Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji, Machi 2016
Kuumbwa katika Mfano wa Mungu.
Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kushiriki. Je! Kuelewa “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” kunawezaje kuongeza imani yako katika Mungu na kuwabariki wale unaowachunga kwa njia ya ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;
“Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” (Mwanzo 1:26–27).
Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, na Alituumba kwa mfano Wake. Kuhusu ukweli huu, Rais Thomas S. Monson alisema: “Mungu Baba yetu ana msikio ambayo kwayo anasikia maombi yetu. Yeye ana macho ambayo kwayo anaona matendo yetu. Yeye ana mdomo ambao kwao anatuongelesha. Yeye ana moyo ambao kwao anahisi huruma na upendo. Yeye ni halisi. Yeye yu hai. Sisi watoto wa Mungu, walioumbwa kwa mfano Wake. Tunafanana naye, Naye anafanana nasi.”1
“Watakatifu wa Siku za Mwisho wanawaona watu wote kama watoto wa Mungu katika hali zote na ukamilifu; wanamchukulia kila mtu kuwa na uungu katika uasili, hasili, na uwezo.”2 Kila mmoja ni “mwana ama binti mpendwa wa kiroho wa wazazi wa mbinguni.”2
“[Nabii] Joseph Smith pia alijifunza kwamba Mungu anataka watoto Wake wapokee aina hiyo hiyo ya hali iliyoinuliwa ambayo ndivyo alivyo.”4 Kama Mungu alivyosema, “Kwa maana tazama, hii ndiyo kazi yangu na utukufu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).
Maandiko ya Ziada
Mwanzo 1:26–27; 1 Wakorintho 3:17; Mafundisho na Maagano 130:1
Kutoka katika Maandiko
Kaka wa Yaredi katika Kitabu cha Mormoni akitafuta njia ya kuangaza mashua nane ambazo zilisanifiwa kuwabeba Wayaredi kuvuka maji hata nchi ya ahadi. “Alichoma mawe kumi na sita madogo kutoka kwa mwamba” na kuomba kwamba Mungu “ayaguse mawe haya” kwa kidole Chake “kwani yaweze kung’aa katika giza.” Na Mungu “alinyoosha mbele mkono wake na kugusa yale mawe moja moja.” Na pazia lilitolewa machoni mwa kaka ya Yaredi, na “akaona kidole cha Bwana; na kilikuwa kama kidole cha mtu….
Na Bwana akamwambia: “Utaamini maneno ambayo nitayasema?”
“Naye akajibu: Ndio, Bwana.”
Na “Bwana kisha akajionyesha kwa [kaka ya Yaredi]” na kusema, “Je, unaona kwamba uliumbwa kwa mfano wangu? Ndio, hata watu wote waliumbwa katika mwanzo kwa jinsi ya kama maumbile yangu.” (Ona Etheri 3:1–17.)
© 2016 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/15. Tafsiri iliidhinishwa: 6/15. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, March 2016. Swahili 12863 743.