Liahona
Tumeitwa Kutenda Mema
Juni 2024


“Tumeitwa Kutenda Mema,” Liahona, Juni 2024.

Ujumbe wa kila mwezi wa jarida la Liahona, Juni 2024

Tumeitwa Kutenda Mema

Tunaujenga ufalme wa Mungu tunapowatumikia wengine, tunapoinua juu nuru yetu, na kutetea uhuru wa dini.

Gideoni alitambua mafundisho ya uongo alipoyasikia. Aliyasikia hapo mwanzoni kutoka kwa mfalme Nuhu na makuhani wake—makuhani ambao “walijiinua kwa kiburi cha mioyo yao” na ambao “walisaidiwa katika uvivu wao, na katika ukahaba wao, na ukafiri wao, kwa zile kodi ambazo mfalme Nuhu aliwatoza watu wake” (Mosia 11:5–6).

Kibaya zaidi, Mfalme Nuhu alimhukumu nabii Abinadi kufa na alitafuta kumwangamiza Alma na watu wake walioongoka (ona Mosia17; 18:33–34). Ili kukomesha uovu wa jinsi hiyo, Gideoni aliapa kumuua mfalme, ambaye alimwacha hai kwa sababu ya uvamizi wa Walamani (ona Mosia 19:4–8).

Baadaye, Gideoni kwa usahihi aliwalaumu makuhani wa Nuhu kwa kuwateka mabinti 24 wa Walamani. Aligundua kwamba unabii wa Abinadi dhidi ya watu wale ulikuwa umetimia kwa sababu walikataa kutubu. (Ona Mosia 20:17–22.) Alisaidia kuwakomboa watu wa Limhi, waliokuwa utumwani kwa Walamani (ona Mosia 22:3–9).

Sasa akiwa mzee zaidi, Gideoni alikabili vyote, kiburi na uovu kwa mara nyingine tena aliposimama mbele ya Nehori, ambaye alianzisha ukuhani wa uongo miongoni mwa watu. Nehori alikuwa “akilivunja Kanisa na akijaribu kuwaongoza watu kwenye upotofu. (Ona Alma 1:3, 7, 12; ona pia 2 Nefi 26:29.)

Akitumia neno la Mungu kama silaha, shujaa Gideoni alimwonya Nehori kwa sababu ya uovu wake. Akiwa amekasirika, Nehori alimshambulia na kumuua Gideoni kwa upanga wake. (Ona Alma 1:7–9.) Hivyo ndivyo zilivyoisha siku za “mtu mwenye haki” ambaye alikuwa “amefanya wema mwingi miongoni mwa watu hawa” (Alma 1:13).

Siku za mwisho tunazoziishi zinatupa fursa nyingi za kumuiga Gideoni kama “chombo mikononi mwa Mungu” (Alma 1:8) kwa kuwa “wenye kuhudumu” (Mosia 22:4) kwa wengine, kutetea haki, na kuhimili vitisho kwenye uhuru wetu wa kuabudu na kumtumikia Mungu. Tunapofuata mfano wa uaminifu wa Gideoni, sisi pia tunaweza kufanya mengi yaliyo mema.

Picha
mwanamke mwenye sinia la chakula akiwa amesimama pembeni ya mwanamke aliyelala kitandani

Kuungana katika Huduma

“Kama wafuasi wa [Mwokozi], tunatafuta kumpenda Mungu na majirani zetu kote ulimwenguni,” Urais wa Kwanza umesema. “Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lina hamu ya kuwabariki wengine na kuwasaidia wale wenye shida. Tumebarikiwa kuwa na uwezo, rasilimali, na miunganiko ya kuaminika ulimwenguni katika kutimiza jukumu hili takatifu.”1

Ninayo shukrani kwa huduma na utumishi usio wa kibinafsi ambao waumini wa Kanisa wanatoa katika mahekalu yetu, na katika kata na matawi na vigingi vyao. Ninayo shukrani pia kwamba waumini wa Kanisa wanatoa huduma katika jumuiya zisizo na idadi, taasisi za kielimu, na taasisi za hisani na kwamba wanajihusisha katika maelfu ya miradi ya kibinadamu kila mwaka, wakijitolea mamilioni ya saa kwenye nchi na majimbo takribani 200.2

Njia mojawapo ya Kanisa kutanua fursa za kuhudumu katika nchi mbalimbali ni kupitia JustServe.org. Ikifadhiliwa na Kanisa lakini ikipatikana kwa mtu yeyote anayetaka kuwabariki wengine, JustServe.org “inaunganisha mahitaji ya kujitolea ya jumuiya na wenye kujitolea” ambao “wanainua ubora wa maisha katika jumuiya.”3

