Vitabu vya Maelekezo na Miito
34. Fedha na Ukaguzi


“34. Fedha na Ukaguzi,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho (2020)

“34. Fedha na Ukaguzi,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

34.

Fedha na Ukaguzi

34.9

Ukaguzi

34.9.5

Upotevu, Wizi, Ubadhirifu au Matumizi Mabaya ya Fedha za Kanisa

Ikiwa fedha za Kanisa zimepotea au kuibiwa, au kama kiongozi amefanya ubadhirifu au ametumia vibaya fedha za Kanisa, rais wa kigingi au mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi ya kigingi anapaswa kutaarifiwa mara moja. Yeye anaitaarifu Idara ya Ukaguzi ya Kanisa (au mthibiti wa eneo ikiwa kitengo kipo nje ya Marekani au Kanada). Idara ya Ukaguzi ya Kanisa (au mthibiti wa eneo) anatuma fomu ya ripoti ya upotevu kwa rais wa kigingi au mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi. Chini ya maelekezo ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa (au mthibiti wa eneo), rais wa kigingi au mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi anahakikisha kwamba swala limechunguzwa kikamilifu na fomu ya upotevu imekamilishwa kikamilifu na imewasilishwa.

Kama matumizi makubwa mabaya ya fedha yamegundulika, rais wa kigingi au mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi anamtaarifu pia Rais wa Eneo.

Chapisha