“Somo la 14: Kazi na Ajira,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 14,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 14
Jobs and Careers
Shabaha: Nitajifunza kuzungumza kuhusu kazi ya mtu na wapi wanafanya kazi.
Personal Study
Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: You Are a Child of God
Wewe ni mtoto wa Mungu
I am a child of God with eternal potential and purpose.
Mimi ni mtoto wa Mungu aliye na uwezekano wa kuwa na kusudi la milele.
Wewe ni binti au mwana wa Baba wa Mbingunimwenye upendo. Yeye atakuongoza. Kwa msaada wake, unaweza kufanya zaidi kuliko ambavyo ungeweza kufanya wewe mwenyewe. Katika Kitabu cha Mormoni, tunajifunza kuhusu mvulana aliyeitwa Nefi ambaye alikuja kuwa nabii-kiongozi wa watu wake. Mungu alitaka kumwongoza Nefi na watu wake hadi kwenye nchi mpya. Nchi hii ilikuwa ng’ambo ya bahari, na Nefi alipaswa kujenga mashua. Hakuwahi kujenga mashua awali. Kaka zake hawakuamini angeweza kufanya hivyo. Nefi alimtegemea Mungu kwa ajili ya maelekezo.
Nefi aliwaambia kaka zake, “ikiwa [Mungu] … amefanya miujiza mingi miongoni mwa watoto wa watu, je, kwa nini hawezi kunishauri, kwamba nijenge merikebu?” (1 Nefi 17:51).
Kwa msaada wa Mungu, Nefi na familia yake walijenga merikebu na kufanya safari iliyo ngumu ya kuvuka bahari. Kama tu vile Mungu alivyomsaidia Nefi, Mungu anataka kukusaidia wewe. Unaweza kusali kwa ajili ya maelekezo. Unaweza kusali ili kuelewa na kukumbuka kitu unachojifunza. Unaposali, kuwa msikivu kwa ajili ya mawazo na hisia ambazo zitakuja. Kisha tenda kwa imani. Unaweza kufanya zaidi kwa msaada Wake kuliko bila msaada huo.
Ponder
-
Je, safari yako ya kujifunza Kiingereza inafananaje na hadithi ya Nefi kujenga merikebu?
-
Unapojifunza Kiingereza, unaweza kumuomba Mungu kitu gani ili akusaidie?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno hayo katika maisha yako. Fikiria kuhusu lini na wapi ungetumia maneno haya.
job |
kazi |
Nouns 1
factory |
kiwanda |
hospital |
hospitali |
office |
ofisi |
restaurant |
mgahawa |
school |
shule |
store |
duka |
Nouns 2
accountant |
mhasibu |
artist |
msanii |
cashier |
keshia |
computer programmer |
mtengeneza programu za kompyuta |
cook |
mpishi |
custodian |
mtunzaji |
doctor |
daktari |
electrician |
fundi umeme |
factory worker |
mfanyakazi wa kiwandani |
farmer |
mkulima |
lawyer |
mwanasheria |
mechanic |
fundi mitambo |
nurse |
nesi |
office worker |
mfanyakazi wa ofisini |
salesperson |
mtu wwa mauzo |
server |
mhudumu |
teacher |
mwalimu |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: Where do you work?A: I work at a (noun 1).
Examples
Q: Where do you work?A: I work at a hospital.
Q: Where does she work?A: She works at an office.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kusema mipangilio kwa sauti. Fikiria kujirekodi mwenyewe. Zingatia matamshi yako na ufasaha wake.
Q: What’s your job?A: I’m a (noun 2).
Examples
Q: What’s your job?A: I’m a nurse.
Q: What’s his job?A: He’s an electrician.
Q: What’s her job?A: She’s an artist.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kazi ya kila mtu. Chukueni zamu.
Example: Carlos
-
A: Where does Carlos work?
-
B: He works at a school.
-
A: What’s his job?
-
B: He’s a teacher.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Uliza na ujibu maswali kuhusu kazi yako na mahali unapofanya kazi. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
New Vocabulary
home |
nyumbani |
student |
mwanafunzi |
university |
chuo kikuu |
Example
-
A: What’s your job?
-
B: I’m an electrician.
-
A: Where do you work?
-
B: I work at factory.