Kanisa na waumini wake pia wanashirikiana na taasisi zingine za huduma kote ulimwenguni. Kanisa, shukrani kwa waumini wake, lilikuwa “mchangiaji pekee mkubwa wa harakati za Msalaba Mwekundu za kuchangia damu katika mwaka 2022.” Kwa nyongeza, Kanisa hivi karibuni lilifanya mchango wa $8.7 milioni kwa Msalaba Mwekundu.4

Kanisa pia linaungana na taasisi mbalimbali katika miradi ya kuleta maji safi na salama kwenye maeneo mbalimbali ulimwenguni. Katika mwaka 2022, Kanisa lilishiriki katika miradi ipatayo 158 ya aina hiyo.5 Pia tunashirikiana katika kazi na tunatoa mchango kwa mawakala wengine ambao wanatoa misaada kwa watoto wa Mungu wanaoteseka.6

“Tunapoungana mikono ili kuwahudumia watu walio katika shida,” alisema Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, “Bwana anaunganisha mioyo yetu.”7

Picha
Mikono kwenye umbo la mwumiko ikiwa na mwanga wa jua

Inua Juu Nuru Yako

Kama wafuasi wa Mwokozi, pia tunawabariki majirani zetu tunaposhika maagano yetu na kuishi maisha kama ya Kristo. Kitabu cha Mormoni kinafundisha kwamba “watu wa Kanisa” siyo lazima wachague haki bali pia wafanye sauti zao za haki zisikike kama wanataka Bwana awalinde na kuwastawisha (ona Alma 2:3–7; ona pia Mosia 29:27). Bwana anatutegemea tushiriki imani na kusadiki kwetu na kuinua juu nuru yetu. “Tazama Mimi ni mwangaza ambao mtainua” (3 Nefi 18:24).

“Hatumtumikii Mwokozi wetu vyema kama tunamwogopa mwanadamu zaidi kuliko Mungu,” alisema Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza. Aliongeza, “Tumeitwa ili kuweka viwango vya Mwokozi, siyo kuufuata ulimwengu.”8

Iwe shuleni, kazini, au michezoni, likizoni, kwenye miadi au mtandaoni, wafuasi wa Bwana “hawaoni aibu kujichukulia juu yao jina la Kristo” (Alma 46:21). Kwa maneno na matendo yetu, tunatoa ushahidi kwamba Mungu yu hai na kwamba tunamfuata Mwana Wake.

“Imani yetu haijagawanywa, au kwa hakika haipaswi kugawanywa. Imani siyo tu kwa ajili ya Kanisa, siyo tu kwa ajili ya nyumbani, siyo tu kwa ajili ya [shuleni],” alisema Paul Lambert, Mtakatifu wa Siku za Mwisho ambaye ni mtaalamu wa mambo ya dini. “Ni kwa ajili ya kila kitu unachokifanya.”9

Hatujui matokeo ya ushuhuda wetu, mfano wetu mwema, na matendo yetu mema yanachoweza kuwa kwa wengine. Lakini tunaposimama kwa ajili ya haki na kuinua juu nuru ya Mwokozi, watu watatutambua na mbingu zitatushangilia.

Picha
mwanamke akiwa amesimama nje ya hekalu

Tetea Uhuru wa Dini

Leo ukuhani wa uongo, pamoja na jamii zinazozidi kuwa za kidunia kuwadharau watu wa imani, siyo tofauti na zile za nyakati za Kitabu cha Mormoni. Sauti za wale wanaopinga kazi muhimu za dini katika umma na katika majukwaa ya kisiasa ziko juu sana. Watu wasio na dini na serikali, ikijumuisha shule nyingi na vyuo vikuu, vinalazimisha mwenendo na kugeuza imani kuwa ukosefu wa maadili, kutoamini kuwa kuna Mungu, na dhana kwamba hakuna kanuni ya kuamua ikiwa jambo ni jema au ovu.

Mashambulizi juu ya uhuru wa dini yatafanikiwa kama hatutasimama kutetea haki zetu za dini. “Kama kanisa,” hivi karibuni nilifundisha, “tunaungana na dini zingine kuwalinda watu wa imani zote na maoni na haki yao ya kuzungumza imani zao.”10

Vita mbinguni vilipiganwa juu ya maadili ya haki ya kujiamulia—uhuru wetu wa kuchagua. Ili kuilinda haki yetu ya kujiamulia inahitaji kwamba tuwe na bidii katika kulinda uhuru wetu wa dini.

