“Wafu Watasimama Mbele za Mungu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Des. 2023.
Ujumbe wa kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Desemba 2023
Wafu Watasimama Mbele za Mungu
Katika ufunuo wake, Yohana aliona Hukumu ya Mwisho.
Wafu wakubwa kwa wadogo watasimama mbele za Mungu
Uweza wa Ufufuko wa Yesu Kristo unawaleta watu wote katika uwepo wa Mungu ili wahukumiwe (ona Alma 11:42–44; 33:22; 40:21; Helamani 14:15–17; Mormoni 9:13–14).
na vitabu vilifunguliwa
Vitabu hivi vinawakilisha kumbukumbu zinazotunzwa duniani za mambo ambayo watu walifanya duniani katika kufuata njia ya agano (ona Mafundisho na Maagano 128:7).
kitabu cha uzima
“Kwa namna moja Kitabu cha Uzima ni jumla ya mawazo, na matendo ya mtu—kumbukumbu ya maisha yake. Hata hivyo, maandiko pia yanaonyesha kwamba kumbukumbu za kimbingu zinatunzwa kwa walio waaminifu, ikijumuisha majina yao na kumbukumbu za matendo yao ya haki” (Mwongozo wa Maandiko, “Kitabu cha Uzima,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org).
hukumiwa
Hukumu ya Mwisho inakuja baada ya watu kuwa wamefufuka. Yesu Kristo atakuwa Hakimu wa kila mtu. Hukumu hii itaamua utukufu wa milele atakaopokea kila mtu. (Ona Mwongozo wa Maandiko, “Hukumu ya Mwisho,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org; Alma 41:3–5; Mafundisho na Maagano 88:26–32.)
kulingana na matendo yao
Kila mtu atahukumiwa kwa yale waliyofanya na kile walichotamani kufanya (ona Mafundisho na Maagano 137:9). Watahukumiwa kulingana na ikiwa walikuwa watiifu katika amri za Mungu na walitenda kulingana na nuru na ukweli wowote walioupokea katika maisha haya.
© 2023 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19 Tafsiri ya Monthly For the Strength of Youth Message, December 2023. Language. 19049 743