2014
Wito Mtakatifu wa Yesu Kristo: Mchungaji Mwema
Februari 2014


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Februari 2014

Wito Mtakatifu wa Yesu Kristo: Mchungaji Mwema

Kwa maombi jifunze ujumbe huu na jitahidi kujua kile cha kushiriki. Kuelewa maisha na ujumbe wa Mwokozi kutaongezaje imani yako Kwake na kubariki wale unaowaongoza kupitia ualimu tembelezi? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenyewww.reliefsociety.lds.org.

Imani • Familia • Usaidizi

Yesu Kristo, Mchungaji Mwema, alifundisha:

“Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kwenda nyikani, aende kumtafuta yule aliyepotea hata amwone? …

“Nawaambia, vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye” (Luka 15:4, 7).

Tunapokuja kuelewa kwamba Yesu Kristo ndiye Mchungaji Mwema, hamu yetu huongezeka kufuata mfano Wake na kuhudumia walio na mahitaji. Yesu alisema: “Mimi ndimi mchungaji mwema, nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo” (Yohana 10:14–15). Kwa sababu ya Upatanisho wa Kristo, hakuna yeyote miongoni mwetu atakayewahi kuwa amepotea sana kwamba hatuwezi kupata njia yetu kwenda nyumbani. (ona Luka 15).

Rais Thomas S. Monson alisema, “Letu ni jukumu la kutunza mifugo. Tuweze kila mmoja wetu kujitokeza kuhudumu.”1

Kutoka kwenye Maandiko

Zaburi 23; Isaya 40:11; Mosia 26:21

Kutoka kwenye Historia yetu

Elizabeth Ann Whitney, aliyehudhuria mkutano wa kwanza wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alisema kuhusu uongofu wake mnamo 1830: “Mara tu niliposikia injili Wazee walipokuwa wakihubiri, nilijua ilikuwa sauti ya Mchungaji Mwema.”2 Elizabeth alifuata sauti ya Mchungaji Mwema na akabatizwa na kudhibitishwa kama mshiriki.

Sisi pia tunaweza kusikia sauti ya Mchungaji Mwema na kushiriki mafunzo Yake na wengine. Rais Monson alisema, “Sisi ndio mikono ya Bwana duniani, tukiwa na jukumu la kuhudumu na kuinua watoto Wake.”3

Kama tu vile mchungaji hutafuta kondoo aliyepotea, wazazi wanaweza kumtafuta mtoto aliyepotea. Rais James E. Faust (1920–2007), Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alisema: “Kwa wazazi wale waliovunjika moyo ambao wamekuwa wema, wa kujitahidi, na wa kuomba katika kufundisha watoto wao wasiotii, tunasema kwenu, Mchungaji Mwema anawaangalia. Mungu anajua na anaelewa huzuni wenu wa kina. Kuna tumaini.”4

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, “Heavenly Homes, Forever Families,” Liahona, Juni 2006, 70.

  2. Elizabeth Ann Whitney, katika Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 128.

  3. Thomas S. Monson, “What Have I Done for Someone Today?” Liahona,Nov. 2009, 86.

  4. James E. Faust, “Dear Are the Sheep That Have Wandered,” Liahona, Mei 2003,68

Naweza Kufanya Nini?

  1. Kujua kwamba Mwokozi ndiye Mchungaji Mwema kunawezaje kuleta amani maishani mwako?

  2. Tunaweza kutumikia kwa njia gani wale ambao “wamepotea” kutoka ushiriki Kanisani ama wale ambao si wa imani yetu?

  3. Ninawezaje kuwasaidia wazazi ambao watoto wao wamepotoka kutoka kwa kuishi injili?

Chapisha