Imani thabiti ya dini inaimarisha na kulinda familia, jumuiya, na mataifa. Inaleta utii kwa sheria, inadumisha heshima kwenye uhai na mali, na inafundisha hisani, uaminifu, na maadili—utu wema unaohitajika ili kuendeleza jumuiya ya haki, huru, na ya kiraia. Hatuhitaji kamwe kuomba radhi kwa ajili ya imani yetu.

Juhudi zetu za kimisionari, ibada zetu kwa niaba ya wafu katika mahekalu, juhudi zetu za kuujenga ufalme wa Mungu, na furaha yetu ya kweli vinahitaji kwamba tutetee imani yetu na uhuru wetu wa dini. Hatuwezi kupoteza uhuru huo pasipo kupoteza uhuru mwingine.

Nabii Joseph Smith alifundisha, “Ni mapenzi ya uhuru ambayo huivutia nafsi yangu—uhuru wa kisiasa na dini kwa jamii yote ya mwanadamu.”11 Uhuru wa dini utavutia pia nafsi zetu karidi ambavyo tunafuata ushauri wa viongozi wetu wa Kanisa:

  • “Pata habari kuhusu mambo muhimu ya umma, na kisha zungumza kwa ujasiri na ustaarabu.”12

  • “Tambua kwamba mmomonyoko wa uhuru wa dini kwa kiasi kikubwa utaathiri fursa yetu ya kukua katika nguvu na ufahamu wa injili, kubarikiwa kupitia ibada takatifu, na katika kumtegemea Bwana kuliongoza Kanisa Lake.”13

  • “Simama na uzungumze kuthibitisha kwamba Mungu yupo na kwamba kuna ukweli kamili ambao amri Zake huuthibitisha.”14

  • “Toa changamoto kwenye sheria ambazo zitalemaza uhuru wetu wa kutenda kulingana na imani yetu.”15

  • “Nendeni ulimwenguni mkafanye mema, mkajenge imani katika Mungu Mwenyezi, na kusaidia kuwaleta wengine mahali palipo na furaha zaidi.”16

  • Nyenzo za kujifunzia kwenye religiousfreedom.ChurchofJesusChrist.org na kwenye religiousfreedomlibrary.org/documents.

Tunaujenga ufalme wa Mungu tunapohudumu, tunapoinua juu nuru yetu, na kutetea uhuru wa dini. Naomba Bwana atubariki katika juhudi zetu za kufanya “wema mwingi” miongoni mwa familia zetu, jumuiya, na mataifa.

Muhtasari

  1. “Ujumbe kutoka Urais wa Kwanza,” katika Caring for Those in Need: 2022 Annual Report of The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 3, ChurchofJesusChrist.org.

  2. Ona Caring for Those in Need: 2022 Annual Report, 4, ChurchofJesusChrist.org.

  3. Justserve.org/about. JustServe iko hai katika mataifa 17. Maelfu ya watu na taasisi zinabarikiwa kupitia mpango huu.

  4. Ona Kaitlyn Bancroft, “Church Donates $8.7 M as Part of Red Cross Collaboration,” Church News, Apr. 22, 2023, 23.

  5. Ona Mary Richards, “Church Joins with Groups around the World to Tap into the Gift of Water,” Church News, Mei 27, 2023, 12.

  6. Ona Dallin H. Oaks, “Kuwasaidia Masikini na Wanaoteseka,” Liahona, Nov. 2022, 6–8.

  7. Henry B. Eyring, “Fursa za Kutenda Mema,” Liahona, Mei 2011, 25.

  8. Dallin H. Oaks, “Huduma Isiyo na Ubinafsi,” Liahona, Mei 2009, 94–95.

  9. Paul Lambert, katika Rachel Sterzer Gibson, “Why Is There a Need for Faith in the Workplace?” Church News, Apr. 22, 2023, 16.

  10. Ronald A. Rasband, “Kuuponya Ulimwengu,” Liahona, Mei 2022, 92.

  11. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2011), 345.

  12. D. Todd Christofferson, “Religious Freedom—A Cherished Heritage to Defend” (address at Freedom Festival Patriotic Service, Provo, Utah, June 26, 2016), 5–6, speeches.byu.edu.

  13. Ronald A. Rasband, “Free to Choose” (Brigham Young University devotional, Jan. 21, 2020), 3, speeches.byu.edu.

  14. Dallin H. Oaks, “Truth and Tolerance” (Brigham Young University devotional, Sept. 11, 2011), 2, speeches.byu.edu.

  15. Dallin H. Oaks, “Ukweli na Uvumilivu,” 4.

  16. Ronald A. Rasband, “Free to Choose,” 5, speeches.byu.edu.

Chapisha