2014
Msimu wa joto wa Huduma
Februari 2014


Vijana

Msimu wa joto wa Huduma

Mwandishi anaishi Virginia, USA.

Msimu wa joto mmoja nilitumia muda katika nchi ya kigeni nikifanya kazi na watoto walio na mahitaji maalum. Nilipokutana na watoto kwa mara ya kwanza, nilikuwa na woga sana. Sikuongea lugha yao, lakini nilitumaini kwamba Roho angeniongoza katika muingiliano wangu. Nilipopata kujuana na kila mtoto, niligundua kwamba lugha si kizuizi kwa upendo. Nilicheza, nikacheka, na kutengeza sanaa pamoja na watoto na singejizuia ila kuhisi upendo kamili kwao. Nilitazama kwa mara moja upendo ambao Baba wa Mbinguni anao kwa watoto Wake, na furaha iliyojaza moyo wangu ilishinda kuelezeka.

Wakati wowote ninapohudumia wengine, mimi huhisi upendo si tu kwa wale ninaowahudumia lakini pia kwa Baba wa Mbinguni. Hakika nimekuja kujua kwamba “mnapotumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu” (Mosia 2:17). Lengo la huduma yangu, iwe katika miradi mikubwa ya huduma ama kupitia vitendo vidogo vya wema, limekuwa kumtukuza Mungu (ona Mathayo 5:16). Natumaini kwamba ninapohudumia wengine, watu watatambua upendo wangu kwa Baba wa Mbinguni na Nuru ya Kristo inayowaka ndani yangu.