2013
Ujumbe kwa Misonari anayesita
Februari 2013


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Februari 2013

Ujumbe kwa Misionari anayesita

Rais Dieter F. Uchtdorf

Wafuasi wa Yesu Kristo daima wamekuwa na jukumu la kupeleka injili Yake duniani. (Ona Marko 16:15 – 16). Hata hivyo, wakati mwingine ni vigumu kufungua midomo yetu na kuongea kuhusu imani yetu kwa wale walio karibu nasi. Huku baadhi ya washiriki wa Kanisa wakiwa na kipaji asili cha kuzungumzia wengine kuhusu injili, wengine husita kidogo au huhisi kufedheheshwa, kuaibika, ama hata uoga wa kufanya hivyo.

Kwa madhumuni hayo, acha nipendekeze vitu vinne ambavyo yeyote anaweza kufanya ili kufuata agizo la Mwokozi kuhubiri injili “kwa kila kiumbe” (M&M 58:64).

Kuwa Mwangaza

Msemo ninaoupenda sana unaodhaniwa mara nyingi kuwa wa St. Francis wa Assisi unasoma, “Hubiri injili kila wakati na ikihitajika, tumia maneno.”1 Kilicho wazi katika msemo huu ni kuwa mara nyingi mahubiri ya kuvutia zaidi huwa hayasemwi.

Wakati tuna uadilifu na kuishi kwa viwango vyetu kwa uaminifu, watu hufahamu. Tunaponururisha shangwe na furaha, wao huona hata zaidi.

Kila mtu anataka kuwa na furaha. Wakati sisi washiriki wa Kanisa tunanururisha mwangaza wa injili, watu wanaweza kuona furaha yetu na kuhisi upendo wa Mungu ukijaza na kupindukia maishani mwetu. Wanataka kujua ni kwa nini. Wanataka kuelewa siri yetu.

Hio huwaelekeza kuuliza maswali kama vile “Ni kwa nini una furaha sana?” ama “Ni kwa nini wewe huwa na mtazamo mwema kila wakati?” Majibu ya maswali haya, kwa kawaida, huelekezea kikamilifu mjadala kuhusu injili rejesho ya Yesu Kristo.

Kuwa wa Kuzungumza

Kuleta mada ya dini hasa kwa marafiki na wapendwa wetu kunaweza kuonekana vigumu na kuwa na changamoto. Haifai kuwa. Kutaja uzoefu wa kiroho au kuzungumza kuhusu shughuli za Kanisa au matokeo katika majadiliano ya kawaida kunaweza kuwa rahisi na kwa kufurahisha tukiweka ushujaa na maarifa ya kawaida.

Mke wangu, Harriet, ni mfano mzuri. Tulipokuwa tunaishi Ujerumani, angepata njia ya kutia mada inayohusiana na Kanisa katika majadiliano yake na marafiki na jamaa. Kwa mfano, wakati mtu aliuliza kuhusu wikendi yake, angesema, “Jumapili hii tulikuwa na tukio la kuvutia katika kanisa letu! Mvulana chipukizi mwenye miaka 16 alitoa hotuba mzuri mbele ya mkusanyiko wa watu 200 kuhusu kuishi maisha masafi.” Ama, “Nilijifunza kuhusu mwanamke mwenye umri wa miaka 90 ambaye alishona blanketi zaidi ya 500 na kuzipatia mpango wa usaidizi wa Kanisa ili kutumiwa watu wanaohitaji duniani kote.”

Mara nyingi, watu ambao walisikia haya walitaka kujua zaidi. Waliuliza maswali. Na hiyo ilielekezea fursa za kuongea kuhusu injili kwa njia ya kawaida, ujasiri, bila kusukumiza.

Na mwanzo wa matumizi ya tovuti na vyombo vya habari vya jamii, ni rahisi siku hizi kuzungumza kuhusu mambo haya kwa njia ya majadiliano kushinda awali. Kile tunahitaji ni ujasiri tu wakufanya hivyo.

Kuwa wa kujawa na Neema

Kwa bahati mbaya, ni rahisi sana kubishana. Inafanyika mara nyingi kwamba sisi hugombana, hudharau, na kulaani. Wakati tunapokuwa na hasira, wafidhuli, au wa kuumiza watu, jambo la mwisho wanalotaka ni kujifunza zaidi kutuhusu. Haiwezekani kujua ni watu wangapi wameacha Kanisa au kamwe kujiunga na Kanisa kwa sababu mtu alisema kitu kilichowaumiza au kuwaudhi.

