Njoo, Unifuate
Kiambatisho D: Kwa ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana—Ajenda ya Mkutano.


“Kiambatisho D: Kwa ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana—Ajenda ya Mkutano,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Kiambatisho D,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Kiambatisho D

Kwa ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana—Ajenda ya Mkutano.

Tarehe ya mkutano:

Mwendeshaji (mshiriki wa darasa au urais wa akidi):

Ufunguzi

Wimbo (si lazima):

Sala:

Rejelea Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni.

Shaurianeni pamoja

Wakiongozwa na mtu anayeendesha mkutano, darasa au akidi hutumia dakika kama 5 hadi 10 kushauriana pamoja kuhusu wajibu wao katika kazi ya wokovu na kuinuliwa. Hii ni fursa kwa ajili ya urais wa darasa au wa akidi kufuatilia mambo yaliyojadiliwa katika mkutano wa urais au mkutano wa kata wa baraza la vijana.

Mtu mwenye kuendesha angeweza pia kutumia moja au zaidi ya maswali haya.

Kuishi injili

  • Ni tukio gani la hivi karibuni limeimarisha shuhuda zetu juu ya Yesu Kristo na injili Yake?

  • Je, tunafanya nini ili kusogea karibu zaidi na Mwokozi? Ni kwa jinsi gani tunajaribu kuwa zaidi kama Yeye?

  • Ni kwa jinsi gani tumehisi mwongozo wa Bwana katika maisha yetu?

Kuwajali wale walio katika shida

  • Ni nani tumehisi kuongozwa kumsaidia au kumhudumia? Ni majukumu yapi tumeyapokea kutoka kwa uaskofu ili kumsaidia mtu aliye na shida?

  • Je, ni changamoto gani washiriki wa darasa au akidi yetu wanakabiliwa nayo? Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana katika mambo tunayoyapitia?

  • Je, Kuna mtu amehamia karibuni kwenye kata yetu au kujiunga na Kanisa? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wahisi kukaribishwa?

Kuwaalika watu wote waipokee injili

  • Ni kitu gani tunaweza kufanya ili kuwasaidia wengine wahisi upendo wa Mungu?

  • Je, kuna shughuli gani zinazotarajiwa ambazo tunaweza kuwaalika marafiki zetu wahudhurie?

  • Ni mipango gani ya kushiriki injili imejadiliwa katika mikutano ya baraza la vijana la kata? Ni kwa jinsi gani darasa letu au akidi yetu inaweza kushiriki?

Kuziunganisha familia milele

  • Ni kwa njia gani tunaweza kuunganika vyema na wanafamilia, ikijumuisha babu na bibi na binamu zetu?

  • Tunafanya nini ili kupata majina ya mababu zetu ambao wanahitaji ibada za hekaluni? Tunaweza kufanya nini ili tuwasaidie wengine wapate majina ya mababu zao?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kushiriki zaidi katika kazi ya hekaluni—binafsi, na kama darasa au akidi?

Jifunzeni Pamoja

Kiongozi mtu mzima au mshiriki wa akidi au darasa huongoza maelekezo kuhusu kusoma Njoo, Unifuate kwa wiki hii. Wanatumia mawazo ya kujifunza katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani. Wazo la kujifunza lenye ikoni hii ikoni ya seminarilinaenda sambamba na seminari na linafaa hasa kwa vijana. Hata hivyo, wazo lolote la kujifunza linaweza kutumika. Sehemu hii ya mkutano kwa kawaida huchukua dakika 35 hadi 40.

Kufunga

Mtu anayeendesha mkutano:

  • Anatoa ushuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Anajadili jinsi gani darasa au akidi watakavyotenda juu ya kile ambacho wamejifunza—kama kundi au mtu binafsi.

Sala: