Mkutano ya Uongozi wa Mkutano Mkuu
Mafunzo ya Uongozi kwa Aprili 2021


scenes of people participating in ordinances

Fungamana na Mwokozi kupitia Maagano na Ibada

Mafunzo haya ya uongozi yalitambulishwa wakati wa mkutano mkuu wa uongozi wa Aprili 2021.

Muhtasari wa mafunzo kwa ajili ya mabaraza ya uratibu ya Eneo, Misioni, Kigingi, Kata, na Tawi

Wakati wa mafunzo haya, utaona na kusikia uzoefu wa watoto wa Baba yetu wa Mbinguni katika sehemu tofauti tofauti wakiwa kwenye njia ya kufungamana na Mwokozi kupitia maagano na ibada. Utasikia jinsi upendo, kushiriki, na kualika kumewasaidia wao kuendelea katika njia ya agano kwa furaha. Unaweza kutambua jinsi gani kushiriki injili, kazi ya hekaluni na historia ya familia, na kuwajali wenye shida vyote vinavyochangia. Lakini juu ya yote, unaweza kugundua jinsi vitu hivi vyote “vitakavyojumlishwa vyote … katika Kristo” (Waefeso 1:10).

Maisha hatua ya 1: Watoto

Tazameni video ya Rais Joy D. Jones na watoto, na kisha jadilini ni nini mtakwenda na kufanya ili kuwasaidia watoto kufungamana wao wenyewe na Mwokozi kwenye njia ya agano.

8:0
  • Je, Roho alitufundisha nini wakati tukiangalia video hii?

  • Je, ni kwa namna gani kanuni za upendo, kushiriki, na kualika huwasaidia watoto wanapojitahidi kushiriki injili?

  • Je, ni kwa namna gani huduma huwasaidia watoto kubaki kwenye njia ya agano baada ya ubatizo?

Msichana akiwasomea wazazi akiwa juu ya kochi

Maisha hatua ya 2: Vijana

Tazameni video ya Rais Bonnie H. Cordon na Rais Stephen J. Lund na vijana, na kisha jadilini ni nini mtakwenda na kufanya ili kuwasaidia vijana kufungamana wao wenyewe na Mwokozi kwenye njia ya agano.

7:59
  • Je! tunawezaje kuwasaidia vijana kuyashika maagano yao ya ubatizo na kujiandaa kwa hatua inayofuata kwenye njia ya agano?

  • Je, ni kwa namna gani kanuni za upendo, kushiriki, na kualika huwasaidia vijana kushiriki katika kazi ya hekaluni na historia ya familia?

  • Je! tunawezaje kuwasaidia vijana kuhisi matumaini na kuhisi kuwa sehemu ya, wakati wanapokuwa wamefungamana na Mwokozi?

Maisha hatua ya 3: Vijana Wakubwa

Tazameni video ya Rais Mark L. Pace na vijana wakubwa, na kisha jadilini ni nini mtakwenda na kufanya ili kuwasaidia vijana wakubwa kufungamana wao wenyewe na Mwokozi kwenye njia ya agano.

9:2
  • Je, tunajifunza nini kutokana na upendo, kushiriki, na kualika ambavyo wengine hutupatia?

  • Je, tunawezaje kuwasaidia vijana wakubwa kuhisi matumaini na kuwa sehemu ya, wakati wanapoongezeka katika kujitegemea na kuwatumikia wengine? Je, tunawezaje kuwasaidia kujua kwamba wao wanahitajika katika Kanisa la Bwana?

  • Je, shughuli za Kanisa na viongozi wenye kujali wana jukumu gani katika kuwafungamanisha vijana wakubwa na Mwokozi?

Maisha hatua ya 4: Watu Wazima

Tazameni video ya Rais Jean B. Bingham na watu wazima, na kisha jadilini ni nini mtakwenda na kufanya ili kuwasaidia watu wazima kufungamana wao wenyewe na Mwokozi katika njia ya agano.

10:20
  • Je, ni kwa namna gani maagano yetu huleta uponyaji na kutusaidia kubakia kwenye njia—hata katika nyakati ngumu?

  • Ni njia zipi ambazo tumezipata za kuwasaidia waumini kufungamana wao wenyewe na wengine kwa Mwokozi kupitia maagano na ibada?

  • Ni kwa jinsi gani kukuza kujitegemea kwetu kiroho kunatusaidia sisi kupenda, kushiriki, na kualika?

