2015
Sifa za Kiungu za Yesu Kristo: Mwenye Nguvu na Aliyejawa na Utukufu
Septemba 2015


Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji, Septemba 2015

Sifa za Kiungu za Yesu Kristo: Mwenye Nguvu na Aliyejawa na Utukufu

Kwa sala jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kufundisha. Kuelewa sifa tukufu za Mwokozi kunawezaje kuongeza imani yako Kwake na kuwabariki wale unaowachunga kwa njia ya ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda reliefsociety.lds.org.

Picha
Nembo ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani, Familia, Usaidizi

Maandiko yanatufundisha kuwa Yesu Kristo “akapokea uwezo wote, kote mbinguni na duniani, na utukufu wa Baba ulikuwa pamoja naye” (M&M 93:17). Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ma Mitume Kumi na Wawili alisema kuwa kupitia nguvu hizi Mwokozi wetu aliumba mbingu na dunia, akafanya miujiza, akavumilia uchungu wa Gethsemane na Kalvari.1 Tunapofika kuelewa hili, Imani yetu katika Kristo itaongezeka na tutaimarika zaidi.

Tunapofanya na kuweka maagano ya Hekaluni, Bwana hutubariki kwa nguvu zake. Linda K. Burton, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama alisema: “Kushika maagano huimarisha, hutupa nguvu na kutulinda. … Hivi majuzi nilikutana na rafiki mpya mpendwa. Alishuhudia kwamba baada ya kupokea endaumenti yake ya hekaluni, alisikia kuimarishwa na nguvu ya kuweza kushinda majaribu.”2

Nefi anashuhudia kuhusu nguvu za maagano: “Mimi, Nefi, niliona nguvu za Mwanakondoo wa Mungu, kwamba zilishuka … juu ya watu wa agano wa Bwana, … na walikuwa wamejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu katika utukufu mkuu. (1 Nefi 14:14).

Maandiko ya Ziada

Yeremia 51:15; Ufunuo 1:6; Yakobo 4:6–7; Mosia 3:17

Kutoka katika Maandiko

Akiwa amejawa na huruma kwa Martha na Maria, Yesu Kristo alimfufua kaka yao Lazaro kutoka kwa wafu kwa nguvu ya Mungu aliyokuwa nayo.

Yesu alifika nyumbani mwa Martha na Maria baada ya Lazaro kuwa kaburini kwa siku nne. Walikwenda kwenya kaburi la Lazaro na Yesu akaamuru kwamba jiwe lililokuwa langoni liondolewe. Yesu Akamwambia Martha “Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?” Kisha akasali kwa Mungu na “akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.

“Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi.” (Ona Yohana 11:1–45.) Mwokozi hutumia nguvu zake kutukomboa na kutuimarisha. Imani yetu Kwake itaongezeka tunapokumbuka kuwa Amejawa nguvu na utukufu.

Muhtasari

  1. Ona M. Russell Ballard, “This Is My Work and My Glory,” Liahona, May 2013, 18.

  2. Linda K. Burton, “The Power, Joy, and Love of Covenant Keeping,” Liahona, Nov. 2013, 111.

Zingatia Hili

Nguvu za Mungu zinatuvika vipi kwa nguvu na utukufu?

Chapisha