasi

Rais Thomas S. Monson.

Miaka iliyopita nikiwa mzee kijana, niliitwa pamoja na wengine katika hospitali Salt Lake City kutoa baraka kwa watoto wagonjwa. Mara baada ya kuingia, tuliona kuwa mti wa Krismasi pamoja na mataa yake angavu na ya urafiki na kuona pakiti zilizofungwa kwa uangalifu chini ya viungo vyake vilivyonyoshwa. Kisha tukapitia ushoroba ambapo wavulana na wasichana wadogo—wengine wakiwa na plasta katika mikono au miguu, wengine wakiwa na magonjwa ambayo pengine hayangeponywa haraka—walitusalimia kwa nyuso za tabasamu.

Mvulana mdogo, mgonjwa sana alisema nami “Jina lako ni nani?”

Nikamwambia jina langu, akauliza, “Je! Utanipa baraka?”

Baraka ilipeanwa, na tulipogeuka kuondoka kitandani mwake, alisema, “Asante sana”

Tulitembea hatua chache na kisha nikasikia akiita, “Oh, Ndugu Monson, Krismasi njema kwako.” Kisha tabasamu kubwa iliangaza kote usoni mwake.

Mvulana huyo alikuwa na roho ya Krismasi. Roho ya Krismasi ni kitu ambacho ninatumaini kila mmoja wetu angekuwa nacho katika mioyo yetu na maisha yetu—sio tu kwa huu msimu hasa bali pia kote katika mwaka.

Tunapokuwa na roho ya Krismasi, tunamkumbuka Yeye ambaye kuzaliwa kwake tunasherehekea katika msimu huu wa mwaka: “Maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu Mwokozi, ndiye Kristo Bwana” (Luka 2:11).

Katika siku yetu, roho ya kutoa zawadi huchukua nafasi kubwa katika kusherehekea msimu wa Krismasi. Nashangaa kama tunaweza kufaidika kwa kujiuliza, Ni zawadi zipi ambazo Bwana angetaka mimi kumpa au kuwapa wengine katika msimu huu wa thamani wa mwaka?

Hebu nipendekeze kuwa Baba yetu wa mbinguni angetaka kila mmoja wetu kumpa Yeye na Mwanawe zawadi ya utiifu. Ninahisi kuwa angetuuliza kujitolea na kutokuwa wachoyo au wenye tamaa au wenye ugomvi kama vile Mwanawe wenye thamani anapendekeza katika Kitabu cha Mormoni:

“Kwani amin, amin, nawaambia, yule ambaye ana roho ya ubishi siye wangu, lakini ni wa ibilisi, ambaye na huchochea mioyo ya watu kubishana na hasira mmoja kwa mwingine.

Tazama, hili sio fundisho langu, kuchochea mioyo ya wanadamu kwa hasira, moja dhidi ya mwingine; lakini hili ndilo fundisho langu, kwamba vitu kama hivi viondolewe mbali.” (3 Nefi 11:29–30).

Katika kipindi hiki cha ajabu cha utimilifu wa nyakati, nafasi zetu za kupenda na kujitolea kusio na mipaka, bali pia azimaliziki. Hivi leo kuna mioyo ya kufurahisha, maneno ya upole ya kusema, matendo ya kufanywa na nafsi za kuokolewa.

Mmoja aliyekuwa na ufahamu makini wa roho ya Krismasi aliandika:

Mimi ndiye roho ya Krismasi—

Ninaingia nyumba ya umaskini, nikisababisha watoto wenye nyuso zilizochujuka kufungua macho yao wazi, katika mshangao wa furaha.

Ninasababisha mikono iliyofungwa ya mchoyo kufumuliwa na hivyo kupaka alama angavu katika nafsi yake.

Ninawasababisha wakongwe kutengeneza upya ujana wao na kucheka katika njia kongwe ya furaha.

Ninaweka hai mahaba katika roho ya utoto, na kuangaza usingizi kwa ndoto za ajabu.

Ninasababisha miguu yenye hamu kupanda ngazi zenye giza na mikoba iliyojaa, wakiacha nyuma nyoyo zilizoshangazwa na wema wa dunia. .

Ninasababisha mpotevu kutua katika asili yake ya uharibifu, na kutuma kwa wenye upendo wa wasiwasi ishara ndogo inayoachilia machozi ya furaha—machozi ambayo yanaonsha mistari migumu ya huzuni.

Ninaingia katika seli za korokoroni, nikikumbusha uume ulio na uoga kuhusu kile ambacho kingekuwa na kuwaashiria siku njema zijazo.

Ninakuja polepole katika nyumba tulivu nyeupe ya uchungu, na midomo iliyodhaifu sana kuzungumza, inayotetemeka tu katika kimya na shukrani ya uwazi.

Katika miaka elfu moja, ninasababisha ulimwengu uliochoka kuona juu katika uso wa Mungu na kwa muda mdogo kusahau vitu ambavyo ni vidogo na vya unyonge.

Mimi ni Roho ya Krismasi.1

Na acha kila mmoja wetu agundue roho ya Krismasi—hata Roho wa Kristo.

Muhtasari

  1. E. C. Baird, “Christmas Spirit,”Katika James S. Hewitt, ed., Illustrations Unlimited

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Unaposhiriki ujumbe wa Rais Monson na familia, fikiria kusisitiza swali lililoulizwa kuhusu zawadi ambazo Bwana angetaka sisi kumpa Yeye au wengine katika msimu huu. Wahimize wanafamilia kurekodi fikira zao na mawazo yao (au kwa watoto wadogo, kuchora picha) kuhusu jinsi ya “kugundua upya roho ya Krismasi—hata Roho wa Kristo.”