Nyenzo kwa ajili ya mabaraza ya Eneo, Uratibu, Misioni, Kigingi, Kata na Tawi

Kwa ajili ya Watoto na Vijana

Maelezo ya Jumla kwa Watoto na Vijana

Programu ya Watoto na Vijana imeundwa ili kuimarisha imani ya kizazi kinachoinukia katika Yesu Kristo, na kuwasaidia watoto, vijana, na familia zao kuendelea mbele wakiwa kwenye njia ya agano wakati wanapokabiliwa na changamoto za kimaisha. Huwasaidia watoto na vijana katika juhudi zao za kushiriki katika kukusanya Israeli na kazi ya wokovu na kuinuliwa katika maisha yao ya kila siku. Inalenga nyumbani na kusaidiwa na kanisa.

familia ikipanda mlima

Matumaini kwa ajili ya Kizazi Kinachoinukia

Programu ya Watoto na Vijana husaidia kizazi kinachoinukia kukua katika njia nyingi, ikijumuisha kupitia ufunuo, haki ya kujiamulia, na mahusiano. Watu binafsi hujifunza kupokea na kufanyia kazi ufunuo binafsi wanapoifanyia kazi haki ya kujiamulia na kuchagua fursa za kukua kwa ajili yao wenyewe. Hii pia hutokea wakati vijana wanapojifunza kuongoza katika urais wa akidi na darasa. Wanajenga uhusiano na familia zao, viongozi wao, na wengine wa rika lao wanapofanya kazi na kuhudumu pamoja na kujua kwamba wao ni wa muhimu na wanahitajika katika kazi ya Bwana.

Je, Tunapaswa Kuanzia Wapi Leo?

Tunawaalika watoto, vijana, na wazazi na viongozi wao kujiwekea ahadi au kufanya upya tena ahadi ya kuwa zaidi kama Mwokozi kwa kushiriki katika kazi Yake. Jitihada hizi hazitakiwi kuwa ngumu! Hizi ni baadhi ya sehemu rahisi za kuanzia:

Wazazi
  • Ikusanye familia yako kwa ajili ya kujifunza injili. Nyenzo za Njoo, Unifuate zinaweza kusaidia. Unaweza kufikiria kuwa na majadiliano juu ya mada kama vile maagano, ufunuo, haki ya kujiamulia, na baraka za patriaki.

  • Panga shughuli ya familia. Je, unawezaje kwa usalama kumhudumia mtu katika mtaa au jumuiya yako? Pale ambapo, JustServe inapatikana, inaweza kukusaidia kupata mawazo.

  • Kutana na kila mwana na binti mmoja mmoja. Jadili masilahi yao na ongea juu ya jinsi wanavyotaka kukua. Saidia na unga mkono maendeleo yao binafsi. Ongea juu ya malengo gani wamejiwekea au wanataka kufanyia kazi.

Viongozi wa Msingi
  • Jua hali za nyumbani za watoto, na utafute ufunuo ili kuwasaidia kama watu binafsi.

  • Anza kufanya mikutano ya Jumapili na shughuli za Msingi ana kwa ana au kimtandao (ikiwa ni salama na imeidhinishwa).

  • Usijali kuhusu kuunganisha malengo ya watu binafsi na shughuli! Fokasi yako iwe juu ya kuwaunganisha na kuwabariki watoto na familia zao—hususan wanapokuwa na shida au wanapoomba msaada.

Watu wazima viongozi wa vijana
  • Anza kufanya mikutano ya Jumapili na ya akidi na shughuli za darasa ana kwa ana au kimtandao (ikiwa ni salama na imeidhinishwa). Watie moyo vijana kukariri na kuanza mikutano kwa dhima mpya ya darasa la Wasichana na akidi ya Ukuhani wa Haruni.

  • Waite na wasimike, uwezeshe urais wa akidi na wa darasa. Wasaidie kufanya mikutano ya mara kwa mara ya urais na kupanga na kuongoza mikutano ya Jumapili na shughuli. Fanyeni mabaraza ya vijana ya kata, na himiza ushiriki katika mikutano ya uratibu ya wamisionari na kazi za hekalu na historia ya familia. Shauri na saidia urais kadiri inavyowezekana bila ya wewe kuchukua nafasi yao. Saidia urais kujifunza stadi za uongozi kwa kutumia nyenzo za urais wa akidi na wa darasa.

  • Panga na kufanya kambi za vijana na mkutano wa vijana kwa mwaka 2021, kwa kufuata miongozo ya usalama.

  • Usijali kuhusu kuunganisha malengo ya watu binafsi na shughuli! Weka nguvu yako katika kuunganika na vijana wenyewe. Unaweza pia kusaidia urais wa akidi na wa darasa kuunganisha shughuli na mahitaji ya vijana.

Kwa maelezo zaidi, ona ChildrenandYouth.ChurchofJesusChrist.org.

