2016
Ndoa Imetakaswa na Mungu
Februari 2016


Ujumbe wa Mwalimu MTEMBELEAJI, Februari 2016

Ndoa Imetakaswa na Mungu

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kushiriki. Ni jinsi gani kuelewa “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” kunazidisha imani yako kwa Mungu na kubariki wale unaowachunga kupitia Ualimu wa Kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.

Imani , Familia ,Usaidizi

Manabii, mitume, na viongozi wanaendelea kutangaza kwa “heshima kwamba ndoa kati ya mwanaume na mwanamke imetakaswa na Mungu, na kwamba familia ni ya muhimu katika mpango wa Muumba.”1

Mzee D. Todd Christofferson wa Jamii ya Mitume kumi na Wawili alisema: “Familia iliyojengwa kwa msingi wa ndoa ya mwanaume na mwanamke huleta mazingira bora kabisa kwa mpango wa Mungu kufanikiwa. … “

… Sio sisi au binadamu yeyote anaweza kugeuza huu mpango mtakatifu wa ndoa.”2

Bonnie L. Oscarson, Raisi Mkuu wa Wasichana, alisema: “Kila mtu, haijalishi hali yao ya ndoa au idadi ya watoto, anaweza kuwa mtetezi wa mpango wa Bwana ambao umeelezwa katika tangazo la familia. Ikiwa ni mpango wa Mungu, unafaa kuwa mpango wetu pia.!3

Mzee Christofferson aliendelea: “Wengine wenu hamjabarikiwa na ndoa kwa sababu kama ukosefu wa wakutazamiwa, kuvutiwa na jinsia sawa, ulemavu wa mwili na akili, au tu hofu ya kufeli. … Au waweza kuwa uliolewa, lakini hiyo ndoa ikavunjika. … Wengine kati yenu mliooana hamuwezi kupata watoto. 

… “Hata hivyo, kila mmoja anaweza kuchangia katika kuendeleza mpango mtukufu kwa kila kizazi.”4

Maandiko ya Ziada

Ufunuo 2:18-24; 1 Wakorintho 11:11; Mafundisho na Maagano 49:15–17

Simulizi Hai

Ndugu Larry M. Gibson, aliyekuwa mshauri wa kwanza katika Uraisi Mkuu wa Wavulana, alikumbuka wakati Shirley, sasa bibi yake, alisema:“‘

Nakupenda kwa sababu najua unampenda Bwana kuliko jinsi unavyonipenda mimi.’ … 

“Jibu hilo liligusa moyo wangu. 

“… [Na] Nilimtaka yeye ahisi kila siku kuwa nilimpenda Bwana zaidi ya mengine yote.”5

Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha: “Bwana Yesu Kristo ni kitovu katika uhusiano wa ndoa ya agano. … [Hebu fikiria kuwa] Mwokozi akiwa katika kilele cha pembe tatu, na mwanamke katika wigo wa kona moja na mwanaume katika wigo wa kona ile nyingine. Sasa zingatia kile kinachofanyika katika uhusiano baina ya mwanaume na mwanamke kibinafsi na kimakini ‘wanapokuja kwake Kristo’ na kujitahidi ‘kukamilika ndani Yake’ (Moroni 10:32). Kwa sababu ya na kupitia kwa Mkombozi, mwanaume na mwanamke huja karibu sana pamoja.”6

Muhtasari

  1. Familia Familia: Tangazo kwa Ulimwengu, Liahona, Nov. 2010, 129.

  2. D. Todd Christofferson, The Power of Covenants, Liahona, Mei 2015, 52.

  3. Bonnie L. Oscarson, “Defenders of the Family Proclamation,” Liahona, May 2015, 15.

  4. D. Todd Christofferson, Why Marriage, Why Family, 52.

  5. Larry M. Gibson, Fulfilling Our Eternal Destiny, Ensign, Feb. 2015, 21–22.

  6. David A. Bednar, Marriage Is Essential to His Eternal Plan, Liahona, June 2006, 54.

Zingatia Hili

Ni namna gani mimi binafsi najitahidi ”mje kwa Kristo?“