Kuna ufidhuli mwingi katika dunia siku hizi. Kwa sababu ya kutokujulikana katika tovuti, ni rahisi zaidi kuliko awali kusema mambo mabaya au maovu kwenye mtandao. Je, hatupaswi sisi, wafuasi tutumaini Kristo wetu mpole, kuwa na kiwango cha juu zaidi cha hisani? Maandiko yanafundisha, “Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu” (Wakolosai 4:6).

Ninapenda wazo la maneno yetu kuwa wazi kama anga ya jua na wingi wa neema. Je, unaweza kufikiria vile familia zetu, vigingi, mataifa, na hata dunia ingelikuwa kama tungeweza kutumia kanuni hii rahisi?

Jawa na Amani

Wakati mwingine sisi hujichukulia sifa nyingi, au lawama nyingi wanapokuja wengine kukubali injili. Nimuhimu kukumbuka kwamba Bwana hatarajii sisi kufanya uongofu.

Uongofu huja si kupitia maneno yetu lakini kupitia hudumua ya mbinguni ya Roho Mtakatifu. Wakati mwingine kile kinachotakikana tu ni kishazi kimoja cha ushuhuda wetu au kuhusu tukio ili kuanzisha ulainishaji wa moyo au ufunguzi wa mlango unaoweza kuwaongoza wengine kufurahia ukweli mtukufu kupitia ushawishi wa Roho.

Rais Brigham Young (1801–77) alisema alijua injili ilikuwa kweli wakati “alimuona mtu bila lugha ya kushawishi, au kipaji cha kuhutubia umati, ambaye aliweza kusema tu, ‘Ninajua, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kuwa Kitabu cha Mormoni ni cha kweli, kuwa Joseph Smith ni Nabii wa Bwana’”. Rais Young alisema wakati alisikia ushuhuda huo wa unyenyekevu, “Roho Mtakatifu alitoka kwenye mtu huyo binafsi akamulika ufahamu wangu, na mwangaza, utakatifu, na uzima wa milele ukawa mbele yangu”.2

Ndugu na dada, iweni na amani. Bwana anaweza kutukuza maneno unayosema na kuyafanya yawe yenye nguvu. Mungu hawaulizi kubadilisha watu lakini tu kufungua midomo yenu. Kazi ya kuongoa watu si yako, hiyo ni ya mtu anayesikiliza, na ya Roho Mtakatifu.

Kila Mshiriki mmisionari

Marafiki zangu wapendwa, leo kuna njia zaidi kuliko awali ya sisi kufungua midomo yetu na kushiriki na wengine ujumbe wa furaha wa injili ya Yesu Kristo. Kuna njia ya kila mtu —hata mmisionari anaye sita— kushiriki katika kazi hii kuu. Kila mmoja wetu tunaweza kupata njia ya kutumia vipaji vyetu vya kipekee na shauku katika kuhimili kazi hii kuu ya kujaza dunia na nuru na kweli. Tunapofanya hivyo, tutapata furaha inayowajia wale walio waaminifu na wajasiri kutosha “Kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote” (Mosia 18:9).

Muhtasari

  1. St. Francis of Assisi, katika William Fay and Linda Evans Shepherd, Share Jesus without Fear (1999), 22.

  2. Teachings of Presidents of the Church: Brigham Young (1997), 231.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Njia moja ya kufaa ya kufundisha ni “kuhimiza wale unaowafundisha kuweka malengo ambayo yanaweza kuwasaidia kutumia kanuni ulizofundisha” (Teaching, No Greater Call [1999], 159). Fikiria kuwaalika unaowafundisha kuweka lengo kwa maombi kushiriki injili na mmoja au zaidi ya watu mwezi huu. Wazazi wanaweza kujadili jinsi watoto wadogo wanavyoweza kusaidia. Unaweza pia kuwasaidia wanafamilia kuchangia mawazo au kuigiza njia za kuleta injili katika majadiliano ya kawaida na kufikiria juu ya shughuli za Kanisa zinazokuja ambapo wanaweza kualika rafiki.