Kwa ajili ya Watu Wazima

Sehemu za Kukusanyika za VWW

Urais wa Kwanza umetoa idhini kwa maeneo kuanzisha maeneo ya kukusanyika kwa vijana wakubwa waseja kulingana na mahitaji ya eneo. Mahali pa kukusanyika ni mahali palipoteuliwa katika jengo lililopo (kama vile nyumba ya mkutano au jengo la chuo) ambapo vijana wakubwa waseja na marafiki zao wanaweza kukusanyika kushiriki katika baadhi au shughuli zote zifuatazo (kulingana na mahitaji ya sehemu husika na nyenzo):

  • Elimu ya dini na kujifunza injili (ikiwemo chuo)

  • Huduma na shughuli za kijamii

  • Shughuli za hekalu na historia ya familia

  • Fursa za kujitegemea na za kielimu

  • Shughuli za umisionari na ufikiwaji wa jamii

  • Programu nyingine za Kanisa

Sehemu zote za kukusanyika lazima ziidhinishwe na Urais wa Eneo na kusimamiwa na marais wa vigingi na maaskofu.

Vijana wakiongea wao kwa wao

Miito kwa ajili ya Vijana Wakubwa Waseja na Watu Wazima Waseja

Mabadiliko ya sera ya hivi karibuni na ufafanuzi wake umesuluhisha hali ya uwezekano wa kutokuelewana na mila potofu kuhusu mipaka juu ya fursa za kuhudumu kwa waumini waseja katika Kanisa la Bwana. Mabadiliko haya ya sera na ufafanuzi wake, vilivyoidhinishwa na Urais wa Kwanza na Akidi ya wale Kumi na Wawili na kujumuishwa katika Kitabu cha Maelezo ya Jumla, yanaeleza kwamba vijana wakubwa waseja na watu wazima waseja wanaweza kubarikiwa kwa, na wanaweza kuwabariki wengine katika miito mingi, ikijumuisha kama viongozi wa kigingi na kata. Sera hizo hizo sasa zinafanya kazi katika matawi au kata zote za Kanisa, pamoja na kata au matawi yote ya vijana wakubwa waseja na watu wazima waseja. Vizuizi dhidi ya vijana wakubwa waseja na watu wazima waseja kuhudumu katika urais wa kigingi, uaskofu, na urais wa kigingi wa Muungano wa Usaidizi katika vitengo vya vijana wakubwa waseja na watu wazima waseja vimeondolewa.

Waumini wasio na wenzi wanaweza kutumikia katika nafasi za uongozi ikiwa ni pamoja na urais wa kata na kigingi, urais wa akidi ya wazee, washauri wa uaskofu, wajumbe wa baraza, na washauri wa urais wa kigingi.

Kuhitaji na Kukaribisha Vyote—Upendo, Kushiriki, na Kualika

Waumini wanapopambana ili kuhisi hali ya kuwa sehemu ya, nyakati zingine viongozi na wengine pasipo kukusudia husema vitu ambavyo huonyesha mkazo kwa waumini hawa kuamini kuwa hawastahili au hawahitajiki.

Vijana wakiongea wao kwa wao

Kukumbuka kweli hizi juu ya upendo, kushiriki, na kualika kunaweza kusaidia katika kuwakaribisha wote kwenye shughuli, ushirika, na kuwa wa Kanisa la Yesu Kristo:

  • Kila mtu ni mtoto mpendwa wa Mungu aliye na asili na hatma ya kiungu. Katika nyongeza ya baraka za milele anazowaahidi walio waaminifu, Yeye anataka kuwabariki watoto wake sasa, wakati wa maisha haya.

  • Kila mtoto wa Mungu anahitajika katika kazi ya kujenga ufalme Wake.

  • Ili kumsaidia mtu kuhisi yeye ni sehemu ya, na anahitajika, anza na upendo. Sikiliza ili kuelewa uzoefu wake. Usifikirie kuwa tayari unajua au unaelewa.

  • Hatuna majibu ya maswali yote ambayo sisi au wengine wanakabiliwa nayo katika maisha haya. Kwa mfano, sisi hatujui sababu za mtu fulani kukabiliwa na changamoto.

  • Kuwa muwazi na usihukumu. Mkaribishe kila mtu, popote mtu huyo alipo katika safari yake. Toa msaada, na zingatia ukweli kwamba kila mtu anahitajika katika Kanisa.

  • Ikiwa umesema bila kukusudia jambo lenye kuumiza, usijitetee; omba radhi kisha tafuta msamaha na kuwa bora.

Kwa maelezo kuhusu kuwasaidia waumini katika hali maalumu, ona Counseling Resources.

Jinsi Gani Uongofu Mmoja Ulivyokua na kuwa Kundi Kubwa la Akina Kaka

3:46

Kanuni za Upendo, Shiriki, na Alika

2:33

Tumeahidiwa baraka kadiri Tunavyopenda, Kushiriki, na Kualika

1:16